Kitendo cha kupitisha kanuni ya kuzuia mwandishi wa habari atakae andika habari ambazo si sahii kwa mwono wenu(wajumbe wa bunge la katiba) ni kujiwekea madaraka yasiyo yenu.
Tasinia ya habari inayomamlaka yake inayoweza fanya kazi hiyo, halikadhalika kama kutakuwa na kitu kikubwa cha kuwakwaza sana serikali kupitia mamlaka husika wataona nini cha kufanya. Napenda kuwakumbusha kazi yenu si kuwafatilia watu watakao wakosoeni au kueleza muono wao juu ya kazi zenu. ikumbukwe Bunge la katiba si muhimili hapa nchini hivyo liheshimu mihimili iliyopo hivyo si busara kujiwekea madaraka ambayo halina, kama kuna ambaye atawakwaza pelekeni taarifa mamlaka husika.
Tafadhalini! heshimuni kazi tuliyo wapa na tuna uhuru wa kupata taarifa yeyote ya yanayojiri humo ndani ili mwisho wa kazi yenu tukubali au tukatae kama wananchi.
SISI WANANCHI NDO WENYE MAAMUZI YA MWISHO SI NYINYI MSIJISAHAU.
Majukumu mema ya kuleta katiba bora.