Jumababu
Senior Member
- Jan 11, 2013
- 146
- 132
Nimestushwa na kuogopa tena nikalazimika kuisoma Katiba ya Zanzibar mara mbili.
Leo Waislamu wa Zanzibar wanawavamia na kuwapiga vibaya Wazanzibar wenzao ambao sio Waislamu kwakuwa tu wanakula kwa mama lishe mchana mda ambao wale waislamu wanakuwa wamefunga,
Vipigo vimeenea kila kona ya mji wa Zanzibar na uhasama unakua kila kukicha, serikali ipo kwenye mfungo mtukufu, Wakristo hawa Wazanzibar hawana msaada, nani awaokoe vijana wa kikikristu ambao hawajao wanaotegemea kwa mama lishe na migahawani kupata mlo wao? Nao wafunge???
Nini tutarajie majibu ya wahanga hawa kama sio gharika? Serikali inasubiri kuunda tume baada ya mauaji??
Nimeisoma na kuipekua katiba ya Zanzibar kuona kama kuna kifungu kinachowapa haki waislamu kudhibiti uhuru wa watu wengine,
Zaidi nilitaja kujua kama Zanzibar ni nchi ya kidini au ni nchi inayotawaliwa kwakufuata sharia.
Sehemu mhimu ya katiba ya Zanzibar ni hii hapa, jioneeni kama ni haramu kula chakula hadharani nchini Zanzibar.
SURA YA KWANZA- ZANZIBAR
Sehemu ya Kwanza
1.Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
2. Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
3.(1) Kutakuwa na Muhuri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao alama yake itakuwa kama itavyokubaliwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
(2) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na uwezo wa kuweka kitu chochote kitachokuwa kielelezo cha Serikali kama itavyokubaliwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
4. Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.
5. Zanzibar itafuata mfumo wa Kidemokrasia wa Vyama Vingi vya Siasa wenye kuheshimu utawala wa sheria, haki za binaadamu, usawa, amani, haki na uadilifu.
5A.(1) Zanzibar itafuata mfumo wa mgawanyo wa madaraka kati ya mamlaka tatu, Mamlaka ya Utendaji, Mamlaka ya Kutunga Sheria na Kusimamia Utekelezaji wa Shughuli za Umma na Mamlaka ya Kutekeleza Utoaji Haki.
(2) Mamlaka ya Utendaji ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mamlaka ya kutunga Sheria na Kusimamia Utekelezaji wa Shughuli za Umma ni Baraza la Wawakilishi na Mamlaka ya Kutekeleza Utoaji Haki ni Mahkama.
(3) Hakuna mamlaka itakayoingilia Mamlaka nyengine isipokuwa kama na kwa kadri ilivyoelezwa katika Katiba hii.
Hii mada imekaa kigombanishi gombanishi. Hivi mtu unajisikiaje
Kutunga uongo? Au kuandika mada ili watu wafarakane? Hivi kweli ndo ulivyofunzwa na wazazi wako na walimu wako wa dini?
Sent from my iPhone using JamiiForums