Mkuu andiko lako zuri ila ni kama umechanganya mambo! Hivi Kuna tofauti gani kati ya Wayahudi na Waisrael? Ebu cheki hapa ulichoandika; " 3.Hao Waisrael na Wayahudi ni wabaguzi,wa hali ya juu......................",. "Kimsingi,yeyote mbatizwa ni Taifa la Mungu yaani Israel"
Kama huelewi wapo wa isiraeli ambao sio wayahudi
Kwa ufafanusi wayahudi ni ukoo wa yuda mwana wa isiraeli Kati ya watoto kumi na mbili wa yakobo ambaye ndiye isiraeli hivyo watoto wengine kumi na moja pia ni Wana wa isiraeli
Poa Kwa nyongeza kuna tofauti Kati ya waebrania na wa Ibrahim
Kumbe Ibrahim alikua muebrania akazaa watoto wakawa Wana wa Ibrahim
ishimael mtoto wa hagiri mmisli
isaka mtoto wa sala muebrania
Pia Akawazaa watoto Kwa ketura suria wake Ibrahim zimrani na yokshani na medani na midiani na ishabaki na shua
Wana wote wa Ibrahim walikua wanane
hai
Hayo walikua Wana wa Ibrahim I na pia walikua waebrania Kwa kua Baba Yao ni muebrania
Vivyo hivyo Kwa Wana wa Israel walikua kumi na wawili mtoto wa mke mkubwa wa yakobo Leya alizaa mtoto wake wa nne aliye muita yuda ambaye huyo kwake aliandaliwa kuzaa wafalme watakao watawala Wana wote wa isiraeli
Kwa huyo yuda walitoka kabila la wayahudi ambao Leo wote wanaitwa wayahudi Kwa kua myahudi ndiyo alikua mtawala wao
Kwa hiyo wote Kwa ujumla wao ni waebrania Wana wa Ibrahim
Kati Yao kuna wa Ismael(nebayoth/kedari/abdeel/mbisam NK)
Kuna wa isihaka(waedom na waisrael)
Kuna wa zimrani Kwa ketura na ndugu zake
Hivyo ipo tofauti ya waisrael wayahudi na Jamaal zao Kwa kuwaunganisha wote waite waebrania hapo hayupo atakaye kataa