Mkuu, lazima uheshimu utaratibu wa watu, wapo katika nchi ambayo almost 98% ni waislamu, hivo wanapaswa kuwa wastaarabu. Hata hivo nipo unguja, sijaskia wakiristo wakipigwa, hao mama ntilie wako wapi? Mi najua sehemu zinazouza chakula mchana na watu wanakula wala hawapigwi.... Ustaarabu kitu cha muhimu, utakaa maskani ule wakati wenzako wote wamefunga? Utafukuzwa tu, hawana wake he nyumba pia hawana? Hata hotel migahawa ya kitalii wanaustaarabu wa kufunika tambara ili anaepita asione. Kama upo unguja nenda six degrees south utaona walivoweka, ni mgahawa upo stone town. Wamefanya ustaarabu, kwanini wewe usiwe mstaarabu? Dini yenu haikufundishini ustaarabu? Mbona waislam walioko UK USA na kwengineko hawalalamikii wasio waislam wakila hadharani? Ni kwa sababu wanajua wapo katika nchi ya watu wengi wasiowaislam hivo na wao wanapaswa kuwaheshimu wanaokula hadharani