LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Kwahiyo nini kilitokea 1947 ghafla wakawa taifa?
Mwaka 1947 Umoja wa Mataifa ulipiga kura kuigawa ardhi ya Palestina kuwa nchi mbili. Wayahudi ambao idadi yao ilikuwa 650,000 walikubaliana na uamuzi huo na kutangaza rasmi kuunda Taifa la Israel mnamo 14 May 1948 chini ya David Ben Gurion ambaye alikuwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kizayuni Duniani (World Zionist Organization)


Wapalestina (Waarabu) ambao idadi yao ilikaribia 1,200,000 waliuchukulia uamuzi huo kama muendelezo wa mkakati wa muda mrefu wa Wayahudi kuwaondoa katika ardhi zao waliukataa mpango huo. Huo ndio ukawa mwanzo wa Mgogoro wa ardhi unaoendelea sasa baina ya Wapalestina na Waisrael. Wanamgambo wa Wapalestina wakisadiwa na mataifa ya kiarabu ya Misri, Jordan, Iraq na Syria walitangaza vita dhidi ya Israel mnamo tarehe 15 May, 1948.Vita vilimalizika tarehe 10 March 1949 kwa Israel kushinda na kunyakua ardhi zaidi kutoka mikononi mwa Wapalestina ambao wengi wao waliuawa na zaidi ya laki saba (700,000) kulazimishwa kuondoka katika ardhi zao hali iliyopelekea waishi katika makambi ya wakimbizi tatizo ambalo hadi sasa bado halijapata ufumbuzi.
 
Sasa mbona kama unatuambia sisi wkt wameambiwa wapalestina?ebu tuone kama hawataweza...wanaweza kutia tia huruma wakaongezewa masaa mengine 12
 
Yupi ni mcokozi kati ya Israel na Palestine juu ya kile kinacho endelea pale middle east?
Israel ndo mchokozi na mvamizi. Imagine anapigana vita na watu ambao anawakalia kimabavu, ambao hawawezi kutoka mpaka kwa amri yake, halafu kawakatia umeme, maji na kazuia madawa, nyie israehell ni washenzi na waoga
 
Hamas ndiyo walioanzisha mashambulizi dhidi ya Israel na sasa Israel inajibu mapigo kwa nguvu zilizopitiliza!
 
Hellow guys.
kupitia michango ya wadau mbalimbali kupitia vita hivi basi kuna hatua muhimu ambazo serikali inapaswa kuzichukua.

1-Ifatilie kwa karibu saana mafundisho yanayotolewa kwenye dini zetu zote.
2-Serikali iwe na mkono wake kwenye vikao,mikutano na mikusanyiko ya dini zote na ikibidi kabla ya kutoa vibali vya vikao na mikutano basI hata ajenda za wanachoenda kujadili zijulikane.
3-Missionary personally wote kutoka nje wanaokuja kuhubiri katika dini zetu inabidi wafanyiwe vetting ya maana kabla ya kupewa vibali vya kazi.
4-Elimu ya uraia hasa uhusiano wa nchi(ardhi) na taifa(watu) ipewe kipaumbele mno kama somo la msingi.
5-Wakati wa ajali/maafa jamii ikumbushwe umuhimu wa kutoa msaada kwa wahanga badala ya kurekodi matukio au majanga kwa lengo la kupata engagement.
6-Viongozi wenye misimamo mikali sana ya kiimani WASIPEWE MADARAKA NA NAFASI NYETI KWENYE VYOMBO VYA MAAMUZI NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA
7-Watu wakumbushwe hakuna aliyewahi kumuona mungu ila waishi kwa AKILI katika matabaka yao.
8-Watu wakumbushwe kuivunja amani ni tukio la sekunde,dakika,saa au ikizidi siku.ILA mchakato wa kujenga na kuleta amani unagharimu VIZAZI VINGI.
 
Kwahiyo Israel ilipora zaidi ya ilichopewa na azimio, sio?
Kitu kama hicho.

Mara tu baada ya UN (1947) kupitisha mpango wa ugawaji wa Palestina baina ya Wayahudi na Waarabu, vikazuka vita -- na havijawaji kukoma.

Vita hivyo kwa sehemu kubwa sana vimekuwa na matokeo mabaya kwa upande mmojawapo -- ardhi kumegwa, ongezeko la Wayahudi wahamiaji, wakimbizi kwa upande mwingine, uendelezaji wa makazi mapya, sheria kandamizi dhidi ya upande hasimu, na fursa ya kujitanua kijeshi, kisiasa, diplomasia na uchumi.

^To the victor goes the spoils^
 
Sasa mbona kama unatuambia sisi wkt wameambiwa wapalestina?ebu tuone kama hawataweza...wanaweza kutia tia huruma wakaongezewa masaa mengine 12
Hata wangeweka wiki nzima bado haitoshi watu milioni 1 na laki 2ni wengi usichukulie kirahisi.
 
Israel ndo mchokozi na mvamizi. Imagine anapigana vita na watu ambao anawakalia kimabavu, ambao hawawezi kutoka mpaka kwa amri yake, halafu kawakatia umeme, maji na kazuia madawa, nyie israehell ni washenzi na waoga

Soma historia vzr acha ushabiki maandazi,wote niwavamizi,cha msingi atakayeshinda achukue ardhi.
 
And this is it
Hata kwenye biblia ndivyo ilivyo...
Watu wabishi wanakuja hapa na ngonjera za 1947
Wakati ilianzia kabla ya Yesu......

Anyway,haya mambo hayapo kimwili zaidi km wanavyoona , ndo maana tunacheka sbb tunajua it's a spiritual thing....
 
waeleze mkuu.
Naangalia news hapa
Mamia ya wapelestina wanaondoka Gaza!
Na baadhi ya nchi zimeomba raia waongezewe muda wa kuondoka
Muondoke tu mkifa wenzenu wanakula nchi tu!
 
Unajua ni marangapi wapalistina walitawala Israel mkuu au kwakua Una iko kijiramani unadhani ndio basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…