LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Majibu ya Israel huwa ni ya kikatili mark my words huu ndo mwisho wa hamas na mwanzo wa maisha mabaya sana kwa wapalestina
Hamna, haitakuwa mwisho wa HAMAS, na kama HAMAS ikafa basi yataibuka makundi mengine.

Kwa mujibu wa maandiko, Israel waliambiwa wawaangamize wakaani wote ila hawakufanya hivyo, kwahiyo Mungu akawaambia hao watakuwa kama miiba mbavuni mwenu ktk maisha yenu yote.
 
Akizungumza kwenye kanali ya 13 ya utawala ghasibu wa Israel, Amir Avivi, Brigedia Jenerali wa Akiba wa Jeshi, ametoa wito wa kuelewa ukweli kwamba makombora yenye shabaha ya Hezbollah ni 'tishio kubwa sana la kistaratajia.'

Akielezea sababu ya onyo hilo, amesema: Tunaweza kukatiza njia ya roketi iliyorushwa, na hili ni rahisi kwetu, lakini suala la kombora ni tofauti kabisa, hivyo si rahisi kwa makombora yetu kuyazuia."

Hizbullah haijawahi kutoa maelezo ya kina kuhusu uwezo wake wa kijeshi, lakini kwa miaka mingi, Wazayuni wamekuwa wakichunguza na kutathmini uwezo wa kijeshi wa Hizbullah kuliko inavyofanya Hizbullah yenyewe.

Baada ya kulishinda mara mbili jeshi la Kizayuni mwaka 2000 na 2006, Hizbullah ya Lebanon imejiimarisha kijeshi katika masuala ya vikosi vya ardhini na kuboresha mifumo yake ya makombora hususan kwa kutengeneza makombora ya kulenga shabaha bila kukosea.

[https://media]Kombora la Hizbullah

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, Hizbullah ina zaidi ya makombora 200,000, na zaidi ya nusu yake ni makombora yanayolenga shabaha bila kukosea ambayo ukingo wa makosa yake hauzidi mita chache. Hezbollah ina makombora ya Katyusha na Grad yenye uwezo wa kulega kilomita 40, makombora ya Fajr 3 yanayolenga zaidi ya kilomita 45 na Fajr 5 yenye yanayofika umbali wa zaidi ya kilomita 75. Kundi hilo pia lina makombora ya Raad 2 na Raad 3 yanayofika umbali wa kilomita 70, Khybar 1 yenye umbali wa zaidi ya kilomita 100, Zelzal 1 na 2 yanayolenga shabaha iliyo umbali wa takriban kilomita 160 na 210, Fateh 110 ambalo ni kombora la balestiki, lenye uwezo wa kulega shabaha iliyo umbali wa kilomita 300 na uwezo wa kubeba kichwa cha vita chenye uzito wa kilo 500.

Lakini makombora ambayo yanawatia wasiwasi Wazayuni zaidi ni kombora jipya aina ya Scud, ambalo linalenga umbali wa zaidi kilomita 700 na uwezo wa kulega maeneo yote muhimu na nyeti ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Aidha, Hezbollah ina mifumo kadhaa ya kukinga makombora ya vifaru ambayo inaweza kulemaza operesheni za kikosi kizima cha jeshi la Israel.

Hezbollah pia ina makombora ya nchi kavu kuelekea baharini ambayo ni ya umbali tofauti na ambayo yanaweza kulenga na kutokomeza meli na boti za kijeshi za Israeli. Kama ilivyotokea katika vita vya Julai 2006 ambapo manowari ya Sa'ar 5 ya utawala wa Kizayuni ililengwa na kuharibiwa mbele ya pwani ya mji wa Sur. Kwa mujibu wa vyanzo vya Israel na Marekani, hivi sasa Hezbollah ina mifumo ya makombora ya kuharibu meli za aina mbalimbali, kama vile kombora la Noor lenye umbali wa kilomita 200, kombora la Qadir lenye umbali wa zaidi ya kilomita 300, na la Russia Yakhont, ambalo linafikia umbali wa zaidi ya kilomita 300 na ambalo linachukuliwa kuwa moja ya makombora ya kisasa kabisa duniani ya kutokomeza meli.

Licha ya hayo, Hezbollah pia ina makombora mengine yenye shabaha ya kulenga umbali wa kilomita 1000 ambayo yanaweza kurushwa kutoka majukwaa thabiti na yanayotembea na ambayo yanahesabiwa kuwa tishio kubwa la baadaye dhidi ya meli za kivita za utawala ghasibu wa Kizayuni. Zana za kisasa za ulinzi wa anga za Hezbollah ni sehemu nyingine ya uwezo wa kijeshi wa harakati hiyo ya mapambano.

Kwa mujibu wa vyanzo vya Israel, Hezbollah ina makombora ya nchi kavu kwenda angani ambayo yanaweza kulenga shabaha kutoka umbali wa kilomita 5 na kwa masafa ya juu ya kilomita 3.5.

[https://media]Wanajeshi wa Hizbullah

Hezbollah pia ina zaidi ya drone 2,000 za aina mbalimbali, nyingi zikiwa za kushambulia. Ndege hizo zisizo na rubani huko nyuma ziliundwa kwa ajili ya utafiti wa angani, lakini leo, kwa kuboreshwa teknolojia ya akili bandia, zimeimarishwa na kutumika kulenga shabaha sahihi na kufanya uharibifu mkubwa katika medani ya adui. Kwa mfano, ndege hizo zisizo na rubani zinaweza kulenga shabaha nyeti kama vile rada zilizounganishwa kwenye mifumo ya ulinzi na kuziharibu.

Kwa upande wa usahihi, kasi, muda wa kuruka, umbali na uzito wa vilipuzi vinavyoweza kubebwa, ndege za Hezbollah zinaendelea kuboreshwa katika mifumo ya rada na mbinu za akili mnemba na zinatumiwa katika vita vya kielektroniki.

Aidha, Hizbullah ina kikosi chenye nguvu cha nchi kavu, hususan kikosi maalumu cha Rizvan, ambacho wataalamu wa kijeshi wa Kizayuni wanakitaja kuwa mojawapo ya vitengo vyenye uwezo mkubwa zaidi duniani. Uwezo huo wa kipekee wa Hizbullah unatathminiwa katika hali ambayo, kwa mujibu wa Seyyed Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon, iwapo vita vitatokea kundi hilo linaweza kuirejesha Israel katika Zama za Mawe.

4c3q8aee10ed9f2dhti_800C450.jpg
 
[https://abs-0][https://abs-0][https://abs-0] Kiongozi wa Hamas Al-Arouri katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Jazeera: [https://abs-0] Tuna idadi kubwa ya mateka wa Israel, wakiwemo maafisa wa ngazi za juu; [https://abs-0]Tulikuwa na habari kuwa Israel ilikuwa inapanga operesheni ya kijeshi dhidi ya Ghegda na Ukanda wa Gaza baada ya likizo ya Kiyahudi; [https://abs-0]Bado hatutoi maelezo kuhusu wafu na wafungwa wa Israel tulio nao; [https://abs-0] Kampeni ndiyo kwanza inaanza na inaendelea kulingana na mpango.
 
Mungu hafurahii kifo cha wenye dhambi, hata hao magaidi. ila nijuavyo, usiku wa leo yanaweza kutokea makubwa sana. unajua hizi vita mara nyingi huwa zinapiganwa usiku, mchana wanaogopa kamera.
 
Hamna, haitakuwa mwisho wa HAMAS, na kama HAMAS ikafa basi yataibuka makundi mengine.

Kwa mujibu wa maandiko, Israel waliambiwa wawaangamize wakaani wote ila hawakufanya hivyo, kwahiyo Mungu akawaambia hao watakuwa kama miiba mbavuni mwenu ktk maisha yenu yote.
Mandiko gani wewe hio Bibilia yenu Ilitengenezwa wakati hakuna Taifaa la Israel.

Hebu fatilia Israel ilikuwa lini taifa?

Hao walisha laniwa na Mungu wa shukuru Muingereza ndio aliwapa nchi
 
View attachment 2774569

Umeona hio ramani ilivyo Iran mpk Israel pana mwendo sana.

Na mimi nina uhakika Jordan ilni nchi ya amani tuu sidhani kama mfalme wa Jordan atakubali kukalibisha majeshi ya iran na wengine waweke kambi pale.
Ili kupigana maana vita vikichachamaa vinaweza India Jordan pale .

Iran na Saudi Arabia ni paka na panya , Saudi hawezi mkaribisha Iran pale kwake.

Labda Iran aende Syria. But kumbuka Israel wanashikiria milima ya Syria mpk leo waliteka kipindi cha 6 days war mpk leo bado wameshikiria maeneo hayo.

Shida ya waarabu hawana ushirikiano afu kingine waoga hasa majirani wa Israel maana vita vinaweza expand Israel ni nchi ndogo sana.

Afu kingine waarabu siraha hawatengeneza wao wanunua nje. Wanaotengeneza ni Iran tuu. Ambaye hapatani na wengine.

Saudi Arabia silaha anunua USA asilimia kubwa ya silaha. UAE naye ananunua USA. Qatar ananunua USA.
Mwaka 1972 Mfalme wa Jordan alisafiri kwa helicopter kwenda mpakani Israel kukutana na Golda kukwambia Hafez na Anwar Sadat walivyopanga vita. Ila Waarabu wanaijua Jordan vizuri, walikuwa wanamshawishi ajiunge nao wakahisi hajakubali hivyo hawakupanga nae siku rasmi ya kushambulia hivyo hakuwa anajua.

Kwenye Six Days war napo ndege za Israel zilikuwa detected na Jordan zikielekea Egypt, Jordan ukapiga simu HQ za jeshi Egypt kumbe siku hiyo Waziri yuko kwenye mambo yake binafsi na naibu wake katoa marufuku asiamshwe usiku ule. Simu ilikuwa ya high level individual pekee ndio apokee, hawakupokea.

Jordan hawataki shida kwanza wanajua Waarabu walivyo wanafiki, unamkaba mmojammoja unasaini mkataba na mwenye nguvu kati yao kivyake, wengine wanaachwa unakuja kuwabamiza. Wanaanza wakiwa wote, moto ukiwaka kila mtu anatafuta kupona
 
Hii operation Israel hawaiwezi!
Wameanzisha ngoja tuone kama hawawezi. Israel kuanzisha ground operation ni kupunguza collateral damage inayotokana na airstrikes.

Hezbollah ilidai wakiingia Gaza inashambulia, Iran ilidai wakishambulia Hezbollah nayo inawasaidia.
 
Hivi wao si ndo walimuua Qaseem? Acha na wao waonje kudadeki zao. Sawa,ulinzi wanao,lakini hata hayo machache yaliyoweza kuleta maafa,ni ishara kwamba huwezi kujilinda 100%. Basi tu,sema raia wasio na hatia ndo wanafikwa na mauti kwa usenge wa viongozi wa ngazi za juu,wao na familia zao wanajamba huko makwao
 
BREAKING:

Unconfirmed reports of Hezbollah threatening to invade Israel from Lebanon if Israel launches a ground offensive against Gaza

The Egyptian gov. has allegedly passed on the information from Hezbollah to Israel.

It's worth remembering that Hezbollah is an Iranian tool
 
BREAKING:

Unconfirmed reports of Hezbollah threatening to invade Israel from Lebanon if Israel launches a ground offensive against Gaza

The Egyptian gov. has allegedly passed on the information from Hezbollah to Israel.

It's worth remembering that Hezbollah is an Iranian tool
 
View attachment 2774569

Umeona hio ramani ilivyo Iran mpk Israel pana mwendo sana.

Na mimi nina uhakika Jordan ilni nchi ya amani tuu sidhani kama mfalme wa Jordan atakubali kukalibisha majeshi ya iran na wengine waweke kambi pale.
Ili kupigana maana vita vikichachamaa vinaweza India Jordan pale .

Iran na Saudi Arabia ni paka na panya , Saudi hawezi mkaribisha Iran pale kwake.

Labda Iran aende Syria. But kumbuka Israel wanashikiria milima ya Syria mpk leo waliteka kipindi cha 6 days war mpk leo bado wameshikiria maeneo hayo.

Shida ya waarabu hawana ushirikiano afu kingine waoga hasa majirani wa Israel maana vita vinaweza expand Israel ni nchi ndogo sana.

Afu kingine waarabu siraha hawatengeneza wao wanunua nje. Wanaotengeneza ni Iran tuu. Ambaye hapatani na wengine.

Saudi Arabia silaha anunua USA asilimia kubwa ya silaha. UAE naye ananunua USA. Qatar ananunua USA.
Unachosahau Jordan kuna washia wengi na wengi wao wapo Hizbullah! Ukiigusa Iran middle east yote itachafuka hiyo!

Na ukiigusa Saudia middle east yote inachafuka hiyo!
 
Back
Top Bottom