Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,780
Wadau,
Baada ya kuwawakilisha vema siku ya jana tarehe 7.3.2014, leo tutaendelea kuwajuza yatakayojiri Dodoma kwenye semina ya Bunge Maalum. Kazi kubwa ya leo ni upitishwaji wa vile vifungu vya Rasimu ya Kanuni kuanzia cha 32 hadi 43 ambavyo vilitakiwa vipitishwe jana lakini ikashindikana. Mtakumbuka kuwa kabla Mwenyekiti hajaahirisha Semina ya jana, alitangaza Kamati maalum ya maridhiano ambayo iliketi jana kuanzia saa 9 alasiri kutafuta namna nzuri ya kupitisha vifungu hivyo.
Aidha, makundi maalum yanayounda Bunge Maalum yalikutana kuanzia saa 12 jioni ili kupata taarifa juu ya yale yaliyoafikiwa na Kamati ya Maridhiano. Kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa siku ya leo hoja kutoka kwenye floor hazitakuwa nyingi na kali kwa vile vipengele hivyo vitapitishwa kimaridhiano.
As usual, nitakuwa sambamba na Simiyu Yetu kuwahabarisha wana JF. JF itakuwa ya kwanza daima na wengine watafuatia. Pamoja sana.
Stay Connected.
==========================
UPDATES 1
Semina imeahirishwa hadi saa 9 Alasiri. Sababu ya kuahirishwa ni kuwa maridhiano yalikuwa hayajapatikana kuhusuvifungu vya 32 hadi 43. Kipengele kinachovuta hisia za wabunge wengi ni kifungu cha 37 na 38 juu ya ufanywaji wa maamuzi. Hata hivyo kuna dalili muafaka ukapatikana katika kipengele hicho hasa baada ya baadhi ya wabunge waliokuwa wanapinga Kura ya Siri kulegeza msimamo Wao.
Kuanzia saa tano ile Kamati ya Maridhiano ambayo iliundwa kushughulikia muafaka wa vifungu hivyo itaendelea na kikao chake.
=========================
UPDATES 2 (saa 16.00)
Kamati ya Maridhiano inaendelea na kikao chake kutafuta suluhu ya vifungu vya 32 hadi 43. Taarifa zilizopo ni kuwa kila kundi linaendelea kusimama na misimamo yake hali inayoipa Kamati ya Maridhiano kazi ngumu. Kuna taarifa kuwa baadhi ya makundi yametishia kutoingia ukumbini iwapo maamuzi yao hayatapita. Pamoja na hayo busara zinaendelea kutumika ili kulimaliza jambo hili kwa njia ya maridhiano

Bungeni Dodoma: CCM yasisitiza kura ya wazi na kukataa maamuzi ya theluthi mbili
Nipo ndani ya bunge now na ccm wamemaliza mkutano wao soon kwa kukataa katakata kura ya siri katika maamuzi yote na kutaka kura ya wazi. Aidha ccm pia wamekusudia leo hii kurudisha nyuma kwa kutengua kanuni ya upitishaji maamuzi ili iwe nusu ya wajunbe wa zanzibar na nusu ya watanganyika na kuifuta theluthi mbili iliyokubalika na kupitishwa.
Kamati aliyounda kificho ya maridhiano imeshindwa kukubaliana na hadi ninapotuma andiko hili bado kikao kinaendelea cha kamati ya maridhiano kujua cha kuganya kwani kikao huenda kikavunjika mapema leo.
Endeleeni kusubiri zaidi