Wadau,
Baada ya msimamizi kutaja majina ya walioomba kugombea uenyekiti wa Bunge maalum la Katiba ambapo walikuwa ni wanne kati yao ni wawili tu ndio wametimiza masharti ya kugombea. ambao ni Hasheem Rungwe na Samwel Sitta. Msimamizi amesema kura zitapigwa kwa mtindo wa SIRI.
Aliyeanza kujieleza ni Mh. Hasheem ambapo mwenyekiti wa muda alimtaka Mh. Sitta atoke nje ili Mh. Hasheem aanze kutoa maelezo yake na hatimae kuomba kura.
Mh. Hasheem alianza kwa kutoa maelezo yake na kubwa zaidi ni kwamba yeye ndiye mfanyabiashara wa kwanza kufanya biashara ya magari hapa Tanzania. Kisha akaomba kura ijapokuwa maelezo yake hakuyamaliza.
Ndipo alipofuta Mh. Sita nakueleza kuwa yeye ni mzee wa viwango na kasi. Kubwa zaidi ni pale aliposema wakimrudisha Sitta kwenye kiti cha Uspika ni sawa na kumrudisha chura kwenye dimbwi la maji.
Sasa kura za SIRI zinaanza kupigwa kwa kanuni ya nane ya mwaka 2012.