Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Jumatano, Tarehe 26 Novemba, 2014

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Jumatano, Tarehe 26 Novemba, 2014

Status
Not open for further replies.
Sisi ndio tumerogwa na mchawi wetu ndio huyo CCM. We unafikiri hili zogo tunalopiga humu kama tungeamua kulifanya kwa vitendo kwakwenda kukesha nje ya bungu (au mahala popote pale penye uwazi) usiku wajana wote, unadhani ingekuaje? Wenzetu MSUMBIJI ilipanda bei ya mkate tu, lakini watu walionyesha hisia zao kwa vitendo lakini sisi jambo kubwa kama hili (au tunasubili kubwa lipi zaidi? ) tumejazana JF (na mitandao mingine ya kijamii) tunatiana ujinga tu. Hili swala litapita kama "upepo " yalivyo pita mengine yaliyo tangulia.
Hebu anza basi, tueleze wapi huko ili na sisi tukufuate. Acha kulalamika tu pasipo vitendo!
 
Mbona hatua mlishachukua, au wewe huzioni? Si ni hizi za ku-post na kuishia kulalamika nyuma ya keyboard tu, au kwani Watz wanajua hatua zingine za kuchukua zaidi ya hii? Haitakaa ikatokea, nyie endeleeni ku-post tu hapa huenda wale wazee watawasikia na kurudisha pesa zenu kwa wingi wa posts zenu humu!

nchi ya mazuzu, ni kwa neema za Mungu pekee mambo yatakuwa mazuri
 
Huo "umoja" maana yake ni nini? Unasubiri watu wawe wangapi ndio uone kwamba huo umoja umekuwa na nguvu? Katika nchi zote zilizowahi kufanya mapinduzi duniani, mara nyingi mapinduzi hayo huanzishwa na mtu mmoja then kikundi kidogo na hatimaye wanakuwa wananchi wengi. Sasa wewe badala ya kutumia muda huu ku-organize watu wachache kwa ajili ya kulianzisha cha ajabu uko busy hapa JF una-post lawama kibao. Utasubiri miaka elfu 6 kwa hilo unalolitaka kutokea ikiwa hii ndio mentality ya watu wanaojiita GT kama wewe! Yaani ni heri kukaa kimya tu na kuacha mambo yajiendee kwa kudra za Mwenyezi Mungu!

Na wewe unafanya nn hapa!
Niache mie nilieamua kupost hapa
 
Jamani watanzania,tusipoangalia hili jambo litazimwa hivi hivi na hawa wabadhilifu watapenya!TUAMKE WATANZANIA,SUALA LA ESCROW LINATUGUSA WOTE
 
Kama hukuelekeza akili zote kwenye eskroo, maswali yaliisha mapema

Ndiyo maswali yaliisha na lilitakiwa kufuata ni report, lakini wewe unataka kutuaminisha kwamba ule ndo muda bunge huwa linaisha tusishangae ndo napingana nalo.
 
Mhh!! Ndugu bunge linaisha siku zote saa 5? Maana ndo muda lilipohairishwa,hapana usitupotoshe...

Kama hukuelekeza akili zote kwenye escrow, utakuwa uligungundua kuwa maswali yaliisha mapema kabla ya wakati. Hiyo so sababu ya kujadili kisichokuwapo kwenye ratiba ya mda huo. Mfano shuleni: Ukimaliza mtihani mapema uruhusiwa kwenda kupumzika, hutapewa mwingine kabla ya muda wake kiratiba. Maana Yangu tuelekeze ufahamu wetu kwa ratiba rasmi.
 
christine ibrahim kuna mtu humu alinichekesha sana Jana humu nilishindwa kuelewa amefikiri nini? Jamaa alisema! " Hivi wanaume wote tuliopo Tanzania kama sakata la Escrow likifanyiwa mizengwe na tukashindwa kufanya chochote kwanini tusiolewe tuu?"

Nilicheka sana daaa huyu jamaa ana machungu sana na hakika watanzani tuko nyuma sana angalia nchi za wenzetu mtoto kapigwa risasi watu wame react hadi Us defense secretary anataka kujiuzulu!

Hakika mahakama zinatumika vibaya sana tena sana! Ngoja tuone jioni!

I am seriously surprised, it's you writing this and you seem to be happy!! I hope................. your mind will keep put so that tomorrow you do not praise or defend the same people!! By the way, the US defense secretary is not quitting because of the Ferguson ........... scandal!!
 
Na wewe unafanya nn hapa!
Niache mie nilieamua kupost hapa
Mimi niko hapa kusahihisha watu wanaotaka kupotosha hali halisi ya nchi yetu. That's why hata wewe ujumbe umeupata,nisingekuwa hapa usingejua chochote At least mimi nimeweza kuleta impact kwako, sasa wewe unayeishia kupost tu hapa umeleta badiliko gani? Ndio maana nikakushauri ukae tu kimya usije ukapoteza nguvu zako bure!
 
Jamani watanzania,tusipoangalia hili jambo litazimwa hivi hivi na hawa wabadhilifu watapenya!TUAMKE WATANZANIA,SUALA LA ESCROW LINATUGUSA WOTE
Usiishie kusema tuamke, tuamke twende wapi? Na wewe uliyeamka uko wapi huko ili na sisi tukufuate? Au ndio wewe unayehangaika kuamsha wenzako mwishowe unalala wewe?!
 
Kama hukuelekeza akili zote kwenye escrow, utakuwa uligungundua kuwa maswali yaliisha mapema kabla ya wakati. Hiyo so sababu ya kujadili kisichokuwapo kwenye ratiba ya mda huo. Mfano shuleni: Ukimaliza mtihani mapema uruhusiwa kwenda kupumzika, hutapewa mwingine kabla ya muda wake kiratiba. Maana Yangu tuelekeze ufahamu wetu kwa ratiba rasmi.

Haya nimekuelewa kwahiyo ilipangwa isomwe jioni siyo? Ok ngoja tusubiri masaa hayagandi saa 11 siyo mbali.
 
kama sheria na kanuni za bunge zinasema bunge haliwezikuzuiwa kufanya kazi zake kamati ya uongozi ilikutana kujadili nini wakati kwa mujibu wa sheria na kanuni za bunge hakukuwa na cha kujadili maana hilo zuio kama lipo automaticaly ni null and void? Wanapokeaje zuio ambalo halitambuliwi kisheria na kikanuni?

Unless waseme wanajadili directives na vimemo kutoka juu....

ndugu achana na wanasiasa, huwa wanaongea kama walokole wanavyokuwa wananena kwa lugha.hakuna ukweli kwamba bunge haliwezi kuingiliwa.bunge haliko juu sheria.mahakama ina wajibu wa kutafsiri sheria na kutoa haki.kama bunge likienda kinyume na sheria ikiwa ni pamoja na kupokonya haki za wengne,mahakama ndo inaingia hapo.nadhani nao wangepinga hoja ya mahakama kuu kwa kukata rufaa na sio kukaidi kwa kisingizio kwamba hawaingiliwi ama wajenge hoja kwamba mahakama inatumika na katika haina mamlaka nalo wangeeleweka!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom