LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
F7iS2rVW0AAxkh2.jpeg

Wanawasalimia. Baba na mama
 
Jasmoni Tegga Kwahiyo Israeli waliwapora waPalestina ardhi mwaka 1947 kijeshi kwa msaada wa Marekani (under UN disguise) , Sivyo? Kwmaba katika partition Israeli alipewa 95% ya Ardhi na Palestine akaachwa kwenye kaukanda ka Gaza, sio? Au hiyo partion ilikiwa asilimia ngapi kwa ngapi?
Uamuzi ulipitishwa na Baraza Kuu la UN (Nov 1947), ikiwemo Marekani na USSR.

Ardhi ya Palestina zaidi ya nusu (56%) ilikabidhiwa kwa Wayahudi, huku Yerusalemu ikiwekwa chini ya usimamizi wa kimataifa.

Wayahudi walikubali mpango huo, lakini Waarabu wakakataa kuuafiki.

Mapigano ya Wayahudi na Waarabu Palestina yakazuka mara tu baada ya uamuzi wa UN.

Kufuatia vita hivyo, Israeli ilifanikiwa kuchukua maeneo mengi ya Waarabu wa Palestina, ikiungwa mkono na Mfalme Abdullah wa Transjordan (Jordan kwa sasa), ambaye hakupenda Palestina iwe nchi huru kwa sababu ya maslahi binafsi ya kutaka kuimiliki yeye.

Hadi kufikia mwaka 1950 (miaka 3 tu baadaye) Israeli ilikuwa ikimiliki 77% ya ardhi ya Palestina. Mfalme Abdullah alikuwa amejitwalia Mji wa zamani wa Yerusalemu na eneo la kati la Palestina (sasa yajulikana kama West Bank).

Wakati huu ni Waarabu wapatao 160,000 pekee ndio walikuwa wamesalia katika maeneo yaliyokuwa yakitawaliwa na Israeli.
 
Uamuzi wa HAMAS kuishambulia Israel ulikuwa hauna busara, sababu Gaza strip ilivyo ukibananishwa huna pa kukimbilia, yaani HAMAS watakamatwa kama kuku bandani.

Nenda kwenye ramani uangalie vizuri ukanda wa Gaza ulivyo - exit ni mbili tu - either ukimbilie Lebanon, Mistri ama Syria ambapo ni km nyingi mno kutoka Gaza na check points za kutosha on the way.

Sasa fikiri mipaka yote imefungwa yaani banda limefungwa sasa ni muda wa kukimbiza kuku - aisee hali ni mbaya. ka ukanda haka hakana ulinzi wa anga, hakuna maji wala umeme wa kujitegemea - kila kitu kiko linked na Israel na ndiyo wameminya kitufe - hamna kutoka hamna kuingia - yaani nje ntinti & ndani ntiti.

Si jambo la mzaha, ndugu zangu Gaza ni damu - Israel ni damu.
Vita sio lele mama.
 
Sasa kinachokufanya utukane ni kipo? Wewe unawafahamu Wayahudi kuliko Wapalestina? Wapalestina wenyewe wanajua kuwa Wayahudi wamekuwa nao pale miaka yote walikua wamegawana maeneo ya kukaa, wanachokidai ni baadhi ya maeneo wanayogombania ambayo kila mmoja ana historia nayo, pia maeneo mengine ni yale ambayo Israel aliyachukua na kuyakalia kimabavu kwa sababu za kiusalama.
Halafu unaibuka wewe kutoka sijui mashimo ya wapi huko na ubishi wako wa Kiswahili baada ya kushiba kande ngumu unajitoa akili kuongea vitu ambavyo inabidi mtu atumie hekima kukujibu kama ninavyokujibu. Otherwise mwingine anaweza akakuona umerukwa na akili tu.
Sera ya kuifuta Israel kwamba pale siyo kwao hiyo haijawahi kuwa sera ya wapalestina, sababu wanajua fika kuwa wale wapo nao pale miaka yote. Sera ya kuifuta Usrael wala siyo hata ya waarabu wote, hiyo ni sera ya Iran na baadi tu ya waarabu.
Ukifundishwa na mwenye chuki lazima aiharibu akili yako. Kwa kifupi unaweza kusema waalimu wenu waliowafundishe mgogora wa Israel na Palestina walizif%i#r@ akila zenu badala ya kuzifundisha na sasa mmebaki kuwa mashoga wa kiakili
Achana nae huyo
Hana analojua ndo maana full kutukana baada ya kuona walichokitegemea Kwa isarel hakijatimia
 
Achana nae huyo
Hana analojua ndo maana full kutukana baada ya kuona walichokitegemea Kwa isarel hakijatimia
kwa miaka mingi wamekuwa wakipotosha watu humu kwa historia zao za kuchonga tulikua tunawaangalia kama hatujui.
Binafsi sikuwahi kufikiria nitakuja kuandika kuhusiana na mgogoro ule pamoja na kuujua kiundani.
This time nimelazimika sababu yanayotokea pale ni serious kwa pande zote halafu wansibuka watu kujadili kwa misingi ileile ya chuki na kupotosha.
Haiwezekani kutafuta achievements kupitia chuki na upotoshaji.
Watu wanakufa, binaadam anadharirika heshima ya mtu inaondolewa halafu watu wanadhani chuki na upotoshaji ndiyo vitatuliza hali ya mambo. Hawajui sumu wanayoitengeneza.
Waarabu ndiyo wamewaharibu kabisa Wapalestina, Wamewafanyia Wapalestina Arabanization mpaka sasa huwezi kupitia utamaduni ukamtafuta Mpalestina umtofautishe na Mwarabu.
Ni rahisi sana kwa Mpalestina kuoa au kuolewa ma Myahudi kuliko Mpalestina kuoa Mwarabu. Hayo hawayaoni kabisa,
 
Hofu na mkanganyiko umeibuka huko Gaza, baada ya Jeshi la Israel kuwaambia zaidi ya Wapalestina milioni 1 waliokwama Kaskazini mwa eneo lililozingirwa kuhamia Kusini, ndani ya saa 24 kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa.
 
Isiwe taabu, tunaondoka....HAMAS pambaneni na wanaume wenzenu.

Katika picha mtoto anaonyesha aama ya Piece na Love na sisi tunamwambia "mwaaa.."

1697185483770.png
 
Waarabu ndiyo wamewaharibu kabisa Wapalestina, Wamewafanyia Wapalestina Arabanization mpaka sasa huwezi kupitia utamaduni ukamtafuta Mpalestina umtofautishe na Mwarabu.
Ni rahisi sana kwa Mpalestina kuoa au kuolewa ma Myahudi kuliko Mpalestina kuoa Mwarabu. Hayo hawayaoni kabisa, kumbafu zao
Technically, hakuna tofauti kati ya Mpalestina na Mwarabu. Wote ni Waarabu.

Kuna Waarabu wa Saudi, Syria, Yemen, Palestina etc.

Palestina ni geographical location ambapo wakazi wake wanaitwa Wapalestina.
 
Technically, hakuna tofauti kati ya Mpalestina na Mwarabu. Wote ni Waarabu.

Kuna Waarabu wa Saudi, Syria, Yemen, Palestina etc.

Palestina ni geographical location ambapo wakazi wake ni Wapalestina.
Technically, yeah nakubaliana na wewe.
Wapalestina sasa hivi hawana culture tofauti na ile ya Mwarabu.
Ila, wakisimama Mpalestina na Mwarabu, just kwa kuwaangalia unaweza kuwatofautisha bila kupepesa.
 
Back
Top Bottom