Akizungumza kwenye kanali ya 13 ya utawala ghasibu wa Israel, Amir Avivi, Brigedia Jenerali wa Akiba wa Jeshi, ametoa wito wa kuelewa ukweli kwamba makombora yenye shabaha ya Hezbollah ni 'tishio kubwa sana la kistaratajia.'
Akielezea sababu ya onyo hilo, amesema: Tunaweza kukatiza njia ya roketi iliyorushwa, na hili ni rahisi kwetu, lakini suala la kombora ni tofauti kabisa, hivyo si rahisi kwa makombora yetu kuyazuia."
Hizbullah haijawahi kutoa maelezo ya kina kuhusu uwezo wake wa kijeshi, lakini kwa miaka mingi, Wazayuni wamekuwa wakichunguza na kutathmini uwezo wa kijeshi wa Hizbullah kuliko inavyofanya Hizbullah yenyewe.
Baada ya kulishinda mara mbili jeshi la Kizayuni mwaka 2000 na 2006, Hizbullah ya Lebanon imejiimarisha kijeshi katika masuala ya vikosi vya ardhini na kuboresha mifumo yake ya makombora hususan kwa kutengeneza makombora ya kulenga shabaha bila kukosea.
[https://media]Kombora la Hizbullah
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, Hizbullah ina zaidi ya makombora 200,000, na zaidi ya nusu yake ni makombora yanayolenga shabaha bila kukosea ambayo ukingo wa makosa yake hauzidi mita chache. Hezbollah ina makombora ya Katyusha na Grad yenye uwezo wa kulega kilomita 40, makombora ya Fajr 3 yanayolenga zaidi ya kilomita 45 na Fajr 5 yenye yanayofika umbali wa zaidi ya kilomita 75. Kundi hilo pia lina makombora ya Raad 2 na Raad 3 yanayofika umbali wa kilomita 70, Khybar 1 yenye umbali wa zaidi ya kilomita 100, Zelzal 1 na 2 yanayolenga shabaha iliyo umbali wa takriban kilomita 160 na 210, Fateh 110 ambalo ni kombora la balestiki, lenye uwezo wa kulega shabaha iliyo umbali wa kilomita 300 na uwezo wa kubeba kichwa cha vita chenye uzito wa kilo 500.
Lakini makombora ambayo yanawatia wasiwasi Wazayuni zaidi ni kombora jipya aina ya Scud, ambalo linalenga umbali wa zaidi kilomita 700 na uwezo wa kulega maeneo yote muhimu na nyeti ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Aidha, Hezbollah ina mifumo kadhaa ya kukinga makombora ya vifaru ambayo inaweza kulemaza operesheni za kikosi kizima cha jeshi la Israel.
Hezbollah pia ina makombora ya nchi kavu kuelekea baharini ambayo ni ya umbali tofauti na ambayo yanaweza kulenga na kutokomeza meli na boti za kijeshi za Israeli. Kama ilivyotokea katika vita vya Julai 2006 ambapo manowari ya Sa'ar 5 ya utawala wa Kizayuni ililengwa na kuharibiwa mbele ya pwani ya mji wa Sur. Kwa mujibu wa vyanzo vya Israel na Marekani, hivi sasa Hezbollah ina mifumo ya makombora ya kuharibu meli za aina mbalimbali, kama vile kombora la Noor lenye umbali wa kilomita 200, kombora la Qadir lenye umbali wa zaidi ya kilomita 300, na la Russia Yakhont, ambalo linafikia umbali wa zaidi ya kilomita 300 na ambalo linachukuliwa kuwa moja ya makombora ya kisasa kabisa duniani ya kutokomeza meli.
Licha ya hayo, Hezbollah pia ina makombora mengine yenye shabaha ya kulenga umbali wa kilomita 1000 ambayo yanaweza kurushwa kutoka majukwaa thabiti na yanayotembea na ambayo yanahesabiwa kuwa tishio kubwa la baadaye dhidi ya meli za kivita za utawala ghasibu wa Kizayuni. Zana za kisasa za ulinzi wa anga za Hezbollah ni sehemu nyingine ya uwezo wa kijeshi wa harakati hiyo ya mapambano.
Kwa mujibu wa vyanzo vya Israel, Hezbollah ina makombora ya nchi kavu kwenda angani ambayo yanaweza kulenga shabaha kutoka umbali wa kilomita 5 na kwa masafa ya juu ya kilomita 3.5.
[https://media]Wanajeshi wa Hizbullah
Hezbollah pia ina zaidi ya drone 2,000 za aina mbalimbali, nyingi zikiwa za kushambulia. Ndege hizo zisizo na rubani huko nyuma ziliundwa kwa ajili ya utafiti wa angani, lakini leo, kwa kuboreshwa teknolojia ya akili bandia, zimeimarishwa na kutumika kulenga shabaha sahihi na kufanya uharibifu mkubwa katika medani ya adui. Kwa mfano, ndege hizo zisizo na rubani zinaweza kulenga shabaha nyeti kama vile rada zilizounganishwa kwenye mifumo ya ulinzi na kuziharibu.
Kwa upande wa usahihi, kasi, muda wa kuruka, umbali na uzito wa vilipuzi vinavyoweza kubebwa, ndege za Hezbollah zinaendelea kuboreshwa katika mifumo ya rada na mbinu za akili mnemba na zinatumiwa katika vita vya kielektroniki.
Aidha, Hizbullah ina kikosi chenye nguvu cha nchi kavu, hususan kikosi maalumu cha Rizvan, ambacho wataalamu wa kijeshi wa Kizayuni wanakitaja kuwa mojawapo ya vitengo vyenye uwezo mkubwa zaidi duniani. Uwezo huo wa kipekee wa Hizbullah unatathminiwa katika hali ambayo, kwa mujibu wa Seyyed Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon, iwapo vita vitatokea kundi hilo linaweza kuirejesha Israel katika Zama za Mawe.