LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
AGITATOR.
Hivi wapalestina waliwakosea nini wayahudi mpaka wawafanye wakimbizi/watumwa ndani ya nchi yao.
Hakika ukinijibu vizuri nitakurushia voucher ya elfu tano.
Hakuna sabau ya kuua watu huvyo ni roho mbaya tu. Tourati inasemma amri mbili kuu.
1. Sikia EeIsraeli Bwana Mu gu ni mmoja nawe Mpe xe Mu gu kwa moyo wako wotekwa roho yako yote na kwanguvu zako zote
Ya pili
2. Mpe de jirani yayako kama nafsi yako
Hii ndio jumla ya taurati yote na Manabii.
Sasa hapo upendo kwa jirani uko wapi ibada yoyote inayojenga chuki kwa mwenzako ni ibada ya kishetani.
Ndio maana manabii walisema " Siku zinakuja ambapo wale wanaoua wataona kama wanamtolea Bwana ibada, eti wanaua kwa jina la Mungu.
Israeli na Palestine wote ni watoto wa Mungu kwa Uumbaji na Ukombozi japowanatuo a sisi Afrika kama uzao wa laana Lakini wao wana LAANA KUBWA.
Ngano za kiyahudi zinadai mtu mweusi analaana toka kwa Hamu wakati yaliye laaniwa ni Kaanani.
Lakini ikiwa mtu anauamini mpango wa Mungu wa Ukombozi kupitia Yesu hakuna tena utengano.
Vita hii ni ishara dini yao ni mfu na dhaifu kabisa ambayo mtu hatatamani kuwa ndani yake.
 
Siku zote israel hupewa msaada mikubwa na US tangu mwaka 1947 ila leo kakikundi ambako kapo staless na kamezingilwa pande zote, kama "biggest open prison in the world" kana mtia hofu mpa kutumia siraha zito F 16 mbombandiments, wanajeshi laki tatu, hapo kuna jambo kubwa tusio lijua.
Ukiona mbwa anabweka kwa mbwembwe sana ujue mwenye mbwa hayuko mbali.
Ni kweli Hamas ni kakundi kadogo lakini jiulize kamepata wapi hizo nguvu na silaha? Kanapata wapi jeuri ya kupigana na Taifa kubwa duniani? Fikiri mara mbili. Na Israel siyo wajinga, hope wana info zote through their security channels. PM wao Ben hakuongea vile alivyoongea kwa kujifurahisha, usimfananishe na Bashite.
 
Ukiona mbwa anabweka kwa mbwembwe sana ujue mwenye mbwa hayuko mbali.
Ni kweli Hamas ni kakundi kadogo lakini jiulize kamepata wapi hizo nguvu na silaha? Kanapata wapi jeuri ya kupigana na Taifa kubwa duniani? Fikiri mara mbili. Na Israel siyo wajinga, hope wana info zote through their security channels. PM wao Ben hakuongea vile alivyoongea kwa kujifurahisha, usimfananishe na Bashite.
Israel ni taifa kubwa duniani!?..kubwa kwa lipi!?..wanaishi kwa misaada
 
Huo ni mtazamo wako tu usio na uhalisia, Rusia kamwe hawezi kuwatumia Hamas kumpiga muisraeli. Hivi ulishawahi sikia mahali popote Rusia na Israeli wanavutana?
Wakati wa Hitler Ulaya ilikuwa imeshaelekea Kibla, ni Russia pekee ndiyo aliyeresist kwa miaka almost 7 ama 8 .

Hatimaye Hitler alichemka vita na Urussi, mwishowe Urussi aliwasaidia sana mateka wa Israel waliokuwa UTUMWANI German.

Inaonekanaga sana Israel wanaliheshimu hilo.
Hawanaga uadui kihivyo, hata Ukrain War Israel kajivutavuta sana mpaka Zele akalalamika
 
Yupi ni mcokozi kati ya Israel na Palestine juu ya kile kinacho endelea pale middle east?
Kuanzia miaka ya 1880 Wayahudi wengi walianza kurejea Palestina na kujipatia ardhi na mijikoloni ya kilimo na makazi, tofauti na awali ambapo msukumo wao ulikuwa kwenda kwa lengo la kujihusisha kwenye utafiti wa masuala ya dini.

Mfano mwaka 1882 ulishuhudia kuingia kwa Wayahudi wengi Palestina kufuatia mateso waliyopata wakiwa Urusi.

Matukio mengine ni yale ya vita vya 2 vya dunia - Adolf Hitler na sera za Wanazi.

1881 (Wayahudi Palestina ~ 24,000)
1914 (~ 85,000)
1944 (~ 565,000)!!!
 
Benjamin Netanyau ana uchungu sana na haya magaidi ya kipalestina mdogo wake akiitwa Yonatan Netanyau aliuwawa kwenye operation entebe alipokuwa akiiongoza kikosi cha kuokoa ndege iliyokuwa imetekwa na magaidi ya kipalestina uokoaji ulifanikiwa 100% ila yeye Yonatan alipoteza maisha.
Si mdogo wake bana, Yonatan alikuwa mtoto wa kwanza.
 
Wakati wa Hitler Ulaya ilikuwa imeshaelekea Kibla, ni Russia pekee ndiyo aliyeresist kwa miaka almost 7 ama 8 .

Hatimaye Hitler alichemka vita na Urussi, mwishowe Urussi aliwasaidia sana mateka wa Israel waliokuwa UTUMWANI German.

Inaonekanaga sana Israel wanaliheshimu hilo.
Hawanaga uadui kihivyo, hata Ukrain War Israel kajivutavuta sana mpaka Zele akalalamika
Lakini pia huyo huyo Russia aliresist kwa msaada wa USA wa kupewa silaha za kutosha na usaidizi mwingine.Angekuwa peke yake pengine asingeweza himili pia.
 
Israel jana usiku ilifanya ambush ya ardhini kwenye baadhi ya ngome za Hamas kaskazini mwa gaza lakini haijamkuta mpiganaji hata mmoja wa hamas badala yake wamekuta baadhi ya mateka wakiwa wameuwa,haijabainika iwapo mateka hao waliuawa na mashambulizi ya anga ya Israel au Hamas ndo wame wauwa.
Wachambuzi wa mambo wana sema wenda Hamas imefanya tukio hilo makusudi kabisa kama onyo kwa Israel, hali hiyo imeiweka Israel kwenye wakati mgumu sana ni namna gani watawaokoa mateka bila kuhatarisha maisha yao.
 
Mwaka 1947 Umoja wa Mataifa ulipiga kura kuigawa ardhi ya Palestina kuwa nchi mbili. Wayahudi ambao idadi yao ilikuwa 650,000 walikubaliana na uamuzi huo na kutangaza rasmi kuunda Taifa la Israel mnamo 14 May 1948 chini ya David Ben Gurion ambaye alikuwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kizayuni Duniani (World Zionist Organization)


Wapalestina (Waarabu) ambao idadi yao ilikaribia 1,200,000 waliuchukulia uamuzi huo kama muendelezo wa mkakati wa muda mrefu wa Wayahudi kuwaondoa katika ardhi zao waliukataa mpango huo. Huo ndio ukawa mwanzo wa Mgogoro wa ardhi unaoendelea sasa baina ya Wapalestina na Waisrael. Wanamgambo wa Wapalestina wakisadiwa na mataifa ya kiarabu ya Misri, Jordan, Iraq na Syria walitangaza vita dhidi ya Israel mnamo tarehe 15 May, 1948.Vita vilimalizika tarehe 10 March 1949 kwa Israel kushinda na kunyakua ardhi zaidi kutoka mikononi mwa Wapalestina ambao wengi wao waliuawa na zaidi ya laki saba (700,000) kulazimishwa kuondoka katika ardhi zao hali iliyopelekea waishi katika makambi ya wakimbizi tatizo ambalo hadi sasa bado halijapata ufumbuzi.
Mgawanyo wa Ardhi walioufanya UN ilikuwa ni asilimia ngapi kwa Palestina na asilimia ngapi kwa Mazayuni mayahudi?
 
Kitu kama hicho.

Mara tu baada ya UN (1947) kupitisha mpango wa ugawaji wa Palestina baina ya Wayahudi na Waarabu, vikazuka vita -- na havijawaji kukoma.

Vita hivyo kwa sehemu kubwa sana vimekuwa na matokeo mabaya kwa upande mmojawapo -- ardhi kumegwa, ongezeko la Wayahudi wahamiaji, wakimbizi kwa upande mwingine, uendelezaji wa makazi mapya, sheria kandamizi dhidi ya upande hasimu, na fursa ya kujitanua kijeshi, kisiasa, diplomasia na uchumi.

^To the victor goes the spoils^
Kwahiyo katika hali ya uonezi kama huo, tunakubaliana kwamba mayahudi yanstahiki kila pigo wanalopata toka kwa Hamas, sivyo?
 
Kishanuka tusepe wanangu....

1697260569763.png
 
Back
Top Bottom