LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Technically, yeah nakubaliana na wewe.
Wapalestina sasa hivi hawana culture tofauti na ile ya Mwarabu.
Ila, wakisimama Mpalestina na Mwarabu, just kwa kuwaangalia unaweza kuwatofautisha bila kupepesa.
Nilishtuka uliposema Waarabu wamewaharibu Wapalestina, wakati wao wenyewe kwa asili ni Waarabu na wamekuwa Waarabu muda wote (at least from 638 AD Jihad Wars of conquest where most of the cultures and people in the Middle East were forced into Arabanization).
 
UMEONA HAMAS WALIVOKUWA WAPUMBAVU, ISRAEL MILLITARY WANAWAAMBIA WATU WA EVACUATE NORTHERN GAZA WAO WANAWAMBIA MSIONDOKE, WANATUMIA WATU KAMA HUMAN SHIELDS, ALAF KUNA WATU MNAKUJA HAPA KUWATETEA.

INAKUAJE ISRAEL MILLITARY INAJALI MAISHA YA WATU WA GAZA KULIKO HAMAS??

ALAF WATU WAKIULIWA KWA MABOMU WANAWAREKODI WANAPOST MITANDAONI.

YAAN KAMA MTU ANAWEZA KUCHUKUA KISU AKAMCHINJA MTU AU AKAKATA KICHWA CHA MTOTO, WE UNADHANI ATAJALI MAISHA YAKO ATAKAMA WE NI MWARABU MWENZAKE.

MI NINACHOJUA NI KITU KIMOJA, MUUAJI NI MUUAJI TUU, AKIMALIZA KUUA MAADUI ZAKE ATAKUJA KUKUUA NA WW TUU HATAKAMA NI RAFIKI AKE.

"THERE IS NO HONOR AMONG CRIMINALS"


View: https://twitter.com/spectatorindex/status/1712734501162582499?t=3-16VrcRPKHYqmMAC0KHyA&s=19
 
Kuna vitu vinalipuka juu ya anga ya gaza haijulikani kama ni camical bomb au nini tusubiri matokeo,
pray for palestian
 
Wapalestina waliupokea Uislam, then wakaufuata uarabu. Chochote kuhusiana na utamaduni wao walikiacha kwa kuwa havikufaa tena na mbele ya usilam vilikua ni kama upagani.
Wakalazimika kuanza kuufuata uarabu, ilikua ni rahisi kwa kuuishi Uislam Kupitia utamaduni wa kiarabu.
 
Watu wengi wanapojadili mzozo kati ya Israel na Palestina,wanajadili wakiwa tayari wamegeemea upande fulani kwa sababu wanazozijua wao,huku wakipuuzia ukweli ulivyokuwa nyakati za zamani na sasa.
Kabla sijaeleza namna gani wahafidhina wanavyochochea mzozo kati yao,kwanza niainishe uhalisi katika mtiririko ufuatao.

Wote,wayahudi na wapalestina wamekuwa wakiishi katika miji ya Yerusalem,Bethlehem, Betania,Yeriko, Hebron,Samaria,Gaza,Galilaya na mingine..,miji iliyopo katika nchi za Israel na Palestina kwa sasa kabla ya kuja kwa mataifa yaliyowatawala na kuwaburuza.

Kimsingi wameishi pamoja kwa karne nyingi sana katika eneo hilo mwa mtindo wa kuhasimiana na kupatana kabla hayo maeneo kuitwa Palestina na Israel.

Baadhi ya Wayahudi,wapalestina na wakazi wengine wa maeneo ya Lebanon,Syria na Jordan katika kipindi fulani miaka ya nyuma waliondoka kwa wingi na kwenda kuishi nchi za mbali na kwao.
Lakini pia baadhi yao, Wayahudi na Wapalestina walibaki katika hilo eneo. Matokeo ya safari zao hizo leo hii yamefanya kuwe na Wapalestina na Wayahudi wanaoishi nje ya nchi yao(diaspora) kuwa wengi kuliko wanaoishi ndani. Wayahudi wanaoishi nje hadi sasa ,hususan America,America ya kusini na Ulaya wanakaribia milioni 6.5. Wapalestina wanaoishi nje hadi sasa ni milioni 7..,wakati wanaoishi ndani milioni 5 tu.

Mkoloni wa mwisho kutawala ,Uingereza, ndiye aliyelipa jina la Palestina eneo hilo...kama ambavyo alivyolipa jina la Tanganyika eneo letu hili. Wapalestina wakafurahi, Wayahudi hawakufurahi.
Wayahudi hawakufurahi kwa vile waliona hilo jina la nchi lingewapa Wapalestina fikra kwamba nchi ni yao,ukizingatia wamekuwa wakiishi kwa kutoaminiana na kuhasimiana kwa miaka yote.
Wayahudi wakaanza ushawishi ili wapate nchi yao peke yao...na wakafanikiwa. Wapalestina nao hawakukubali,wakaendelea kudai wapewe haki ya eneo lao kuwa nchi...Matokeo yake yanajulikana.

Sasa tuiache historia hiyo ya zamani, turukie hali ilivyo miaka hii,katika muda ambao tayari kuna nchi ya Israel na Palestina..ambapo nasema kama kungekuwa hakuna wahafidhina pande zote kati yao suluhu ingekuwa imefikiwa muda mrefu.
Kama kusingekuwa na wahafidhina pengine hata wangeweza kuunganisha maeneo ya miji yao yote na kuishi pamoja kama nchi moja kama walivyoishi kwa zaidi ya miaka 3000 hapo zamani,wakitofautiana kwa tamaduni na desturi tu,lakini wakifanana kwa mengi.
Ikumbukwe,waarabu walipovamia na kutawala hilo eneo lao ndipo Wapalestina wengi wakawa waislam na kuiasili lugha ya kiarabu ya watawala,lakini wenzao Wayahudi wakagoma,wakashikilia desturi zao.

Ndani ya Israel,ukiacha Waislam 14% na Wakristu 2% ambao wengi wao ni Waisraeli-wapalestina, asilimia iliyobaki ambayo ni Wayahudi imegawanyika katika makundi manne ; Hiloni,Masorti,Dati na Haredi. Hiloni,ambao ndiyo wengi wanaishi bila misingi ya kidini(secular). Masorti,wanaishi kwa kufuata tamaduni za zamani. Dati wanaishi kidini. Haredi,ambao ni asilimia 8 tu,wameshikilia msimamo mikali ya kiimani na ni wahafidhina.

Haredi wanaamini kwamba kulitoa eneo lao lolote au kuacha kumiliki maeneo ya zamani ni kumkosea na kumkosoa Mungu aliyewapa eneo hilo.
Ikumbukwe mji wa Hebron ambao uko ndani ya eneo la Palestina kwa sasa,ndiyo ulikuwa makao makuu ya Mfalme Daudi,na ndiko eneo ambalo wazee wao wa kiimani wa zamani,Ibrahim, Isaka na Yakob walizikwa. Sasa wahafidhina Haredi siyo tu hawataki maeneo ya Israel yagaiwe,wanataka yaliyokuwa maeneo ya zamani kama mji wa Hebron,yarudi katika milki yao.
Siyo siri,ni Haredi ndiyo walipanga njama kumuua waziri mkuu wa Israel Yitzihak Rabin kwa kitendo chake cha kukubaliana na Palestina kurudisha baadhi ya maeneo waliyoyateka wakati wa vita ya mwaka 1967. Wahafidhina hao siku za karibuni wamekuwa wakipiga kampeni ili Yigal Amir,aliyemuua Rabin,aachiwe huru sasa.

Upande wa Palestina kuna makundi mawili yenye ushawishi kisiasa...,PLO, chama kinachoongoza nchi na Hamas,kinachoongoza ukanda wa Gaza.
PLO na Hamas,wote wana vikundi vya vya kijeshi. Kundi la tatu ni Islamic Jihad,ambao hawaendeshi shughuli kisiasa..wao ni kikundi chenye wapiganaji wenye silaha.

PLO na jeshi lao la Fatah wana msimamo wa wastani; na ndiyo hao wanaweza kufanya mazungumzo na na Israel kuhusu amani ya eneo lao.

Hamas na Islamic Jihad wanafanana kwa mambo mawili; wote walianzishwa kama matawi ya Muslim brotherhood ya Misri, na pia ni wahafidhina wenye misimamo mikali. Wakati Hamas wanakubali suluhisho la kuwe na nchi mbili lakini hawataki kuitambua Israel, Islamic Jihad wenyewe wanataka eneo lote la Israel la sasa lijumuishwe na kuwa milki ya Palestina...na Waisraeli waondoke kama sivyo wafutiliwe mbali.

Misimamo ya Hamas na Islamic Jihad wameirithi toka kwa chama kilichowaanzisha cha Muslim brotherhood. Kikundi cha Muslim brotherhood kule Misri,kimekuwa na msimamo wa kuiteketeza Israel kwa gharama yoyote. Misri walipoongoza nchi za kiarabu kuishambulia Israel, Muslim brotherhood wakafurahi sana. Lakini rais wa misri Anwar Sadat alipozuru Israel na kufanya mkataba wa amani,kikundi hicho kilighafirika na kuahidi kumuua. Walitekeleza azma yao mwaka 1981 kwa kumuua Sadat kwa risasi akiwa katika stadium. Mmoja wa wanachama wa Muslim brotherhood waliokamatwa kwa kuhusushwa na njama hizo ni Ayman Zahwahir ambaye alikuwa kiongozi masaidizi wa kundi la Alqaeda.

Wahafidhina hawa,Haredi upande wa Israel,pia Hamas na Islamic Jihad upande wa Palestina, ndiyo wanaofanya huo mzozo usipate suluhisho na kuishi kwa amani.

Tofauti na zamani wakati wakiishi kwa kutoaminiana, miaka hii ya karibuni misuguanao yao imepata mashabiki toka katika nchi nyingine,..wanaosaidia na kukuza misuguano yao bila sababu. Kuna mataifa yanaipendelea Israel, na kuna mataifa au watu wanaoipendelea Palestina bila kuwa na hoja za msingi.
Mathalan,kuna watu wanasema ardhi yote ile ni mali ya Israel,kwa vile walipewa na Mungu wao..watakuonesha ushahidi wa maandishi katika kitabu. Hoja dhaifu.
Kuna watu pia wanasema ardhi yote ni ya Palestina kwa vile Mkoloni Uingereza aliwapa wao hadhi hiyo..na kwamba wao wayahudi walitoka. Hoja dhaifu. Yaani utoke katika eneo lako na kuwaacha baadhi ya ndugu zako katika eneo ,kisha urudi ukute eneo lako kuna muhuni anayeitwa mkoloni analiita eneo lako lile lile jina jingine,kisha yule uliyekuwa unaishi naye eneo moja akuambie wewe sasa hivi huhusiki kwa vile tumebadili jina.; utakubali?

Nchi za Africa mashariki kwa pamoja zimepinga mkataba wa kikoloni uliokuwa ukizuia nchi zao kutumia maji ya Ziwa Victoria na kwamba mwenye haki ya kutumia maji ya mto Nile ni Misri pekee...,lakini baadhi ya watu hao hao wanataka Israel iheshimu mipaka ya kikoloni.

Mpaka wa ziwa Nyasa kati ya Malawi na Msumbiji unapita katikati ya ziwa,lakini Malawi wanadai ziwa lote upande wa Tanzania ni mali yao,kwa hiyo watanzania hawana haki ya kutumia maji hayo hata kamayamegusa ardhi yao,..wanasema wanafuata ramani ya mkoloni Muingereza. Tanzania haitaki kusikia ujinga huo wa mkoloni,wanatumia maji kama kawaida na wako tayari kupigana kwa hilo. Lakini baadhi ya watanzania wanapata ujasiri wa kuiambia Israel iheshimu mipaka ya kikoloni.

Namaliza kwa kusema Wayahudi na Wapalestina wanaweza kabisa kuishi eneo moja huku kila mtu akishika tamaduni na desturi zake kama zamani ..na kama ilivyokuwa kwa Ujerumani magharibi na mashariki,zilizokuwa nchi mbili hasimu lakini sasa zimeungana na kuwan nchi moja. Wanaozuia hilo ni wahafidhina tu.
Na sasa kuna mashabiki wahafidhina toka nje ya eneo lile wanaowashwa na pilipili wasiyoila,..wengine wako huku Afrika.
 
WANATUMIA WATU KAMA HUMAN SHIELDS, ALAF KUNA WATU MNAKUJA HAPA KUWATETEA.
exactly, this is what has been practically happened in the past decades. Sasa baada ya muda kuisha wa evacuation ya hiari Gaza kwa innocent citizens watakaobakia wote ni HAMAS, hapo ndipo kwata litakapoanza rasmi - unapigwa ground na air - at the same time jiji ni giza, maji hakuna, mawasiliano hakuna, hosp zimefungwa.

Kama Hamas wakitoboa, basi hakuna wa kuwaweza Duniani.
 
Kimsingi wameishi pamoja kwa karne nyingi sana katika eneo hilo mwa mtindo wa kuhasimiana na kupatana kabla hayo maeneo kuitwa Palestina na Israel.
acha fix, myahudi na mfilisti lini waliishi pamoja ndugu. Phenicie ndiyo wafilisti na ndiyo hawa wanajiita waparestina wa leo.

 
sasa hapo ndio patamu. alikuwa anasubiriwa kwa hamu sana. though kwa akili yake anafikiri kweli israel ingeenda kumpiga kwa ground invasion? ni kwa madege tu. na iran anachotegemea sana ni hamas na hezbolah kwamba watakuwa wanamsaidia.
Kwani iran hana ndege, drones Nk? Tena anadrones za kisasa sana
 
Your browser is not able to display this video.

More American military aids arrive to Israel occupation to support their crimes against civilians in Gaza.

Misaada zaidi ya kijeshi ya Marekani yawasili katika eneo lililokaliwa na Israel ili kusaidia uhalifu wao dhidi ya raia huko Gaza.

Marekani ni Cancer ya dunia.
 
wamumuwahi Iran, unajua mawazo ya iran ilikuwa, Hamas waingie kama walivyoingia kusini, kaskazini wawepo hezbolah, na israel akichoka, Iran iingilie kati kuimaliza Israel. wenzake wamegundua hilo, wakaleta mameli ya vit ana kujiweka tayari kwa lolote hata kabla hamas hajasumbua sana na hezbolah hajasumbua. aliyotarajia yamedondokea pua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…