Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Wanasheria mtusaidie.
Je, quorum itatimia kwa ma CCM kuendelea na Kijiwe chao ?
Kwao CCM kwa kuwa wamezoea vya kunyonga kama alivyobainisha Mwanasheria nguli Tundu Lissu, kwa hiyo hata ikikosekana quaram, kwa kuwa wamebaki peke yao watachakachua tu idadi ya wajumbe, ili waendelee siyo kutunga katiba ya wananchi, bali watatunga katiba yao ya CCM ambayo wataipachika jina kuwa ni katiba ya wananchi!
 
Hamna lolote!
Ukiwaunga mkono Ukawa lazima ujitoe akili kwanza!
Watanzania tutawapuuza!

Nafikiria kwa karibu kuwa ww hauna akili,Watz wote wako nyuma ya UKAWA,hautaki unaacha.Ni lazima kitaeleweka tu,Tanganyika ni lazima
 
Posho vipi wanarudisha au wanapiga kimya! Wengine tulisema toka mwanzo hakuna jipya hawa jamaa wataongeza katika rasimu, wanazo ajenda zao na waliofata mkumbo ndio watajua na msiwabembeleze kesho wateuliwe watu wengine wakapige ndondo.
Kuhusu posho, ni kama kile kiendacho kwa mganga kurudi ni mwiko!
 
Kama CCM ingekuwa mtu tena rais ningediliki kusema kuwa ni DITEKTA.
 
Posho vipi wanarudisha au wanapiga kimya! Wengine tulisema toka mwanzo hakuna jipya hawa jamaa wataongeza katika rasimu, wanazo ajenda zao na waliofata mkumbo ndio watajua na msiwabembeleze kesho wateuliwe watu wengine wakapige ndondo.

Kama ni kweli ninawapa pongezi nyingi UKAWA. Kwa kuendelea kushiriki katika kijiwe cha CCM ni kuhalalisha ama kuwa sehemu ya uwendawazimu unaofanywa na watawala wa CCM ili waendelee kutawala na kurithishana ufalme. Songambele unaweza kutupa ushahidi wo wote kuntu ambapo CCM waliwahi kuonesha nia ya dhati kubadilisha katiba iwe katiba bora? Kinachofanyika na kilichofanyika ni usanii wa Master Msanii kutaka kulazimisha LEGACY kwa kudandia hoja ambayo yeye binafsi na waCCm wenzake hawajawahi kuiona kama hoja muhimu au ya maana (refer ILANI ya uchaguzi ya CCM ya 2010, malumbanao ya mawaziri wa katiba na sheria, nk). Ninashangaa ninapoona watu wanashangaa eti JK anapinga Tume aliyoiunda na maoni ya wananchi ambayo aliridhia yakusanywe. Anatumia hoja dhaifu ya watu wachache waliotoa maoni. Je ni watu wangapi waliompigia kura ya kuwa rais ikilinganishwa na idadi ya watu wenye haki ya kupiga kura? In short, usanii lazima uzae matokeo kama haya!!
 
ni wapuuzi na wezi wa posho zetu,kama nyerere angewakimbia wakoloni tungepata uhuru?
so kwa nini wao wakimbie na wakijua ccm hawajui kujenga hoja?
Ni hakika UKAWA wamejiaibisha na kupoteza imani kwa wananchi....na wasijidanganye wananchi watawaelewa ------- mwanasiasa si ndugu yako hata siku moja!
R.I.P UKAWA
 
Sisiem hawashauriki kwa hoja yoyote inayotoka ukawa zaidi ya kutoa hoja zisizo na nashiko walizokaririshwa wazisimamie
Kuna haja gani ya kukaa na kujadiliana na watu waliokaririshwa cha kusema!?
 
mimi nadhani hawa ukawa ni wakuheshimu sana maana si wao waliopeleka rasimu bungeni bali wao wanataka maoni ya wananchi yaheshimiwe wenzao wanataka kuheshimu maoni ya jk na nape nawaomba watanganyika wote tuwaunge mkono ukawa hadi ccm waone aibu kurudi bungeni mwezi wa nane
 
Lema alikuwa sahihi,pia kama Mh. Sitta atakuwa na kumbukumbu nzuri ataufanyia kazi ushauri wa Lema kuwa bunge hili linaweza kumharibia kisiasa asipokuwa makini.Tunasubiri kupna busara za Sitta baada ya ukawa kumuonyesha kuwa hawako tayari kuburuzwa.
 
pumba.

Leo kimetokea kituko baada ya wale wanafiki wenye lengo baya na Tanzania kutoka nje baada ya kuonyeshwa mkataba wa muungano.

Wanafiki hao walipigwa na butwaa baada ya kuona mkataba huo live bila chenga. Ndipo walipoona wamefilisika kwa hoja na kukimbia.
 
Kwao CCM kwa kuwa wamezoea vya kunyonga kama alivyobainisha Mwanasheria nguli Tundu Lissu, kwa hiyo hata ikikosekana quaram, kwa kuwa wamebaki peke yao watachakachua tu idadi ya wajumbe, ili waendelee siyo kutunga katiba ya wananchi, bali watatunga katiba yao ya CCM ambayo wataipachika jina kuwa ni katiba ya wananchi!

JK is behinde all this, alienda kulichafua bunge sasa ccm watatunga kweli katiba waitakayo
 
ccm ni kichaka cha vijana wavivu wanaojiita wasomi! kama huamini angalia utendaji wa vijana wanaccm wasomi kwenye ofisi za umma!

Vijana wa CCM kwenye ofisi za umma....? Kwani waajiriwa wa serikali ni wanasiasa nyie mshavurugwa na mmevurugika vizuri kwa taarifa yenu hakuna Serikali tatu hapa.
 
zanzania kuna mambo,kila mjuimbe kutoka kundi la walio wengi,kazi yao ni kuiponda tume, yaimewatokea puani walivyo achiwa watengeze katiba ya ccm
 
Proffesor Lipumba na wajumbe wote wa UKAWA nawapongeza sana kwa kitendo cha kizalendo cha kususia bunge leo. Sisi tuko pamoja nanyi. Wito wangu mratibu maandamano na migomo nchi nzima kwa muda usio julikana. Hii ndiyo njia pelee iliyobaki ya kumkomboa mtanzania. Sanduku la kura haliwezi, wenyewe mmejionea kalenga na chalinze.

Watz wako tayari kwa mapinduzi ya nguvu kuiondoa ccm wanahitaji organization tu. Please msipoteze muda. Huu ndio wakati wa mapinduzi, mchuzi wa punda unatakiwa unywewe ukingali wa moto.

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA
 
Tanzania kuna mambo,kila mjuimbe kutoka kundi la walio wengi,kazi yao ni kuiponda tume, yaimewatokea puani walivyo achiwa watengeze katiba ya ccm,wanaojitahidi kuibeba ccm wanazidi kupoteza mvuto mbele ya jamii, baada ndg member kuzomewa Leo bungeni,
 
CCM na washirika wao wanaendelea kutoa vijembe na hoja dhaifu. Kwanza wanalalama wapinzani kuungana. Wapinzani kuungana si ajabu hata Zanzibar CCM na CUF wameungana licha ya kuwa mahasimu kwa miaka mingi sana. Vyama vina sera tofauti. Tofauti hizi zinakuwepo pale vinapotafuta kuungwa mkono na wananchi katika sera zao. Lakini kwa suala lenye masrahi ya kitaifa lazima watanzania waungane bila kujali itikadi za vyama vyao.

CCM ndo wanawagawa watanzania katika misingi ya vyama vyao ili wapitishe mambo yasiyo na masrahi kwa taifa ili waendelee kupora fedha na rasrimali za wananchi. Ndo maana wanalalama sana na kuona nongwa kuona CUF, NCCR-Mageuzi na CHADEMA wameungana lakini cha kusikitisha CCM hao hao hawakulalama wakati CUF na CCM walipoungana ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

Kuhusu gharama za muungano, wizara za muungano zipo hakuna itakayoongezwa. Na kwa muundo wa serikali mbili kuna wabunge zaidi ya 70 wanaotoka zanzibar. Na kwa maana hiyo ili kuweka usawa kati ya bara na visiwaani, inamaana kuna wabunge zaidi ya 70 toka Tanzania bara kufanya idadi ya wabunge zaidi ya 140 wanaoshughulika na mambo ya muungano. Gharama hizi CCM hawazioni kama ni mzigo kwa watanzania. Lakini muundo unaopendekezwa katika rasimu, bunge la muungano litakuwa na wabunge 75 tu wa muungano. Zaidi ya wabunge 65 watapungua katika bunge la muungano. Sasa swali la kujiuliza ni hili: Je, nafasi mbili (2) au Tatu (3) za rais, makamu au na waziri mkuu wa Tanganyika ndo zitachukua gharama za wabunge zaidi ya 65 waliopungua toka kwenye bunge la muungano? CCM acheni vijembe, uongo na upotoshaji!
 
Back
Top Bottom