Yanayojiri kwenye Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA

Yanayojiri kwenye Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA

Emma.

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
19,932
Reaction score
5,563
Kikao cha Kamati Kuu ya chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiendelea muda huu, ikiongozwa na Mh. Freeman Mbowe muda huu.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama wakiwa ukumbini wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa kikao hicho iliyotolewa na Mwenyekiti Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Updates .
#MAAZIMIO_YA_KAMATI_KUU_YA_CHADEMA

Mhe. Freeman Mbowe

Leo nazungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza baada ya miezi saba na nusu ya kuwa kifungoni.

Waandishi mbalimbali walinitafuta kutoka vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi wakitaka mwenyekiti nitoe kauli ya mambo kadha wa kadha yanayojiri katika nchi yetu lakini nilichelea kufanya hivyo

Baadhi ya wale waandishi wa habari walionifikia niliwaambia kila jambo chini ya mbingu lina wakati wake. Nilitambua kwamba kuna kiu na shauku kubwa ya watanzania kusikia kauli ya Mbowe

Lakini kauli ya Mbowe ni kauli ya Chama. Isingekua sahihi kauli ya Mbowe ikatoka kabla Mbowe hajakaa na chama chake

Kwa hiyo nikawaambia chini ya mbingu kila jambo lina wakati wake. Kuna wakati wa kukusanya na kuna wakati wa kutawanya. Basi na mengine mkayasome kwenye Biblia kitabu cha Mhubiri mlango wa tatu

Kwanza niwashukuru sana waandishi wa habari, wanachadema na watanzania wote wa vyama vyote. Hakika nimeushuhudia upendo ambao sina uhakika nitaulipa kwa njia gani

Nimekua gerezani kwa muda mrefu lakini nimejifunza sana. Niwahakikishe watanzania na dunia yote kwamba sikupoteza zile siku. Nimezitumia kujiimarisha kifikra, kimtazamo na hata moyo wangu umebadilika sana

Nimesema na nasema tena, natangaza msamaha kwa yeyote ambaye nafikiri alinifanyia baya. Sina chuki wala sina kisasi.

Nawaomba wanaChadema wenzangu tusiwe na chuki na yeyote katika mapambano haya kwa sababu mapambano haya ni kupigania uhai wa watu, ni kupigania ustawi wa watu. Kamwe hatuwezi kutafuta ustawi wa watu wakati tunatafuta visasi. Visasi sio utamaduni wa chadema,sio utamaduni wa Mbowe.

Kwa hiyo mimi nimetoka na roho nyeupe kabisa, tukiwa tayari kwa kuendeleza kazi ya siasa

Nililetewa salamu za mheshimiwa Rais kwamba angependa kukutana na mimi mapema iwezekanavyo.
Mtakumbuka kwa muda mrefu sisi kama chama tulitaka kuzungumza na Rais tukiamini kwamba ana majibu ama ana ufunguzi wa mambo mengi yanayolisibu taifa letu

Kwa bahati mbaya hatukupata nafasi ya kukutana nae hadi ninakwenda gerezani. Kwa hiyo nikiwa gerezani siku natoka nikaambiwa kwamba mheshimiwa Rais angependa kukuona haraka. Nimetoka gerezani kwa moyo mweupe, wala sikutoka na kiburi, cha kwamba naweza nikapuuza mualiko wa Rais.

Mbowe aliyeingia gerezani ndo Mbowe aliyetoka gerezani, tena pengine akiwa imara zaidi. Kwa hiyo nimezungumza na Rais mambo kadhaa. Lakini sikuyafikisha kwa umma kwa sababu nilihitaji kwanza kuzungumza na Kamati Kuu ya Chama changu na viongozi wenzangu

Nilipokwenda gerezani, chama hiki hakikuenda gerezani. Viongozi wenzangu walikuwepo, vikao vya chama vilifanyika, mashauriano mbalimbali yalitokea. Ninaporejea kutoka gerezani ninapaswa kwanza kukabidhiwa kiti changu ndo nizungumze kama msemaji mkuu wa chama

Kwa hiyo nawashukuru viongozi wenzangu walikilinda chama chetu katika mazingira magumu sana. Kwa hiyo ilinipasa mimi kwanza nizungumze na kamati kuu ya chama changu ili nitakapotoa kauli kwa umma nitoe kauli ya chama na sio kauli ya Mbowe

Waheshimiwa viongozi, nilipokwenda kukutana na mheshimiwa Rais Ikulu, tulichokizungumza ni kitu kimoja tu cha msingi. Kwamba tulikubaliana kutafuta njia za haki, za mazungumzo, za mashauriano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa letu

Hatukuenda kuzungumza hoja yoyote, moja baada ya nyingine. Kwamba nchi hii tukubaliane ni yetu sote, wao wapo kwenye uongozi na utawala wa taifa, sisi ni chama kikuu cha upinzani, na kuna watanzania wengine ambao sio wanachama wa vyama hivi lakini ni watanzania wenzetu

Na tulikubaliana kwamba tuna tatizo moja kubwa la kutokuaminiana kwa sababu tumekuwa na urafiki wa mashaka. Tumekua na urafiki wa mashaka na hakika tuna urafiki wa mashaka, hatuaminiani

Tukakubaliana, ili kuvuka kikwazo hicho, lazima kila upande ujaribu kujenga kwa mwenzake, na majibu yatapatikana kwa wakati, sio jambo au tukio la siku moja. Hilo lilikua la kwanza la msingi

20220316_134245.jpg

IMG-20220316-WA0061.jpg
FB_IMG_1647426182627.jpg
FB_IMG_1647426237039.jpg


20220316_134242.jpg
 
Naamini moja ya maazimio ya hiyo Kamati Kuu itakuwa ni lini Baraza Kuu la chama chao litakaa kuamua rufaa za wale wanawake 19 ili ule mjadala ufungwe rasmi kwa upande wa chama chao.
 
Lissu anafanya consultancy na UN, lema Anafanya kazi ndo maana walikataa kazi za jalalani za yule Mchawi wenu.

Lima upate kula dadangu au tafuta danga lingine.

Kwani UN ni shirika la siasa au branch ya Chadema!???
Ndivyo mnavyodanganyana huko ufipani!??
 
Relax mkuu utakufa na presha, chama ni watu sio majengo!ccm hadi leo wale maadui bado wametamalaki after more than 60yrs ya utawala went,ujinga umasikini na maradhi na rushwa ndio catalyst yenu,fufueni kwanza vile viwanja vya mpira wa miguu kuanzia majimaji hadi kirumba
Chama ni watu pamoja na vitendea kazi, huwezi kukwepa majengo.
 
Kikao cha Kamati Kuu ya chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiendelea muda huu, ikiongozwa na Mh. Freeman Mbowe muda huu.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama wakiwa ukumbini wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa kikao hicho iliyotolewa na Mwenyekiti Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe.

View attachment 2152766
View attachment 2152754View attachment 2152755View attachment 2152756

View attachment 2152765
Polisi wanahabari? Mbona hawajawavamia na kuwakamata kwa kufanya mkusanyiko kinyume na sheria!
 
Back
Top Bottom