LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Chanzo cha kutoweka Amani si ni mayahudi kuchukua Ardhi zaidi ya waliyopewa na UN Sivyo?
Kuhusu Wayahudi kuongeza makazi na ardhi zaidi ya vile ilivyokuwa imeelekeza UN, bila shaka hapo Waarabu Wapalestina na UN yenyewe walaumiwe pia kwa ^kumsaidia^ Myahudi.

Umoja wa Mataifa kimsingi haikuchukua hatua thabiti kumzuia Myahudi asivuke mipaka ya maelekezo ya UN.

Isisahaulike kwamba huu ni wakati ambapo Wayahudi walikuwa wahanga wa mauaji ya halaiki ya Hitler na pia hakuna taifa lililokuwa tayari kuwapokea wakimbizi waliokuwa wamenusurika mauaji hayo ya kutisha. Kimbilio pekee la haraka lilikuwa Palestina.

Kwa upande mwingine, Palestina alikataa uamuzi wa UN wa kuigawa Palestina iwe nchi mbili, akaona suluhu ni ^mtutu wa bunduki^ -- ambao tunaweza kusema pengine hawakuwa nao au waliutunza kwa majirani zao Wayahudi walioibuka washindi kwenye vita na migogoro yote iliyofuata baina yao.

Iwapo Waarabu wa Palestina wangekubali kutambulika kama taifa huru katika maeneo yaliyokuwa yameainishwa na UN, nani ajuaye pengine hii ingewapa ushawishi na nguvu zaidi kwa mataifa mengine katika kudai ardhi ya ziada na kuitawala, na labda vita vingi na umwagaji damu vingeepukwa.

Kwa kiasi fulani Waarabu wa Palestina wameonekana kama nchi na utawala wa kigaidi, wamechukiwa sana na marafiki wa Wayahudi, sababu mojawapo ikiwa ni wao kukosa uhalali wa kuwa nchi huru inayotambulika rasmi na UN.

Tunaweza kusema kwamba Wayahudi walitumia fursa ya udhaifu wa Palestina ili kuendelea kujitanua zaidi.
 
Uwe na uhakika, Israel atatoboa hayo mahandaki tifutifu na kina haniya na midevu yao itatoka hai au maiti lazima kieleweke pale Gaza. R. I. P Hamas, wahini ahadi zenu zile pendwa kule Jannah firdaus
Friday's...paradiso
 
Kwahiyo siku utakapoamua kwa hiari yako kuwa shoga, wa kulaumiwa si wewe bali ni wale ambao hawakukuzuia usiingiliwe kinyume, sivyo?
 
Mkuu mbna jamaa kashusha hoja na Una mtusi, si hoja Kwa hoja au hoja Kwa tusi
Hoja yake ni kwamba mtu akifanya kosa , basi wa kuwajibishwa si mtenda kosa, bali ambae hakumzuia kufanya kosa. Sas animeijibu hiyo hoja kwa kutoa mfano juu ya hoja yake. Au huoni hoja katika huo mfano?
 
Hoja yake ni kwamba mtu akifanya kosa , basi wa kuwajibishwa si mtenda kosa, bali ambae hakumzuia kufanya kosa. Sas animeijibu hiyo hoja kwa kutoa mfano juu ya hoja yake. Au huoni hoja katika huo mfano?
Lakn hakukua na haha ya tusi... Hata Mimi nmeadhibiwa Sana Kwa nakosa ya wadogo zangu kuzingua nkiwatazama, nawalaumu UN waarab na USA
 
Lakn hakukua na haha ya tusi... Hata Mimi nmeadhibiwa Sana Kwa nakosa ya wadogo zangu kuzingua nkiwatazama, nawalaumu UN waarab na USA
Hamna tusi,bali hoja tupu. Kuadhibiwa kwa niaba ya mtu ni kwa mazingira ambayo mtendaji hajui kama analofanya ni kosa (mfano mdogo wako). Ila Wayahudi wanajua kabisa wanatenda uhalifu wa kishetani kabisa dhidi ya waPalestina, wanajua!
 
Your browser is not able to display this video.

Kuna cha kujifunza kwenye historia ya mgogoro huu
 
Katika tukio la kustaajabisha kunguru ameonekana kwenye video inayosambaa mitandaoni akiiondoa bendera ya Israel iliyokuwa ikipepea, tukio hilo linahusishwa na vita inayoendelea huko Israel na palestina. Ambapo inasemekana Kunguru huyo alipata gadhabu na kuamua kuondoa bendera hiyo.

Kunguru ni ndege Smart, Yani wenye akili sana na wanaoweza kujifunza hata kuongea na kutamka baadhi ya maeneo kama ilivyo kwa kasuku. Kitendo icho cha kunguru kuondoa bendera inayopepea kimetafsiriwa kuwa kunguru kakasirika makazi yao na viota vyao kutunguliwa na makombora. Wakati wengine wakisema kitendi icho ni suala la kiimani.

Hata hivyo bado hakijafahamika kuwa ni lini na eneo gani haswa tukio hilo lilitokea

Tizama video ya kunguru huyo hapo chini.


View: https://www.instagram.com/reel/CyfRvqbKhOK/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==
 
makunguru mengine kama yale ya zanzibar ni majini tu. yana akili kama binadamu. huwa yanatumwa hadi kuiba nyama na samaki kwa watu.
 
Kama wanauwezo wa kumtumia bundi, paka nk kusafirisha madude yanayotengenezwa kwa maandishi ya kiarabu wanashindwa kumtumia kunguru? Hujawahi kuona mtoto mdogo anazaliwa akiwa anajua Aya za kitabu Cha kiarabu unadhani ndani yake Kuna nini?
 
hahaa, kusingekua na vita hili tukio lisingetrend,

ngoja waje wale majamaa wa mwisho wa dunia
 
kuna watu hapa watakuja kusema ni nguvu za alah na kwamba allah anawasapoti kwa wanachokifanya israel. wakati hili ni tukio la kawaida sana.
 
Ndege wanafundishika kama ulikuwa hujui, ndege wanaingiza mpaka madawa ya kulevya magerezani, Si ajabu huyo ndege anafugwa na magaidi katumwa afanye hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…