Ndugu wana jamvi mwenye macho haambiwi tazama kwa ninavyoona mimi kinachoendelea bunge la katiba ikweli ni kwamba ccm haikuwa radhi tanzania kupata katiba iliyo bora na yenye maslahi ya taifa. Kwa nini nasema hivyo bila kukosea palishaundwa tume za katiba kama tatu kukusanya maoni ya wananchi na shauku ya wananchi ni kutaka serikali 3 angalao kuweza kupata kile walichokosa miaka 50 swali linakuja ninani anawapa hiyo nguvu ya kukinzana na matakwa na wananchi walio wengi ambao ndio wamewatuma kuikamilisha baada ya kutoa maoni yao ? Kwa nini hawataki kura ya siri ambayo itamfanya mtu kuwa huru kiakili kimsingi ccm kuna mchezo wanatuchezea sisi wananchi na hatutakubali watu kujiona miungu watu kuanza kutuchagulia kile tusichokitaka sisi wananchi sisi tumewatuma ninyi wabunge na taasisi nyingine kwenda kuitimiliza katiba nzuri sio kuitengua .