Yanayojiri Bungeni Dodoma leo March 08, 2014

Yanayojiri Bungeni Dodoma leo March 08, 2014

Wadau,

Baada ya kuwawakilisha vema siku ya jana tarehe 7.3.2014, leo tutaendelea kuwajuza yatakayojiri Dodoma kwenye semina ya Bunge Maalum. Kazi kubwa ya leo ni upitishwaji wa vile vifungu vya Rasimu ya Kanuni kuanzia cha 32 hadi 43 ambavyo vilitakiwa vipitishwe jana lakini ikashindikana. Mtakumbuka kuwa kabla Mwenyekiti hajaahirisha Semina ya jana, alitangaza Kamati maalum ya maridhiano ambayo iliketi jana kuanzia saa 9 alasiri kutafuta namna nzuri ya kupitisha vifungu hivyo.

Aidha, makundi maalum yanayounda Bunge Maalum yalikutana kuanzia saa 12 jioni ili kupata taarifa juu ya yale yaliyoafikiwa na Kamati ya Maridhiano. Kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa siku ya leo hoja kutoka kwenye floor hazitakuwa nyingi na kali kwa vile vipengele hivyo vitapitishwa kimaridhiano.

As usual, nitakuwa sambamba na Simiyu Yetu kuwahabarisha wana JF. JF itakuwa ya kwanza daima na wengine watafuatia. Pamoja sana.

Stay Connected.

===========================================================================

UPDATES 1

Semina imeahirishwa hadi saa 9 Alasiri. Sababu ya kuahirishwa ni kuwa maridhiano yalikuwa hayajapatikana kuhusuvifungu vya 32 hadi 43. Kipengele kinachovuta hisia za wabunge wengi ni kifungu cha 37 na 38 juu ya ufanywaji wa maamuzi. Hata hivyo kuna dalili muafaka ukapatikana katika kipengele hicho hasa baada ya baadhi ya wabunge waliokuwa wanapinga Kura ya Siri kulegeza msimamo Wao.

Kuanzia saa tano ile Kamati ya Maridhiano ambayo iliundwa kushughulikia muafaka wa vifungu hivyo itaendelea na kikao chake.

Sijui kama tutapata katiba mpya!
 
Haiwezekani mpaka leo siku zinapita wanahangaika na kanuni. Ni kuchezea hela za watanzania. Kama muafaka haupo wapige kura jambo liamuliwe. Hizo siku 70 wakianza rasimu si zitaisha na hata 90 hazitatosha!
 
Kwa nini isiwe nyie mnaoipenda ya wazi mlegeze kamba?Kwa nini hamtaki kura ya siri?Kuna ajenda gani hapo?
Mkuu, kama umemwelea vizuri CHABRUMA, ni kwamba wanaopinga kura ya siri na kupenda ya wazi wameamza kwenda kinyume na misimamo yao. Hii ni kusema kuwa wanaweza kuunga mkono kura ya siri kwa lengo tu la maridhiano na kuruhusu mchakato uendelee. Vinginevyo, mchakato wa Bunge Maalum utakuwa umekwama. Nawapongeza sana wale waliokubali kushindwa kwa lengo la kuleta maridhiano
 
Soma hiyo post vizuri, waliolegeza kamba ni wanaopenda kura ya wazi kwa sababu kimsingi hawana hoja za msingi za kupinga kura ya siri...

Kwa nini isiwe nyie mnaoipenda ya wazi mlegeze kamba?Kwa nini hamtaki kura ya siri?Kuna ajenda gani hapo?
 
Mkuu, kama umemwelea vizuri CHABRUMA, ni kwamba wanaopinga kura ya siri na kupenda ya wazi wameamza kwenda kinyume na misimamo yao. Hii ni kusema kuwa wanaweza kuunga mkono kura ya siri kwa lengo tu la maridhiano na kuruhusu mchakato uendelee. Vinginevyo, mchakato wa Bunge Maalum utakuwa umekwama. Nawapongeza sana wale waliokubali kushindwa kwa lengo la kuleta maridhiano

NAshukuru kwa kunieleswesha ,nitairudia na kuisoma upya.Asante tena
 
Ninachojiuliza,je huyo mwenyekiti wa muda alipatikana kwa kura ya wazi au ya siri?Je uchaguzi wa raisi ,wabunge na madiwani inapigwa kura ya wazi au ya siri?Je kwa hiyo kwa upigaji huo wa kura ya siri miaka yote serikali ilivunja demokrasia?Wale wote mnaoshabikia upuuzi wa kura ya wazi eti ndiyo demokrasia ni wapuuzi na chama chochote kinachoshabikia kura ya wazi ni cha kipuuzi!
 
Soma hiyo post vizuri, waliolegeza kamba ni wanaopenda kura ya wazi kwa sababu kimsingi hawana hoja za msingi za kupinga kura ya wazi...

Asante kwa kunielewesha nitarudi na kuisoma upya.
 
Mimi sioni hata wanastahili kupongezwa !

Walikuwa hawana sababu za msingi za kupinga hizi kura tangu mwanzo, na kama mchakato ungekwama, wao ndio wangebeba msalaba ! Kama wao wanapenda wananchi wajue maamuzi yao, wanashindwa nini kuweka kura zao wazi mara baada ya kupiga za siri ? Kwa nini wanataka na wengine wasiotaka kuweka zao wazi, walazimike kufanya hivyo ?

Kwa maneno mengine wale wanaopenda kuweka kura zao wazi, bado wana opportunity ya kufanya hivyo ikiwa watapenda kufanya hivyo....kitu kibaya walichokuwa wanataka kufanya ni kulamisha na wenzao waweke zao hadharani hata kama hawapendi kufanya hivyo ! Kuna watu hapo wasingependa hata waume/wake zao (pamoja na watu wengine) wajue jinsi walivyopiga kura. Sasa kwa nini ulazimishe watu wa aina hiyo waweke kura zao hadharani ? Kama wao ni majasiri kama wanavyodai na wanawapenda sana wananchi wajue walivyopiga kura, kama wanavyodai, sasa wakishapiga kura za siri, wazitangaze za kwao !

Mkuu, kama umemwelea vizuri CHABRUMA, ni kwamba wanaopinga kura ya siri na kupenda ya wazi wameamza kwenda kinyume na misimamo yao. Hii ni kusema kuwa wanaweza kuunga mkono kura ya siri kwa lengo tu la maridhiano na kuruhusu mchakato uendelee. Vinginevyo, mchakato wa Bunge Maalum utakuwa umekwama. Nawapongeza sana wale waliokubali kushindwa kwa lengo la kuleta maridhiano
 
Kwa nini isiwe nyie mnaoipenda ya wazi mlegeze kamba?Kwa nini hamtaki kura ya siri?Kuna ajenda gani hapo?

hujamwelewa, tafadhali rudia kusoma.
 
Haiwezekani mpaka leo siku zinapita wanahangaika na kanuni. Ni kuchezea hela za watanzania. Kama muafaka haupo wapige kura jambo liamuliwe. Hizo siku 70 wakianza rasimu si zitaisha na hata 90 hazitatosha!

Hapo kwa nyekundu,,,,,njia watakayotumia ndiyo itakayokuwa imemaliza mvutano huo wa uwazi na usiri.
 
Hapo kwa nyekundu,,,,,njia watakayotumia ndiyo itakayokuwa imemaliza mvutano huo wa uwazi na usiri.

Wapige kura ya siri kuamua kura ya kupitisha vifungu iwe ya siri au ya wazi. Tusonge mbele huo muafaka wakuhairisha hairisha bunge ni kuwakosea watanzania masikini!
 
Leo tv zote hazina live coverage wakati kificho alisema wangeendelea leo asubuh. Kulikon
 
Hivi nqjiuliza kwa nini watu wang'ang'anie kura ya wazi. Mbona sijawahi kuona uchaguzi wowote unapigiwa kura ya wazi. Wanataka kuwatisha wapiga kura hapa au? Wanashindwa kutofautisha na zile kura za bungeni za Ndiyooooo! Au hapana!!!! Halafu utasikia naona waliosema ndiyo wameshinda. Pale kuna politics hapa siyo penyewe..Labda kama sijaelewa sababu ya ssem kuleta hii ajenga ya kura ya wazi
 
Kura za wazi za CCM zinanikumbusha kura za MLOLONGO za KANU ktk utawala wa Daniel Toroitich Arap Moi mwaka 1986! watu walipanga mstari nyuma ya picha ya mgombea!
 
Ina maana na wewe uliteuliwa kuwepo kwenye hiyo bunge la katiba?
baada ya vikao vya jana kwenda vema hasa vile vya kamati na vile vya usuruhishi leo kanuni zinaweza kupita hatimaye zoezi la kupata mwenyekiti lifuate.
 
Yaani hata mm nawashangaa sana wanaong'ang'ania kura za wazi
hiyo yote wameshaona watanshindwa kiaina na hawa ss em hawataki serikali tatu
hy naona wanataka iwe janja yao kwani wao wako bungeni na ni wengi mno

hivi nqjiuliza kwa nini watu wang'ang'anie kura ya wazi. Mbona sijawahi kuona uchaguzi wowote unapigiwa kura ya wazi. Wanataka kuwatisha wapiga kura hapa au? Wanashindwa kutofautisha na zile kura za bungeni za ndiyooooo! Au hapana!!!! Halafu utasikia naona waliosema ndiyo wameshinda. Pale kuna politics hapa siyo penyewe..labda kama sijaelewa sababu ya ssem kuleta hii ajenga ya kura ya wazi
 
Back
Top Bottom