Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Lowasa nadhani alikuwa anawajulisha wana kambi yake wampigie kura Sita.
 
Na upigaji kura ni kuweka tiki kwenye jina moja tu na upigaji kura kwa wasiojiweza watasaidiwa makaratasi sehemu walipo. Wagombea ni Hashim Rungwe vs Samweli Sitta na hiyo ni baada ya wagombea wengine wawili kutokurudisha fomu. Katika hali isiyotarajiwa Sitta na Lowasa wameshikana mikono baada ya Mh. Sitta kumaliza kuomba kura kutoka kwa wajumbe
 
Manvi anatafuta kuungwa mkono atakapotangaza nia ya kugombea Urais
 
Masanduku yako tupu majani hakuna kura iliyotangulia.M.kiti wa muda wa BMK
 

Attachments

  • 1394631874326.jpg
    1394631874326.jpg
    62 KB · Views: 117
Huo uzi wa Sitta kuzushiwa anaumwa nimeuona huku jamvin..au kunagazeti lilichapisha.?
 
MAMBO YAMEIVA mzee SITTA mzee wa VIWANGO NA SPIDI - uchaguzi ndio umeanza sasa
 
!Natumaini ikitokea chama chake kikamsimamisha kugombea urais mwakani, vyama vyote vionyeshe mshikamano wa kumuunga mkono kama ilivyo sasa.
 
Pointi sio njema kwa kweli:
"kuna kikundi cha watu wachache wanataka kuunjia mbali muungano wetu, sitta kasema atawashughulia ipasavyo na hayupo tayari kuona muungano uliodumu kwa miaka 50 ukivunjwa na watu kama hao.

Kauli hii imenitia shaka sana!
 
Pointi sio njema kwa kweli:
"kuna kikundi cha watu wachache wanataka kuunjia mbali muungano wetu, sitta kasema atawashughulia ipasavyo na hayupo tayari kuona muungano uliodumu kwa miaka 50 ukivunjwa na watu kama hao.

'kikundi cha watu wachache' huenda anamaanisha CDM...ni matumizi YA tafsidah tu.
 
Anayetarajiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa bunge malumu la katiba samweli sita ameweka wazi msimamo wake kuwa anataka mfumo wa serekali mbili hayo ameyasema jion hii mjini dodoma akiwa anajieleza mbele ya bunge malumu
 
Wadau,

Baada ya msimamizi kutaja majina ya walioomba kugombea uenyekiti wa Bunge maalum la Katiba ambapo walikuwa ni wanne kati yao ni wawili tu ndio wametimiza masharti ya kugombea. ambao ni Hasheem Rungwe na Samwel Sitta. Msimamizi amesema kura zitapigwa kwa mtindo wa SIRI.

Aliyeanza kujieleza ni Mh. Hasheem ambapo mwenyekiti wa muda alimtaka Mh. Sitta atoke nje ili Mh. Hasheem aanze kutoa maelezo yake na hatimae kuomba kura.

Mh. Hasheem alianza kwa kutoa maelezo yake na kubwa zaidi ni kwamba yeye ndiye mfanyabiashara wa kwanza kufanya biashara ya magari hapa Tanzania. Kisha akaomba kura ijapokuwa maelezo yake hakuyamaliza.

Ndipo alipofuta Mh. Sita nakueleza kuwa yeye ni mzee wa viwango na kasi. Kubwa zaidi ni pale aliposema wakimrudisha Sitta kwenye kiti cha Uspika ni sawa na kumrudisha chura kwenye dimbwi la maji.

Sasa kura za SIRI zinaanza kupigwa kwa kanuni ya nane ya mwaka 2012.
 
Baadhi ya wabunge wakipiga kura kumchagua mwenyekiti
image.jpg
 
Back
Top Bottom