Wadau,
Baada ya kuwawakilisha vema siku ya jana tarehe 7.3.2014, leo tutaendelea kuwajuza yatakayojiri Dodoma kwenye semina ya Bunge Maalum. Kazi kubwa ya leo ni upitishwaji wa vile vifungu vya Rasimu ya Kanuni kuanzia cha 32 hadi 43 ambavyo vilitakiwa vipitishwe jana lakini ikashindikana. Mtakumbuka kuwa kabla Mwenyekiti hajaahirisha Semina ya jana, alitangaza Kamati maalum ya maridhiano ambayo iliketi jana kuanzia saa 9 alasiri kutafuta namna nzuri ya kupitisha vifungu hivyo.
Aidha, makundi maalum yanayounda Bunge Maalum yalikutana kuanzia saa 12 jioni ili kupata taarifa juu ya yale yaliyoafikiwa na Kamati ya Maridhiano. Kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa siku ya leo hoja kutoka kwenye floor hazitakuwa nyingi na kali kwa vile vipengele hivyo vitapitishwa kimaridhiano.
As usual, nitakuwa sambamba na Simiyu Yetu kuwahabarisha wana JF. JF itakuwa ya kwanza daima na wengine watafuatia. Pamoja sana.
Stay Connected.
===========================================================================
UPDATES 1
Semina imeahirishwa hadi saa 9 Alasiri. Sababu ya kuahirishwa ni kuwa maridhiano yalikuwa hayajapatikana kuhusuvifungu vya 32 hadi 43. Kipengele kinachovuta hisia za wabunge wengi ni kifungu cha 37 na 38 juu ya ufanywaji wa maamuzi. Hata hivyo kuna dalili muafaka ukapatikana katika kipengele hicho hasa baada ya baadhi ya wabunge waliokuwa wanapinga Kura ya Siri kulegeza msimamo Wao.
Kuanzia saa tano ile Kamati ya Maridhiano ambayo iliundwa kushughulikia muafaka wa vifungu hivyo itaendelea na kikao chake.