Mara nyengine katika vita kuna vichekesho sana.Nimewahi kuona bondia kapigwa kaanguka chini kizunguzungu tele halafu anafanya kama anainuka akapigane tena.Muamuzi wa pambano ndiye anayejua huyu mteja wangu akubali tu.
Wanasiasa nao wa mataifa makubwa na madogo wanapopata upinzani au kushambuliwa hujaribu kuwapaka matope wapinzani wao mbele ya macho ya wananchi.
Katika mashambuzi ya juzi Jumamosi yaliyofanywa na Hamas na wenzao wa Palestina kuna watu wanasema
mashambulio yale ni ya woga. Eti wanasema mashambulio hayo yamefanyika rena bila wapalestina kuchokozwa.
Sijui woga huo uko wapi kwa kikundi kidogo cha wapiganaji kwanza kubomoa kituo kizima cha mpaka wa Erez halafu kusonga mbele kwa piki piki tu ndani ya nchi inayosifika kwa walinzi wakali.
Woga huo sijui ukoje kwa kikundi kidogo kuteka kambi nzima ya jeshi la Israel na kuua askari halafu kuteka vifaru na magari ya deraya
Woga huo umekaaje kwa wapiganaji wachache kubeba askari na raia kama mateka kurudi nao Gaza
Kama ni shambulia na mtu muoga mbona
America anapeleka meli za kivita kadhaa mpakani na Israel ili kuilinda nchi hiyo kutokana na hofu ya wapiganaji hao wachache