Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Wasitudanganye eti serikali tatu zitaongeza gharama, mbona leo hii tuna serikali mbili na bado deni la taifa linazidi kukua na hali ya mtz inazidi kuwa mbaya!
Hapa ni serikali tatu mpaka mwisho na hayo ndio maoni ya wananchi!

Tatizo watu wanaopinga rasimu hawatoi hoja zenye mashiko kuikataa na badala yake wanaendeleza chuki kwa tume.
 
Matatizo ya kuwapa fadhila kila ati mtoto wa kiongozi hata kama ni bubusa kama huyu binti wa Kawawa.

Yaani yule Nyerere kawa nani hata asijadiliwe mpuuzi mkubwa huyu.

Maloun aende akasome kisha akasimame tena na marupurupu ya MISUKULE wanzie.
Mkuu, kwa Vita na Zainab Kawawa, hapo utakuwa umeteleza. Hawa watoto ni wazalendo na wana mapenzi ya dhati kwa nchi yao.
 
Abubakar: udhaifu wa muungano unatulazimu tubadilishe katiba.
 
Amefikisha ujumbe mzima mzima, vijana wanasema makavu live
Hakika Mkuu. Yaani kaongea kwa muktadha ule ule ambao wengi wanapenda kuusikia. Ila kuna mtu alikuwa analeta utani eti anamuomba Zainab awe anaongea huku amesimama. Anasema eti wakati anaongea alikuwa amekaa. Huu ni utani sana kwa watu wa kusini ambao wengi wao ni wafupi
 
Abubakar: Makubaliano ya Muungano tulio nao inaonyesha mamlaka 3 ya znz, muungano,Tanganyika ambayo imekuja kutiwa ktk muungano
 
Zainab Kawawa anasema;
Nataka nizungumze na watanzania leo kwanini sikubaliani na serikali inayo itwa ya shirikisho. nchi ndio inayozaa urai na kutengeneza utaifa.
Jamhuri hiyo ya tanzania haitoi huduma za afya, elimu na huduma zozote. haiwezekani.
viongozi wa upinzani igeni mfano wa viongozi wa ccm, kwanini chama kimeendelea kua imara. nyie hamna utashi wa kuvumilia na kukosoana. Muna hadhi gani ya kuvaa koti linalofanana na wasisi wa nchi hii. Wajumbe wameonesha dhamira ya kuvunja muungano wetu.

Hivi nyiynyi mnaotaka serikali tatu kwania mbaya mnaonesha dhamira ya kuuvunja muungano huu. nani asiyejua chadema haina wanachama zanzibar? watanzania ndio wanao gawa uongozi. waroho wa madaraka ninyi. acheni njia za dezo. nawashukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mi naona wanasiasa karibu wote ni waroho wa madaraka.Wanaong'ang' ania tatu naisi kuna kitu watapata na wanaong' sang' ania mbili naisi kuna kitu watakosa.
 
Abubakar: kati ya mabalozi 30 ni 3 tu ambao ni wa Znz
 
Abubakar: tumesikia mbolea bil 10 msaada umetolewa Tanzania lakini Znz hata paketi 2 hazijafika Unguja na Pemba
 
Abubakar: udhaifu wa muungano unatulazimu tubadilishe katiba.
Hakika Mkuu. Ila mambo mengi ambayo anayalalamikia ni ya kiutendaji zaidi na yanaweza kurekebishwa bila hata ya kutobadili mfumo wa muungano. Mambo hayo ni pamoja na mgawanyo wa mabalozi nk
 
Hakika Zainab Kawawa ameongea kwa hisia na jazba za kisiasa

Hulu kudada hulu! Kwahiyo kanasema Chadema wanataka serikali tatu kwasababu ya kutaka madaraka, Wao ccm wanataka serikali mbili kwakutaka nini kabinti kanaonekana kahuni ka kuzaliwa haka! Kanadandia kila kanayemwona hakana hata haya nyambafu.

BACK TANGANYIKA
 
mimi naona huyu zainabu kawawa hajatumia lugha nzuri. ni kama vile wapo kichama kupeana maneno
 
Abubakar anasema;
katiba ni nini? Katiba ni muelekeo wa baadae, katiba ni dira.
katika hii katiba yetu kuna mambo mengi ni dhaifu kwa muungano. katiba inaonyesha ina mamraka tatu, ya zanzibar, tanganyika iliyo tiwa kwenye mamraka ya muungano. katiba haina misingi ya muungano,ibara ya 98[1b].

Bunge inaweza kutunga sheria na kusema tu itumike zanzibar, haiwezekani zanzibar ina wawakirishi wake.
mambo ya nje ina mabalozi kama thelathini kati yao wazanzibar ni watatu tu, je wazanzibar hawafai.? kuna mbolewa imetolewa na japan billioni 10 lakin zanzibart hijapelekwa hata mfuko mmoja huo ni muungano?.

Lililopo hapa Tanganyika imevaa koti la tanzania. ndo maana ikiletwa mbolea inaenda songea na ruvuma. sasa hili koti livuliwe. sisi zanzibar tunataka serikali ya shirikisho, lakini lakini tume imesema serikali moja mbili shirikisho hayafai inayo faa ni serikali tatu basi tumekubaliana nao. Serikali tatu ndo zitatoamuelekeo wa swala hili. asanteni
 
Kwa hakika sioni msingi wowote kwa mtu anayejitambua kuwa Upande CCM zaidi ya kusaka tonge,, au la ni mjinga na kwa sababu ameshindwa kuukataa ujinga hawezi kuikataa CCM,

Kweli mkuu ujinga wetu mtaji wao,na sehemu za wajinga ndiko ccm inatamba
 
Abubakar: Tanganyika imevaa koti la Tanzania ndo maana mbolea ya Tanzania haifiki Znz inaishia Tanganyika
 
Mkuu, kwa Vita na Zainab Kawawa, hapo utakuwa umeteleza. Hawa watoto ni wazalendo na wana mapenzi ya dhati kwa nchi yao.

Ntakufungulia thread mkuu juu ya hayo uloyanena.

Hebu tuendelee na hili kwanza tusiipotoke ndia.
 
Aboubakar kama anajijua hivi...!

Heko mdogoangu kwa hilo.
 
Waziri wa sheria zanzibar kanichekesha sana naye kavua uwaziri kapandwa mzuka katoa mipasho kweli zanzibar ipo kazi juzi jusa aliwekwa wazi kwa kila kitu.
 
Back
Top Bottom