Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Karibu shujaa Lissu tunakusubiri kwa hamu!Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumatano,
Katika Jiji hili kuu la Kibiashara la Dar es Salaam leo majira ya saa 7:35 mchana anatarajiwa kutua mwanamapinduzi wa kweli Tundu Antipas Lissu ambaye anarejea nchini mwake baada ya kulazimika kuwa uhamishoni kwa takriban miaka 6 kutokana na Jaribio la kutaka kumuua.
Tundu Lissu mpinzani mkuu wa aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania John Magufuli anarudi nchini baada ya mazungumzo ya Maridhiano ya kisiasa yanayoendelea kati ya CCM na Chadema yaliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitangaza mwanzoni mwa mwezi huu kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya hadhara lililowekwa kinyume na Katiba na mtangulizi wake John Magufuli.
Mapokezi ya Mwanasiasa huyo mashuhuri yataongozwa na Jabali la Siasa za Tanzania na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Viongozi mbalimbali wa chama hicho na wafuasi wa Chadema waliojiandaa kufanya maandamano makubwa ya kumpokea.
Maandamano hayo ya Mapokezi yatakwenda moja kwa moja Mpaka Uwanja wa Bulyaga Temeke Mwisho ambapo umeandaliwa Mkutano mkubwa wa Hadhara utakaohutubiwa na Lissu kuanzia saa 8 mchana.
Kama kawaida yetu sisi wa Molemo Media tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika Mapokezi hayo tangu anabusu ardhi ya Tanzania na Kisha Mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Temeke Mwisho.
Akizungumza na waandishi wa Habari hapo Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mapokezi ya Lissu Home Coming Mchungaji Peter Msigwa aliyekuwa ameambatana na Katibu wa Kamati Catherine Ruge alisema maandalizi yote yamekamilika na Watanzania watarajie mapokezi makubwa kuwahi kutokea hapa nchini.
Msigwa alisema chama kimeandaa mapokezi hayo kutokana na mazingira yaliyomlazimisha Lissu kukimbia nchi yake na Sasa anarudi nyumbani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuanza kurejesha nchi katika ustaarabu wa kisiasa unaotakiwa.
Kamati hiyo pia inaundwa na Baraka Mwago ambaye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani.
Karibuni Sana!
Ofisii hazikaliki Kwa sasa,Kazi imeshaanza au hujasikia utenguzi jana?
Chongolo amesema Waziiri asiyeweza kutatua matatizo na kuishia kulalamika ATUPISHE!
Sasa unaletewaje picha wakati bado hajafika au unataka apige selfii akiwa angani kisha atume?Tuleteeni Mipicha picha kama ya mbatizaji
[emoji38][emoji38][emoji38]Sasa unaletewaje picha wakati bado hajafika au unataka apige selfii akiwa angani kisha atume?
Ngoja Tusubiri tuone !!Kazi imeshaanza au hujasikia utenguzi jana?
Chongolo amesema Waziiri asiyeweza kutatua matatizo na kuishia kulalamika ATUPISHE!
Anayesema yamedoda ndio athibitisheWapwa mliopo Airpoti nikweli mapokezi yamedoda ya Lissu
Fanyeni unyama wa kapicha kama vipi tuondoe ubishi
Kamanda kishatua .