Ndungu zangu wangu watanzania kwanza kabisa niseme pole yetu kwa kuwa matarajio yetu ya kupata katiba mpya yanazidi kuyoyoma,nasema yanazidi kuyoyoma kwa kuwa sote tunaona staili mpya ya wawakilishi wetu kuwa wameanzisha mashindano ya mashairi na sio kujena hoja tena,kama nilivyo sema hapo juu pole yetu narudia tena pole yetu kwa jinsi tunavyo endelea kukwerwa na watu hawa wanao endelea kutumi kodi zetu kwa akwenda kufanya mazoezi ya mashari na sio kufanya kazi tuliyo watuma ya kututengenezea katiba mpya.
Ukilitizama kwa makini Bunge hili unajiuliza ni kwa nini linaendelea kuwepo pale ukizingatia kuwa kuwa kila kundi linaendelea kuwa msimamo wake na hakuna namna yeyote ya kufikia muafaka,Binafsi sioni nhaya ya wawakilishi hawa kupoteza muda na kula kodi za walala hoi kwa kutusikilizisha mipasho,ni vyema wangeenda kwenye kura na kupata uamuzi juu ya jambo linalo bishaniwa na sio kuendelea kutukana na kuwa fanya watanzania wakose imani nao na kuona kama wanayo yafanya yana lengo la kuendelea kukaa dodoma ili wajichumie fedha za wavuja jasho wa Tanzania ambao kwa sasa hawana pa kusemea zaidi ila wanavumilia maumivu ya kukosa huduma za muhimu ili hali watu wanachezea mapato yao kwa kutukana na kuwasababishi watanzania adha kubwa,kwa siku za karibuni Bunge limekuwa halifai kutizamwa na watu chini ya miaka kumi na nane kwa kuwa yanayo ongelewa hayawafai kwa mila zete.
Mwisho kabisa ningependa kusema jambo moja kuwa umoja siku zote ni nguvu ila umoja unakuwa na nguvu haswa pale ambapo wenye umoja wanaendelea kukubaliana na umoja huo,lakini itakapo fikia wenye umoja mmoja wao kutokubaliana na umoja wenu maana yake umoja huo utakuwa wa hatari sana hauna tofauti na kuwa na mke ambae yeye ameshafikia uamuzi wa kusema sasa basi sitaki kuendele na ndoa hii na mume kusema tutaendelea utake usitake.
Sote tunaona na tunakubaliana kuwa kuna tatizo katika muungano wetu na ni kweli kwamba matatizo tuliyo nayo yanaweza kutatuliwa tu kama tutakubaliana na mfumo wa aina yeyote kati ya mifumo iliyo pendekezwa ila tatizo kubwa hapa ni makubaliano hayo kutokupatikana kwa kuwa makundi yete hayako tayari kulegeza misimamo yao.
Ushari kwa wawakilishi wetu ni vyema wakaelekeza akili zao kwenye njia sahihi ya kuwa na muafaka kwa njia hii wanayo itumia ya mipasho na ushindani narejea kauli ya wengi iliyo wahi kutolewa na watu tofauti tofauti kuwa hapatakuwa na mshindi kwenye hili kama hali hii itaendelea kuwa hivi.
Kuna mengi sana ya kushauri ila kwa leo nishie hapa na wengine wataweza kuongezea.