LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Walienda kuzuia na kuharibu mitambo ya kutengeneza na kurushia maroketi sasa kama walifanikiwa katika hilo hayo maroket yanayo rushwa sasa yanatoka wapi?
 
Hii mbona ipo biblically mkuu ni kwa vile tu haujui na kwa taarifa yako tu Kuna wapelistina wengi wakristo kuliko wayahudi
Waisrael walisema damu ya Yesu iwenu juu yetu na vizazi vyetu vyote.
Walitesekana sana baada ya Yesu kwenda mbinguni mpk leo.
 
Kivumbi leoooo, namna gani pale mashushu wanaosifiwa kutwa washindwe kugundua hapa viongozi wa Israel wanatakiwa waanze kujichunguza wenyewe kwanza kuna tatizo pahala .
 
Wameanzisha ngoja tuone kama hawawezi. Israel kuanzisha ground operation ni kupunguza collateral damage inayotokana na airstrikes.

Hezbollah ilidai wakiingia Gaza inashambulia, Iran ilidai wakishambulia Hezbollah nayo inawasaidia.
Amini ninachokwambia, Israel labda iamue sasa kuwa kama ile ya miaka ya nyuma. Hii ya sasa inashinikizwa kuachia mamia ya Wafungwa ili ipewe maiti mbili ya askari waliouawa na inatii? Sasa hapo unapoona kuna taifa kweli?
Na hivi wamekamatwa askari wao na raia walio hai, hapo wataambiwa ili wenzao hao waachiwe inabidi Israel ifungashe na iomdoke mashariki ya kati na wao watakubali kwamba bora waondoke kuliko mateka wa Kiisraeli kuuawa.
Wamekuwa Mafala sana hao watu siku hizi.

Walibweteka mpaka wakaanza kusherehekea ushenzi kwa kuruhusu na kukubali Tel Aviv uwe mji mkuuu wa Mashoga duniani. Hayo ni matokeo ya watu waliojisahau.

Ngoja warudiwe na akili.
 
Hesbullah nao wanaonya, Israel ikipeleka ground forces Palestina nao wanaingia mzigoni.

Hii kitu inahitaji hekima sana, IDF na Mossad wakubali wamezidiwa wajipange upya. Tukuo kubwa kama hilo nchi nzima haina hata informer ni aibu.
Mkuu ni shambulio la kushitukiza.
Maana hata sisi wenywe Tz hapa tulipata aibu kule mtwara magaidi waliingia na walisumbua kama wiki hivi.
Kuvamia mok vitu vya police.
Kumbuka mpka APC ya jeshi ilipigwa na wanajeshi baadhi walipotea kule mtwara.
Mpk raia kule kitaya walitekwa na wengine kukatwa vichwa.

Watu waligeuka kuwawakimbizi kiule umesahau.

Nafikili ni shambulio la kishitukiza ni kawaida kwa uvamivi.
 
According to Aljazeera atleast 189 people has been killed in Gaza by Israel air attack after Hamas offensive in Israel.
 
Hahahahahaha wabongo bhanaa, yaaani weweee ndo unaionya Israel kuhusu Mambo ya usalama!!!??.... Humu jamii forum kuna vituko saaaana aiseee
 
Hahahahahaha wabongo bhanaa, yaaani weweee ndo unaionya Israel kuhusu Mambo ya usalama!!!??.... Humu jamii forum kuna vituko saaaana aiseee
Sawa, kwani kilichotokea ni kipi?
Mimi sijidharau ninapotakiwa ku air out my views.
Halafu uwe na akili japo kidogo basi. Kwani inakatazwa ku join social media kuchangia? Au kwa akili zako unadhani social media labda ni cabinet au makao makuu ya wizara ya Ulinzi?
 
Ni Six Days war pekee ambapo Israel ilianza kwa nguvu. Vita nyingine huwa wanaanza kama hawataki baadae vipande vya miguu na mikono vikianza kupaa angani tutaita umoja wa mataifa kulalamika na kuomba mazungumzo.

Sijaona yeyote anaita UN mwanzoni mwa shambulizi la Hamas. Sitarajii IDF ikiingia Gaza waitwe UN. Upande mwingine kule Lebanon, UN imevitaka vikosi vyake virudi kambini kwa sasa vuguvugu la Hezbollah lipo.
Hezbollah wameonekana na pikipiki wanakimbilia mpakani kujiandaa. Israel itawajibu soon. Reserves wameitwa na battalions zipo njiani nyingine.

Hao wafungwa wa Palestina wataachwa wote, sio kipaumbele cha Israel kuishi nao. Wote huwa wanateka maasimu wao kwa matumizi ya exchange. Hilo suala la Israel kuondoka pale ilipo lifute kichwani, ikibidi mazao ya jangwa la Negev yatatumika.
 
Makombora ya kwenye makaratasi muda sio mrefu watapiga yowe
 
Sisi inavumilika kidogo ila Israel tangu imekuwepo likelihood ya kitu kama hicho huwa ipo siku yoyote, hamas au hesbullah wanaweza kutia timu. Ndio maana wakatengeneza hadi zile Iron dome, Mifumo ya kupashana habari pia.

Naona jamaa ndani ya muda mfupi wamechukua eneo kubwa zaidi ya Gaza yenyewe. Ila nimesoma Cammander mmoja wa IDF anasema wameibuka wakiwa wengi kuliko kawaida.
 
Walienda kuzuia na kuharibu mitambo ya kutengeneza na kurushia maroketi sasa kama walifanikiwa katika hilo hayo maroket yanayo rushwa sasa yanatoka wapi?
Unamaanisha utengenezaji wa maroketi duniani uliisha mwaka 2014?
Kwamba baada ya kuharibiwa kwa maroketi ya 2014, haiwezekani yakaundwa mengine kuanzia mwaka huo na sasa miaka tisa baadae yawepo. Maroketi ni viumbe hai kwamba Juma Nkamia alifariki hivyo haundwi mwingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…