Yanayojiri Bungeni Dodoma leo March 08, 2014

Yanayojiri Bungeni Dodoma leo March 08, 2014

Si wanatuficha wananchi tusione malumbano yao na nini kinaendelea
ila wajue hata wakituficha lazima haki itendeke huko

leo tv zote hazina live coverage wakati kificho alisema wangeendelea leo asubuh. Kulikon
 
Wadau, nipo hapa viwanja vya bunge tayari kuwaletea yanayojiri kwenye semina ya Bunge Maalum. Nje ya ukumbi, hakuna movements za wabunge. Kwenye Canteen wapo wabunge wachache wanapata chakula. Kile kikao cha Kamati ya Maridhiano kimefanyika na sasa wanaendelea kuandaa taarifa ya walioafikiana na jinsi walivyoafikiana. JF itakuwa nanyi muda wote na hakuna litakalowapita.
 
Taswira ya Ukumbi wa Bunge robo saa kabla ya kikao kuanza. Nipo humu ndani na ni wabunge wasiozidi 10 ndo wameingia. Wengi wameenda kupata chakula hasa kwa vile vikao vya mrejesho wa yale yalioafikiwa vimemalizika hivi punde
image.jpgimage.jpgimage.jpg
 
Wakuu na wanajamvi wote naomba kwa anayejuwa kama bunge maalumu wafanya semina leo saa 4 asubuhi kama m/kiti wa bunge alivyotangaza jana jioni

Mimi muda huo nilikuwa safarini ndio maana sikuweza kufuatilia anayejuwa anijuze tafadhali.
 
Wabunge wa CCM wamedaiwa kupokea vitisho, kama watakwenda kinyume na msimamo wa chama.


Dodoma. Mpasuko miongoni mwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), umechukua sura mpya, baada ya kuelezwa kuwa wabunge 90 wameorodheshwa kwa lengo la kuhojiwa kwa tuhuma za kukisaliti chama.

Wajumbe hao wengi wao wakiwa ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wamekuwa wakiitwa na mmoja wa viongozi waandamizi wa Serikali ya CCM na kuelezwa wazi kuwa chama hakiridhiki na mwenendo wao.

Wengi wa wajumbe hao ni wale waliotamka hadharani kuunga mkono muundo wa Muungano wa Serikali tatu, badala ya Muungano wa Serikali mbili ulioboreshwa, ambao ndiyo msimamo wa chama hicho tawala.

Wengine ni wale wanaotajwa kuunga mkono upigaji wa kura wa siri katika kupitisha vifungu vya rasimu ya Katiba Mpya, ikiwa ni kinyume na msimamo wa CCM wa kutaka kura ya wazi.

“Ni kweli hata mimi niliitwa na (akimtaja jina) na kuniambia ametumwa aniletee ujumbe kuwa niko kwenye orodha hiyo na nikiendelea na msimamo huo nitachukuliwa hatua,” alidai mbunge mmoja.

Hata hivyo, mjumbe huyo alidai kuwa kinachofanywa na CCM ni sawa na kumpa mgonjwa wa saratani dawa ya kutuliza maumivu, lakini mwishowe ugonjwa alionao uko palepale.

“Mimi msimamo wangu ambao naamini ndiyo msimamo wa wabunge wengi ni kutaka kura ya siri na Serikali tatu. Nitasimamia msimamo huo, kwani ndiyo dhamira yangu kwa masilahi ya Watanzania,” alidai.

Mbunge mwingine anayetajwa kuwapo kwenye orodha hiyo (jina tunalo) alipoulizwa jana kama ana taarifa hizo alisema, “Ni kweli kuna orodha hiyo ya wabunge 90, lakini mimi sijaulizwa chochote.”

Mbunge huyo alisema, wabunge hao 90 wamewekwa katika orodha nyeusi (Black list) iliyoandaliwa na CCM kimeandaa kama njia mojawapo ya kuwatesa kisaikolojia ili waachane na msimamo wao.

Tayari CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kilishaweka wazi msimamo wake kuhusu suala la muundo wa Serikali na kutaka wajumbe wake watetee kwa nguvu zote muundo wa Serikali mbili.
 
Wakuu na wanajamvi wote naomba kwa anayejuwa kama bunge maalumu wafanya semina leo saa 4 asubuhi kama m/kiti wa bunge alivyotangaza jana jioni

Mimi muda huo nilikuwa safarini ndio maana sikuweza kufuatilia anayejuwa anijuze tafadhali.
mkuu walihairisha mpaka saa tisa ni kutokana na kamati kuwa bado hawajaafikiana
 
Hata mwali ukisha mchukuwa kazi anapigishwa kwa siri sasa nyie mbona mnang'ang'ania mpigwe kazi wazi wazi sio mila ya mwafrica aalah
 
wanapaswa waseme hadharani, wasijifiche kwani wakiogopa hukumu ya maccm hawataikwepa hukumu ya wananchi ambayo ndiyo ultimate.
 
Taswira ya ukumbi wa Bunge kama ilivyochukuliwa saa 15.06
image.jpg
 
mambo kama haya ndo yanawafanya wabunge kuunga mkono kura ya siri
 
Wabunge wanaendelea kuingia kama mnacyowaona kwa mbali ingawa muda uliopangwa umezidi dakika 12
image.jpg
 
Hata mwali ukisha mchukuwa kazi anapigishwa kwa siri sasa nyie mbona mnang'ang'ania mpigwe kazi wazi wazi sio mila ya mwafrica aalah
Mkuu, umenichekesha sana. Mifano mingine si ya kuiweka kwenye jamvi. Ingebaki kwenye fikra yako tu mkuu
 
Njaa Mbaya sana siku zote unakuwa na mawzo ya kushikiwa na watu, hiyo yote ni uhakika wa maisha
 
Bunge leo lilipaswa lianze saa 3 asubuhi kama alivyotangaza mwenyekiti wa muda Pandu Ameer kificho, kwa mujibu wa taarifa ni kwamba lililazimika kusogezwa hadi saa 9 kamili jioni, lakini tayari saa 9 imefika bado halijaanza! Kulikoni, mlioko huko tujuzeni.
 
inakuaje kura ziwe zawazi na mambo mengine yawe siri. Mara waandishi hawata ruhusiwa wachukue taarifa zote kwa M/kiti mara wanaitwa kwa siri na kuhojiwa haya mambo yamekaaje jamani?
 
Back
Top Bottom