LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Kuamkia leo tarehe 18/10 Israeli imeshambulia hospitali iyopo Gaza na kuuwa zaidi ya watu 500!! HAKIKA kitendo hiki ni kibaya na kimekiuka haki za binaadamu.

Israeli imevuka mipaka kwa kushambulia raia wasio na hatia
 
Kuamkia leo tarehe 18/10 Israeli imeshambulia hospitali iyopo Gaza na kuuwa zaidi ya watu 500!! HAKIKA kitendo hiki ni kibaya na kimekiuka haki za binaadamu.

Israeli imevuka mipaka kwa kushambulia raia wasio na hatia
Hamas mpk waseme,bado hawajasema
 
Mzee unakwama sana. Palestine ilikuwepo Tangu miaka ya BC. Kama unataka kuijua Palestine vizuri soma kuhusu
Philistia Empire.
Wale watu walikuwepo na hawakuondoka eneo la makazi yao. Wale waliokimbia nchi na kwenda Ulaya kufanya kazi za ndani warudi na kuwalazimisha wenyeji waondoke kwenye makazi yao ya miaka zaidi ya 1000, Hii inaingia akilini kweli?

Ulaya ndio hao waliowachinja wayahudi wapo na wajibu wa kuwatafutia eneo la kukaa huko huko ulaya na waliite Israel. Hakuna mjadala zaidi ya hapo na ndio msimamo wa nchi za kiarabu.

Mengine ni propaganda za kindezi kutafuta kuhalalisha mauaji ya wayahudi yaliyotokea huko ulaya.

Karibia wayahudi milioni 6 waliuawa huko ulaya. SItaki unijibu kwa emotions. Nijibu kwa facts ukieleza kwanini Israel wapo kwenye nchi ambayo siyo yao? Kwanini wasiwaombe wakazi wa pale wakaishi nao na jina la nchi likabaki kuwa Palestine?
 
Unapigana na adui anafahamu una silaha kama F 35 stealth fighters, defense system kama iron dome, vifaru
vyenye latest tech kama Merkava, una satellite, meli za kivita, una back up kutoka nchi yenye nguvu kiuchumi na
kijeshi duniani kama US, una nuclear bombs na kila aina ya uchafu.

Halafu huyo adui anakuja kukabiliana na wewe akiwa na pikipiki, Toyota hilux na paragliders wakiwa na rockets zilizotengenezwa kienyeji, AK 47, RPG, grenade na pistol. Ni ngumu kupambana na mtu ana roho ngumu kiasi hiko, adui wa namna hio tayari kajitoa sadaka, hio vita ni ngumu.

Israel iwasikilize hao waarabu wanahitaji nini potelea pote wamalize mzozo na wafikie muafaka, wanaolipia gharama ya vita ni raia wasio na hatia.


Yatakua yale yale ya US kule Afghanstan kukaa zaidi ya miaka 20 na kutumia zaidi ya $2 Trillion na baadae kuachia nchi Taliban, ni kutwanga maji kwenye kinu.

it is much better to lose a battle and win the war.

Kuna filamu inaitwa The Battle at Lake Changjin, inazungumzia Korean war, China ilipeleka askari kuisaidia Korea(North Korea-allied Chinese People's Volunteer Army), wakati askari wa US wakiwa wame retreat wanarudi wanaona askari wa China ameshikilia silaha akiwa amefariki ame freeze kwenye barafu kama yupo hai, General Oliver P Smith alipiga salute akasikika akisema "fighting against such strong-willed men, the U.S. was not ordained to win."
 
Mkuu ila HAMAS na wapalestina kwa ujumla wanahitaji moja tu:





Kulikoni kupora na kuyakalia meneo ya watu?
 
* Jana imetokea sintofahamu. Hospitali ya Kikristo huko Gaza ililipuliwa na watu zaidi ya 800 kupoteza maisha wakiwemo wanawake na watoto. Hamas wamesema Israel waliilipua, Israel wakasema hawahusiki na wamtoa video ikionyesha rocket ya Hamas ikikosa muelekeo na kwenda kulipua hospitali hiyo. Nao Islamic Jihad wamekanusha kuhusika na shambulio hilo.

* Rais wa Marekani, Joe Biden awasili Israel.

* Putin awaomba Israel waachie picha ya satalaiti kuionyesha dunia kwamba kweli hawahusiki na shambulio hilo.

* Israel yanasa sauti ya mawasiliano ya Hamas kuhusika na shambulio la hospitali.

* Marekani yaruhusu wafanyakazi wasio wa kidemokrasia kuondoka Lebanon

* Jeshi la Israel lawataka wakazi wa Kusini mwa Gaza kuhamia Kaskazini.

* Hamas wasema hawana bomu kubwa namna hiyo kulipua hospitali.

* Hamas wasema wapo tayari kuwaachia mateka wote endapo Israel atasitisha kuipiga Gaza. Kumbuka wanaendelea kuipiga ili mateka wao waachiwe.

* Hezbollah wanasema wamekishambulia kifaru cha israel mpakani mwa Lebanon.

* Mfalme wa Jordan, Abdullah II amesema hatoruhusu Wapalestina kuingia nchini mwake. Hiyo ni baada ya Misri kuwakataa pia.

* Balozi wa palestina nchini Japan anasema hospitali hiyo ilipokea onyo kutoka Israel kabla ya shambulio.

KWA TANZANIA: Idadi ya makanisa na misikiti ni mingi kuliko viwanda. Wakristo wakijikita Waisraeli, waislamu wakijikuta Wapalestina. Dini zimeshika hatamu nchini kuliko maendeleo. Mtu anajua biblia na quran kuliko katiba.

Hivyo ni vyanzo vyangu vya taarifa... unaweza kuleta taarifa ya vyanzo vyako pia.
 
Japo issue ilikuwa rahisi: "kwenda haki bin haki."
Ndio maana nilisema mfano US ilikaa Afghan na kutumia zaidi ya dola trilioni 2, lakini wakaja kuacha ardhi kwa Taliban, ifikie muda Israel ijitathmini.
 
Hamas wapigwe kama alivopigwa JAPAN, mpk waache kushobokea vita.
Japan na yeye alihisi anamuweza USA hadi alipopewa dawa ambazo hakuzijua, zilikuw ni siri ya USA na surprise kwa JAPAN. U turn Hamas inabidi ipigwe surprise mpk waichukie vita na wawe wapole milele
 

Israel kwenyewe waislamu ni wengi kuliko wakristo:

approximately 73.8 percent of the population is Jewish, 18 percent Muslim, 1.9 percent Christian, and 1.6 percent Druze.

Wapi huko wakristo au ni waislam zaidi wanakotaka kupigana?
 

Misri haiko tayari kukubali idadi kubwa ya Wapalestina​


EPACopyright: EPA
Rais wa Misri Al Sisi katika mkutano wake na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Cairo todayImage caption: Rais wa Misri Al Sisi katika mkutano wake na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Cairo today
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza anatarajiwa kuzuru Misri hivi karibuni.
Wakati wa mzozo huu kumekuwa na mawazo yanayozunguka kwamba Israel inataka kuwahamisha wakaazi wa Gaza wa milioni 2.3 hadi jangwa la Sinai nchini Misri.
Walihutubiwa katika mkutano wa waandishi wa habari na rais wa Misri hapo awali.
"Kinachotokea sasa huko Gaza ni jaribio la kuwalazimisha wakaazi wa kukimbilia na kuhamia Misri, jambo ambalo halipaswi kukubaliwa," Abdul Fattah al-Sisi alisema.
Alionya kwamba kama haya yangetokea, watu wa Misri wanaweza "kutoka nje na kuandamana kwa mamilioni ".
Cairo tayari imeonya kwamba ikiwa Wapalestina wataondoka katika ardhi yao, inaweza "kuondoa" matumaini ya Wapalestina ya kuwa taifa.
Lakini pia itakuwa hatari sana kwa serikali ya Misri kama ingeonekana kuhusika katika mpango wowote kama huo - na kuwasha hasira ya umma katika ulimwengu wa Kiarabu.
Mmiminiko wowote wa watu pia ungezidisha mzozo wa sasa wa kiuchumi wa Misri na kuibua hofu ya usalama katika eneo lake lenye utulivu la Sinai.
Sisi alipendekeza kwamba kwa vile Gaza iko chini ya udhibiti wa Israel, Wapalestina wanaweza badala yake kuhamishiwa kwenye jangwa la Negev la Israel wakati wa mashambulizi yake dhidi ya Hamas "hadi wanamgambo hao watakaposhughulikiwa".
Mamia ya malori ya msaada yameegeshwa kaskazini mwa Sinai, yakingoja makubaliano ya kuruhusu kutumwa kupitia kivuko cha Rafah ya Misri kuingia Gaza.
Ni kivuko pekee cha eneo la Palestina ambacho hakidhibitiwi na Israel, lakini kibali cha Israel kitahitajika ili kuruhusu kufunguliwa.
Katika siku za hivi karibuni, kivuko hicho kimeshambuliwa mara nne na mashambulizi ya anga ya Israel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…