JANA HIYO[emoji1313][emoji1313]ALIYEANZA UCHOKOZI NI ISRAEL
Umoja wa Mataifa walaani shambulio la utawala wa Kizayuni kusini mwa Nablus
Oct 07, 2023 07:56 UTC
[
https://media]
Umoja wa Mataifa umelaani shambulio la karibuni la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wakazi wa Kipalestina kusini mwa mji wa Nablus.
Ili kufikia malengo yao ya kujitanua na kupora ardhi zaidi za Wapalestina, Wazayuni kila siku hushambulia maeneo tofauti ya Palestina na kuwakamata, kujeruhi na kuwaua shahidi kwa madai ya uwongo na yasiyo na msingi. Vikosi vya muqawama navyo hujibu jinai za utawala wa Kizayuni kwa kutekeleza operesheni za kulipiza kisasi.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Jazeera, Tor Winsland, mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Asia Magharibi amelaani mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel katika mji wa Hawara kusini mwa Nablus usiku wa kuamkia jana Ijumaa, ambapo vijana wa Kipalestina walipambana vilivyo na askari wa utawala huo.
Wapalestina 19 wamejeruhiwa hadi kufia sasa katika shambulio hilo.
Katika mapigano hayo, vijana wa Kipalestina wamechoma moto kituo kimoja chenye mfungamano na majeshi ya utawala ya Kizayuni.
[https://media]Askari wa utawala ghasibu wa Israel wakiwashambulia Wapalestina
Labib Mohammad Zamidi, ambaye alijeruhiwa kwa risasi ya moja kwa moja kutoka kwa walowezi wenye silaha katika makazi ya Hawara, aliuawa shahidi Ijumaa asubuhi.
Huyo ni kijana wa nne kuuawa kwa kupigwa risasi za moja kwa moja na Wazayuni katika muda usipungua saa 24 zilizopita.
Uvamizi wa walowezi hao unafanyika kwa uungaji mkono kamili wa vikosi vinavyoikalia kwa mabavu mji mtakatifu wa Quds, hatua ambayo imeibua mapigano makali na ya umwagaji damu kati ya vijana wa Kipalestina na wa Kizayuni.
Hali ya karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu hususan katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni tata sana, ambapo wapiganaji shupavu wa Palestina wanajibu jinai zisizo na idadi za Wazayuni kwa njia yoyote ile wanayoweza, jambo ambalo limeibua hofu kubwa miongoni mwa walowezi wa Kizayuni.
Haki za wananchi madhulumu wa Palestina zimekuwa zikikandamizwa na utawala ghasibu wa Israel kwa zaidi ya miaka sabini. Katika kipindi hicho utawala huo umefanya jinai za kikatili na za kutisha dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.