Yanayojiri miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar 26/4/2015

Mwaka jana maadhimisho kama haya yalikua weekend wakatangaza j3 mapumziko. Haya tuone leo
 
Nimefurai ITV ku-mute sauti baada ya kusikia brassband ikiimba iena iena.. ccm nambari one.
 

Hawana tofauti kubwa kimbinu..ila wanatofautina katika medani hao marine wamebobea kwa undani katika upambanaji katika maji hao wenye kofia nyekundu au Komando wao wamebobea kufanya kazi kwa kila hali yaani majini,ardhini na angani.Hiki kikosi maalum cha majini hakikuwepo ila imepaswa kuwa na kikosi kama hicho ili kubadili mfumo wa jeshi letu la majini kuwa na askari wanaoweza kufanya mashambulizi ya hali ya juu na uweledi kwa adui.
 
viwanajeshi vya ccm vimepewa navyo bunduki wanazuga chipukizi
 
Ndugu zangu leo ni siku ya muungano wa tanzania ambapo siku kama ya leo Tanganyika na Zanzibar Ziliungana na ndipo tulipopata nchi inayoitwa Tanzania ambayo wote leo tunajivunia kama kisiwa cha amani na upendo na utulivu.

Leo mhe rais alikagua gwaride la heshima la sherehe za muungano amabzo zimekuwa za mwisho kwake kuzikagua kama rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania isipokuwa takuwa akienda kwenye sherehe hizo kama rais mstaafu. sherehe hizo ambazo ziliambatana na shughuli mbalimbali leo kma ngoma za asili halaiki ya watoto waliokuwa wakitengeneza maumbo mbalimbali kama mlima kilimanjaro na majengo ya mji mkongwe Zanzibar n.k

pia kulikuwa na maonesho ya vikosi vyetu mbalimbali majeshi ya ulinzi na usalama, waliopita katika viwanja vyetu vya uhuru kwa stahili mbali mbali, kiukweli kwa yeyote aliyekuwepo uwanjani atakubaliana pamoja na mimi kuwa rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa sana katika kulijenga jeshi letu kuwa imara bora na kisasa kiasi ambacho hata wale majirani wakorofi wanajua kuwa wakituchokoza watakiona cha mtema kuni.

Jk ameliongozea heshima jeshi letu kwa kazi nzuri zinazofanya za kulinda mipaka yetu na kufanikiwa kulinda muungano wetu na wananchi kwa pamoja, pia jeshi limeendelea kufanya vizuri katika nchi mbalimbali chini ya mwamvuli wa UN, tuna vikosi Lebanoni, Dafur, Kongo ambapo wanajeshi wetu wameendelea kuwa mfano wa kuigwa.

Hata sisi tuliopo huku KITETO (KIBAYA) leo tulikuwa tumetulia majumbani mwetu tukiangalia mambo yalikuwa yakifanyika huko Dar es Salaam moja kwa moja kupitia TV zetu kwa stesheni mbalimbali tulipata burudani murua kutoka kwa vikosi vyetu haswa kile cha special force na kikosi cha makomandoo na halaiki za watoto ambapo leo tumeona mambo tofauti kutoka kwa watoto wetu.

ongera jk mungu akupe afya
 
Sasa wanapitisha vitoto vilivyofunfishwa ugaidi
 
Kikwete naona kama kadhoofu sana kiafya sasa hv
 
Huu ni wakati wa kuzidisha upendo miongoni mwetu na siyo kujenga hoja zinazojaza chuki.

Nashukuru mkuu Mr. G kwa kuweka sawa.
 
Tanzania Bara ndio nchi gani na rais wake ni yupi?

Kuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Jakaya Mrisho Kikwete. Akikagua parade ya sherehe za Muungano ambapo yeye ndiye kiongozi mkuu wa muungano huo tatizo linatoka wapi?

Zungumzia kubadili mfumo wa muungano ili uwe fair kwa pande zote mbili za Tanganyika na Zanzibar.

Ni uchochezi kwa kusema Zanzibar ni koloni la Tanzania Bara, nchi ambayo hata haipo kwenye ramani ya dunia.

With all due respect, I am so offended when I hear people referring to Tanganyika as Tanzania bara.. hii nchi haipo jamani.

Bring back our Tanganyika!
 
"Rais mtarajiwa" wa Muungano huu yuko wapi? Mkampeleka jogging imemkosesha sherehe kubwa hii!Ghafla tu afya badala ya kuimarika baada ya tizi ikadhoofu Watu wa CCM kweli wote ni Dhooofuuu..!!!!
 

Huko ndio kunaitwa KULEWA MADARAKA. Serikali ingekuwa sahihi kama kauli miu ingekuwa Jiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, na pia shirikia katika kupiga kura katiba pendekezwa na uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Lakini serikali kuwaelekeza watanzania kupigia kura ya NDIYO katiba pendekezwa ni ULEVI WA MADARAKA

Kuna Watanzania wanafikiri kwamba kufanya kampeni ya kura ya HAPANA ni kosa! Infact sheria ya mabadiliko ya katiba imetoa mwanya huo wa kufanya kampeini ya HAPANA na NDIYO ya katiba pendekezwa. Hivyo kampeni ya NDIYO haiko juu ya HAPANA zote zina equal chance na zinatakiwa ziwe treated equally kwa HOJA.

Lakini huu UKWELI CCM na serikali yake hawataki kabisa Watanzania waufahamu. SIO UHAINI KUIPIGIA KURA YA HAPANA KATIBA PENDEKEZWA.
 
Akili zenu zimejaa maji tuu, hivi unataka serikali iseme upigie kura ya hapana? Hiyo serikali itakuwa ya ajabu sana. Maana itakuwa na hela za kuchezea,

Lakini muda wa kampeni si bado?
Wao wanatoa wapi uhalali wa kufanya hivyo?
 
Huu ni wakati wa kuzidisha upendo miongoni mwetu na siyo kujenga hoja zinazojaza chuki.

Nashukuru mkuu Mr. G kwa kuweka sawa.
Mkuu matenene hakuna anayeleta hoja za chuki, hapa cha msingi ni kujadili hoja mezani ili tuwekani sawa baadhi yetu
 
Last edited by a moderator:

These guys are done bro ngojea utaona hasira za wananchi
 
Hakuna anyeleta uchochezi hapa, cha msingi ni kujadili kwa kina kama Muungano huu ni wa kweli au wa kinyonyaji, kama ni wa kinyonyaji basi serikali 3 haziepukiki
 
"Rais mtarajiwa" wa Muungano huu yuko wapi? Mkampeleka jogging imemkosesha sherehe kubwa hii!Ghafla tu afya badala ya kuimarika baada ya tizi ikadhoofu Watu wa CCM kweli wote ni Dhooofuuu..!!!!

Mkuu Lowassa yuko Dubai amealikwa kwenye sherehe kama hii inayoendelea!!
 

Attachments

  • 1430048971882.jpg
    77.5 KB · Views: 245
Kikwete naona kama kadhoofu sana kiafya sasa hv
Haha..anapiga mahesabu jinsi ya kumwambia mwenzie inatosha kumsafisha?Chezea mkwere na suruali fupi wewe...ZItto,JK,Kova and the type..midomo haifunguki ktk kumpa ------ haki yake au malipo yake.Lowasa hakusoma sana upepo huu...atasikilizia Bashe,Aya..toullah,Jk,kova, na wengine wa kabila hiyo watakavyokuwa baridi ktk kubariki haramu yake.Wakati yeye alibariki haramu yao.
 
Wale vijana wa kamba,,wakisoma,wasipopatiwa ajira ,,ni hatari kwa taifa Ccm na serekali yenu mjipange
 
Unakosea sana mkuu ingawa hoja yako ina mashiko. Hakuna nchi duniani iliyopo au iliyowahi kuwepo ikiitwa Tanzania Bara. Nchi iliyokuwepo na bado ipo katika Historia ni TANGANYIKA. Sehemu yoyote panaposomeka kama Tanzania Bara naomba u-edit na kuandika TANGANYIKA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…