CCM na washirika wao wanaendelea kutoa vijembe na hoja dhaifu. Kwanza wanalalama wapinzani kuungana. Wapinzani kuungana si ajabu hata Zanzibar CCM na CUF wameungana licha ya kuwa mahasimu kwa miaka mingi sana. Vyama vina sera tofauti. Tofauti hizi zinakuwepo pale vinapotafuta kuungwa mkono na wananchi katika sera zao. Lakini kwa suala lenye masrahi ya kitaifa lazima watanzania waungane bila kujali itikadi za vyama vyao.
CCM ndo wanawagawa watanzania katika misingi ya vyama vyao ili wapitishe mambo yasiyo na masrahi kwa taifa ili waendelee kupora fedha na rasrimali za wananchi. Ndo maana wanalalama sana na kuona nongwa kuona CUF, NCCR-Mageuzi na CHADEMA wameungana lakini cha kusikitisha CCM hao hao hawakulalama wakati CUF na CCM walipoungana ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.
Kuhusu gharama za muungano, wizara za muungano zipo hakuna itakayoongezwa. Na kwa muundo wa serikali mbili kuna wabunge zaidi ya 70 wanaotoka zanzibar. Na kwa maana hiyo ili kuweka usawa kati ya bara na visiwaani, inamaana kuna wabunge zaidi ya 70 toka Tanzania bara kufanya idadi ya wabunge zaidi ya 140 wanaoshughulika na mambo ya muungano. Gharama hizi CCM hawazioni kama ni mzigo kwa watanzania. Lakini muundo unaopendekezwa katika rasimu, bunge la muungano litakuwa na wabunge 75 tu wa muungano. Zaidi ya wabunge 65 watapungua katika bunge la muungano. Sasa swali la kujiuliza ni hili: Je, nafasi mbili (2) au Tatu (3) za rais, makamu au na waziri mkuu wa Tanganyika ndo zitachukua gharama za wabunge zaidi ya 65 waliopungua toka kwenye bunge la muungano? CCM acheni vijembe, uongo na upotoshaji!