Yanayojiri Bunge Maalum la Katiba leo Tarehe 7.3.2014.

Yanayojiri Bunge Maalum la Katiba leo Tarehe 7.3.2014.

Mimi naomba tu hao jamaa ( bunge la katiba ) wachekiwe vizuri kuhusu matumizi ya viroba, maana hawasomeki.
 
Kwakweli inatusikitisha sana kuona kanuni tu imekua tatizo sasa itakapofika kwenye masuala ya kitaifa sijui itakuaje na huku mitaani wazee wa serikali za mitaa wanasema wanataka kuleta hoja ya kufutwa kwa serikali za mitaa sababu haijazungumziwa kwenye rasimu yaani vurugu tu sasa
 
Mimi naomba tu hao jamaa ( bunge la katiba ) wachekiwe vizuri kuhusu matumizi ya viroba, maana hawasomeki.

Nakubaliana nawe kwa mantiki kua mtu akitumia kilevi akili yake hupungua uwezo wa kufikiri na kumpambanua mambo. Hivyo kama kuna wajumbe wanatumia vilevi na kuingia ukumbini kwa ajili ya semina hawatutendei haki.

Kwa upande mwingine mi naona wajumbe wasio wabunge wana nguvu za hoja tofauti kabisa na wabunge wetu wa siku zote ambao wao hoja za nguvu ndio msingi wao. Jaribu kumsikiliza Mwalimu Oluwochi kisha umsikilize Mbunge Ole Sendeka kwa uchache kuthibitisha hoja yangu.

Maoni yangu ni kua wabunge wetu wa siku zote bila kujali itikadi za vyama vyao watulie, wawe wasikivu na nidhamu ili mjadala na mchakato uende vyema.
 
Heee! Wonders shall never end, kumbe tayari wazee wa watu walishakua waumini wa dini zile zilizokuja na meli?

Kama elimu na lugha, na siasa na demokrasia na mengine mengi yaliyoletwa na meli. Kama si hao wenye meli, hata leo kusingekuwa na watu Dodoma wanaandika katiba mpya, so far hata rais aliyeagiza mchakato wa katiba asingekuwepo maana kungekuwa na mangi, watemi, watwa n.k.
 
Mkuu mimi naheshimu sana ibada za watu,na ni haki yao wale wanapaswa kuswali kwenda kufanya hivo.
Hoja yangu ni kuwa semiba ilibidi ianze toka saa nne lakini wabunge wameanza kkao saa 5:25 , na baada ya dua tu wakaanza kudai bunge lihairishwe wanaenda kuswali,na.hata ambao hawaswali wametumia mwanya huo sasa kama walijua leo kuna swala kwa nn hawakuwahi? Kama wamekosa utii kwa taifa lao je watamtii Mungu?

Na kwanini waanze saa 4 huku wakijua wataenda kuswali?Hivi hawana uwezo wa kuanza kazi saa 2 angalau kwa kila ijumaa halafu saa 5 hiyo wakaenda msikitini?Wanafiki wakubwa hao

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kama elimu na lugha, na siasa na demokrasia na mengine mengi yaliyoletwa na meli. Kama si hao wenye meli, hata leo kusingekuwa na watu Dodoma wanaandika katiba mpya, so far hata rais aliyeagiza mchakato wa katiba asingekuwepo maana kungekuwa na mangi, watemi, watwa n.k.

Mkuu, kwa mawazo yangu na nionavyo mimi ni kwamba si vyote vilivyokuja na meli ni vizuri ama vibaya, hali kadhalika si vyote tulivyokuanavyo tangu enzi na enzi ni vibaya ama vizuri. Kwa kila upande kuna mabaya na mazuri ila tuchukue mazuri na kuacha mabaya kotekote.

Kwa kauli yangu hapo mwanzo (dini zilizokuja na meli) sikusema kwa ubaya ila nilimanisha kua wazee wetu tajwa hatimaye wameamua kufuata kilicho bora kwao tofauti na mwanzo walivyokua hasa mzee Kingunge. Natumaini umenielewa sasa.
 
Bunge la katiba limeniisha haumu mapema mno;
heri hata lile la yule bi mkubwa.
 
Hawa naona wapo kusaka umaarufu na kula hela tu. Wanakuwa kama watoto? Hata hawaheshimiani wao kwa wao.
 
Msingi wetu ni kuwapa ukweli wa mambo bila ushabiki hii ni kwa manufaa ya watanzania waliowengi ambao ndiyo wenye katiba yao.

Kwani nani aseyejua wewe ni shabiki na mkereketwa wa magamba?????????? Eleza utakayoyaeleza tutakuelewa tu
 
Mkuu mimi naheshimu sana ibada za watu,na ni haki yao wale wanapaswa kuswali kwenda kufanya hivo.
Hoja yangu ni kuwa semiba ilibidi ianze toka saa nne lakini wabunge wameanza kkao saa 5:25 , na baada ya dua tu wakaanza kudai bunge lihairishwe wanaenda kuswali,na.hata ambao hawaswali wametumia mwanya huo sasa kama walijua leo kuna swala kwa nn hawakuwahi? Kama wamekosa utii kwa taifa lao je watamtii Mungu?

Jamani
Watu wanataka kuongeza siku za kukaa, Dodoma, si mlipiga kelele za 700k kwa siku. Zitatimia tu....
 
Ule mvuke wake tu wakati wa kufanya titration nilikua sipendi hata kuusogelea, sasa leo solution yenyewe inatumika kuziba midomo walalahoi, inaumiza. Halafu mkuu hebu naomba umzungumzie Saidi Kubenea kwa ufupi sana.

yaliyomkuta ni jinamizi kwake,anaifahamu kidogo imfanye kipofu.
 
yaliyomkuta ni jinamizi kwake,anaifahamu kidogo imfanye kipofu.

Na yule kijana wa Igunga anayezunguka kwenye mikutano sasa na mchumi daraja la kwanza unaweza kunipa kisa chake?
 
Wajumbe%20Bunge%20Maalum%20la%20Katiba.jpg
 
Hao wabunge wa bunge la katiba sio wa kuwawekea shillingi. Hawaaminiki!
 
Kuna tetesi kwamba limevunjika ingawa kuna wakuu wanchi wamejaribu au wanajaribu kuingilia kati lakini hali ni tete ,hakuna habari imeruhusiwa kutoka ,hadi hivi sasa bado inabaki kuwa tetesi ,lakini wataficha mpaka lini ??
 
Mmh! Ngoja tusubiri...
 
Back
Top Bottom