Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 12,624
- 24,751
Kuhusu Wayahudi kuongeza makazi na ardhi zaidi ya vile ilivyokuwa imeelekeza UN, bila shaka hapo Waarabu Wapalestina na UN yenyewe walaumiwe pia kwa ^kumsaidia^ Myahudi.Chanzo cha kutoweka Amani si ni mayahudi kuchukua Ardhi zaidi ya waliyopewa na UN Sivyo?
Umoja wa Mataifa kimsingi haikuchukua hatua thabiti kumzuia Myahudi asivuke mipaka ya maelekezo ya UN.
Isisahaulike kwamba huu ni wakati ambapo Wayahudi walikuwa wahanga wa mauaji ya halaiki ya Hitler na pia hakuna taifa lililokuwa tayari kuwapokea wakimbizi waliokuwa wamenusurika mauaji hayo ya kutisha. Kimbilio pekee la haraka lilikuwa Palestina.
Kwa upande mwingine, Palestina alikataa uamuzi wa UN wa kuigawa Palestina iwe nchi mbili, akaona suluhu ni ^mtutu wa bunduki^ -- ambao tunaweza kusema pengine hawakuwa nao au waliutunza kwa majirani zao Wayahudi walioibuka washindi kwenye vita na migogoro yote iliyofuata baina yao.
Iwapo Waarabu wa Palestina wangekubali kutambulika kama taifa huru katika maeneo yaliyokuwa yameainishwa na UN, nani ajuaye pengine hii ingewapa ushawishi na nguvu zaidi kwa mataifa mengine katika kudai ardhi ya ziada na kuitawala, na labda vita vingi na umwagaji damu vingeepukwa.
Kwa kiasi fulani Waarabu wa Palestina wameonekana kama nchi na utawala wa kigaidi, wamechukiwa sana na marafiki wa Wayahudi, sababu mojawapo ikiwa ni wao kukosa uhalali wa kuwa nchi huru inayotambulika rasmi na UN.
Tunaweza kusema kwamba Wayahudi walitumia fursa ya udhaifu wa Palestina ili kuendelea kujitanua zaidi.