Yanayojiri Bungeni Dodoma leo March 08, 2014

Chabruma

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2013
Posts
5,660
Reaction score
1,780
Wadau,

Baada ya kuwawakilisha vema siku ya jana tarehe 7.3.2014, leo tutaendelea kuwajuza yatakayojiri Dodoma kwenye semina ya Bunge Maalum. Kazi kubwa ya leo ni upitishwaji wa vile vifungu vya Rasimu ya Kanuni kuanzia cha 32 hadi 43 ambavyo vilitakiwa vipitishwe jana lakini ikashindikana. Mtakumbuka kuwa kabla Mwenyekiti hajaahirisha Semina ya jana, alitangaza Kamati maalum ya maridhiano ambayo iliketi jana kuanzia saa 9 alasiri kutafuta namna nzuri ya kupitisha vifungu hivyo.

Aidha, makundi maalum yanayounda Bunge Maalum yalikutana kuanzia saa 12 jioni ili kupata taarifa juu ya yale yaliyoafikiwa na Kamati ya Maridhiano. Kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa siku ya leo hoja kutoka kwenye floor hazitakuwa nyingi na kali kwa vile vipengele hivyo vitapitishwa kimaridhiano.

As usual, nitakuwa sambamba na Simiyu Yetu kuwahabarisha wana JF. JF itakuwa ya kwanza daima na wengine watafuatia. Pamoja sana.

Stay Connected.

==========================

UPDATES 1

Semina imeahirishwa hadi saa 9 Alasiri. Sababu ya kuahirishwa ni kuwa maridhiano yalikuwa hayajapatikana kuhusuvifungu vya 32 hadi 43. Kipengele kinachovuta hisia za wabunge wengi ni kifungu cha 37 na 38 juu ya ufanywaji wa maamuzi. Hata hivyo kuna dalili muafaka ukapatikana katika kipengele hicho hasa baada ya baadhi ya wabunge waliokuwa wanapinga Kura ya Siri kulegeza msimamo Wao.

Kuanzia saa tano ile Kamati ya Maridhiano ambayo iliundwa kushughulikia muafaka wa vifungu hivyo itaendelea na kikao chake.


=========================

UPDATES 2 (saa 16.00)

Kamati ya Maridhiano inaendelea na kikao chake kutafuta suluhu ya vifungu vya 32 hadi 43. Taarifa zilizopo ni kuwa kila kundi linaendelea kusimama na misimamo yake hali inayoipa Kamati ya Maridhiano kazi ngumu. Kuna taarifa kuwa baadhi ya makundi yametishia kutoingia ukumbini iwapo maamuzi yao hayatapita. Pamoja na hayo busara zinaendelea kutumika ili kulimaliza jambo hili kwa njia ya maridhiano


 
Pamoja sana Kiongozi. Tumeridhika na uwasilishaji wenu ile jana na hakika leo mtaboresha zaidi ili kukonga nyoyo za wana JF
 
Baada ya vikao vya jana kwenda vema hasa vile vya kamati na vile vya usuruhishi leo kanuni zinaweza kupita hatimaye zoezi la kupata mwenyekiti lifuate.
 
Chabruma

kumbe uko na gamba lenzio.hata sina muda wa kufuatilia uchafu wenu maana nyie ni kizazi cha wachakachuaji.
 
Last edited by a moderator:
kumbe uko na gamba lenzio.hata sina muda wa kufuatilia uchafu wenu maana nyie ni kizazi cha wachakachuaji.

Mkuu, naamini kuwa linapokuja suala la kitaifa kama hili la katiba, watanzania ni wamoja. Ndo maana hata kwenye ile kamati ya kanuni kuna akina Simbachawene, Lissu, Abubakar Hamis Bakari na wengine wenye itikadi tofauti kisiasa. Hilo lisikuumize sana. Jana hawa jamaa wamefanya kazi nzuri na naamini leo watakuwa hivyo pia
 
Baada ya vikao vya jana kwenda vema hasa vile vya kamati na vile vya usuruhishi leo kanuni zinaweza kupita hatimaye zoezi la kupata mwenyekiti lifuate.
habar kuletwa na mtu huyu ni habar za kishabiki sana.... hajitambui ---- huyu
 
Sina imani na hii timu kwamba itamtaja lissu kwa usahihi bila kuongeza chumvi
 
Chabruma

Chabruma taarifa yako fupi imetulia sana,naomba uongeze juhudi unaweza kuwa mwandishi bora kabisa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Chabruma
hiyo Kmati ya Maridhiano ni ilikuwa na wajumbe gani Mkuu...Weka na Picha zao kama vip
 
Last edited by a moderator:
Naomba kujua km kuna redio yeyote itarusha. nipo dar ila na kazi yangu ya umachinga siwezi kwenda kukaa bar niangalie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…