Uchaguzi 2020 Yanayojiri kwenye Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA Mh Tundu Lissu Mkoani Geita

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wakuu nawasalimia kwa salamu ya ukombozi , leo tena yule mgombea anayeongoza kwenye kura za maoni Mh Tundu Lissu anaendelea na mikutano yake ya kampeni za kuomba kura kwa wananchi , ambapo leo atakuwepo Geita , huu ndio Mkoa aliouawa kinyama kamanda Alphonce Mawazo, RIP, mchana wa jua kali huku wauaji wanaofahamika hawajakamatwa hadi leo.

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za uhakika .


=======
UPDATES 1
Akiwa Muleba Mh Lissu amewahurumia wananchi wa hapo , baada ya kilichowapata kwenye tetemeko " mmepatwa na tetemeko badala ya kufarijiwa mkasimangwa "



UPDATES 2
Biharamuro , mapema



Video : Katoro
 

Attachments

  • Katoro ... Jirani na CHATO ( 352 X 640 ).mp4
    4.1 MB
Go Lissu hata wana Geita wanamajuto mengi bwana yule anajali kijijini kwao kinachofanyika kiasi ni sehemu ndogo mapato toka mgodi wa GGM ambao wamehodhi karibu 200 km mraba, na kufurusha wachimbaji wadogo kuwa nje mbali ya mji kuanzia 40+++ km, awali wachimbaji wadogo multiplier effect mapato ilikuwa kubwa, Lissu awape ahadi kurejesha baadhi ya maeneo Samina, Katoma, Mgusu,... hata hekari chache zitahuisha maisha mji umekuwa mgumu sana.
 
NI YEYE.

Geita chato na Viunga vyake shamra shamra ndelemo na vifijo kumlaki Rais wao.

Kazi zote zimeaimama Geita wajasiliamali,watumishi wa Uma,vibarua machinga Boda boda wapo njiani kumpokea Mkombozi wao.
Kwani huwezi kutulia ukqandika vizuri?
 
Geita mjini atakuwepo lini ili nikamsikilze sera zake?

Mpaka Sasa mgombea wa CCM nilishamsikiliza kwenye hotuba zake za karibu kila wiki(maana kila wiki lazima awe na tukio mubashara) na hivyo sikuenda kumsikiliza maana nilijua sera zake Ni zilezile za ma-ndege, mabarabara, ma-flyover.

Siku hiyo nitakacha kila ninachokifanya nikamsikilze TAL.
 
Tutakujulisha mkuu , ondoa shaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…