LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Huko sidhani kama watu wanakimbilia ajira za jeshi,maana kila mara wako standby,hakuna lelemama.Kwakweli ni kushukuru kama upo kwenye nchi kama hii.
wayahudi woote duniani huwa lazima waende walau miezi 6 kutumikia jeshi israel. marekani kuna wayahudi karibia 10m, ulaya ni wengi pia, australia na kwengine. wote hao ni wanajeshi, na ikitokea vita namna hii wanaweza kuitwa kurudi kupigania nchi yao.
 
Maandamano ya kusaidia upinzani na watu wa Palestina huko Tunis, mji mkuu

View: https://youtu.be/m2xCOG0gtHE
Leo jioni Jumamosi, idadi ya wanaharakati wa Kitunisia walifanya mkusanyiko kuunga mkono upinzani wa Palestina na watu wa Palestina, mbele ya ukumbi wa mji wa Tunis.
 
Hilo gorofa lililobomoshwa nitashangaa kama viongozi wa hamas watakuwa wamo humo. Ukiisha ichokoza hivyo israel ni either utafute handaki au ukimbie nchi.
 
Kwa hiyo ww makosa yakitokea upande wa unao wapenda ndo hoja ya wao ni binadamu sio mungu ina kuwa na maana, lakini ikitokea upande usio upenda sasa hapo hoja binadamu hajakamilka hivyo ana fanya makosa haina mashiko sio?

Ww si ndo unashinda humu unaziponda integensia za Urusi pale inapo tokea tukio lolote la kiusalama ndani ya nchi hiyo? Au kwenye integensia za Urusi malaika ndo wanao fanya kazi na sio binadamu hivyo hawasitahili kufanya makosa?
Urusi ina zaidi ya mwaka vitani na mafanikio yake na makosa yake hayahitaji nguvu nyingi kuyaona, Israel ina shambulizi halijatimiza hata 24hrs tiyari unailinganisha na Urusi.

KGB ilikuwepo wakati USSR inagawana mbao, Mossad imeipambania Israel ambayo imevamiwa mara nyingi na maadui superior lakini haipotezwi.
Tatizo lako mkuu huwa unaongea kumaliza na ndio maana mwisho huwa unajikuta umeumbuka.

Kila siku ulikuwa unaimwagia sifa mosad lakini leo hii hiyo mosad kwa miaka mingi imeshindwa kudhibiti kabisa silaha zi siifikie Hamas licha ya kuizingira gaza kila upande tena eneo lenyewe ni dogo mno.
Kwa udogo wa eneo la Israel kufanyiwa ambush kama ya leo ni dhihirisho tosha ya kuwa hiyo mosad huwa mnaikuza tu lakini ni ya kawaida sana.
Tulete list ya missions za Mossad vs za FSB hapa tuone nani ana successful missions nyingi?
Tabia yako ya kutokuwa na akiba ya maneno imekufanya mpaka sasa umeukimbia uzi wa vita ya Ukraine.
Si lazima niwepo kwenye ule uzi, sikuanzisha mimi. Nisipokuwepo unapungukiwa nini, zaidi ya mwaka vita inaendelea na sina muda wa kuzungumza jambo lilelile muda wote. Hii ya Israel hata miezi haitopita itakuwa imeisha na mambo mengine yaendelee.
Ulikuwa unashinda kwenye uzi kazi yako ni kuzisifia silaha za kimagharibi kuwa ni bora na za Urusi ni dhaifu ,leo hii Ukraine unafanya Offenseve kwa kutumia maelfu ya hizo silaha za kimagharibi lakini mpaka sasa zimeshindwa kuisaidia Ukraine kuteka hata wilaya moja kwa zaidi ya miezi 5.
Tuseme silaha za Magharibi sio bora, Israel wamezitumia miaka yote kupigana na maasimu wao na matokeo unayajua. Una silaha bora, ni jeshi la pili duniani ila unapigana na nchi dhaifu haipo hata kwenye majeshi 20 bora duniani unakaa mwaka mzima na silaha zako bora hata air dominance tu huna.
Ukibanwa unaleta visingizio Marekani inaisaidia Ukraine, wakati huo unadai silaha za Marekani ni dhaifu. Hutosikia Israel inalialia Hamas na Hezbollah kutumia silaha za kupewa na Iran.
 
Maandamano ya kusaidia upinzani na watu wa Palestina huko Tunis, mji mkuu

View: https://youtu.be/m2xCOG0gtHE
Leo jioni Jumamosi, idadi ya wanaharakati wa Kitunisia walifanya mkusanyiko kuunga mkono upinzani wa Palestina na watu wa Palestina, mbele ya ukumbi wa mji wa Tunis.

waende israel wakawe chakula cha mamba. kuandamana unafikiri kutafanya israel isitishe mashambulizi?
 
Hilo gorofa lililobomoshwa nitashangaa kama viongozi wa hamas watakuwa wamo humo. Ukiisha ichokoza hivyo israel ni either utafute handaki au ukimbie nchi.
Mara nyingi viongozi wakubwa wanakaa kwenye basement ikiwepo vita namna. Hawawezi kaa kwenye jengo la ghorofa 14 na jengo maarufu Gaza nzima.

Ila nyumba ya kiongozi mkuu wa Hamas kwenye Gaza strip imeshambuliwa.
 
viongozi wa hamas wengi wapo uturuki na ukimbizini, wanaongea wakiwa mbali mkuu.
 
wayahudi woote duniani huwa lazima waende walau miezi 6 kutumikia jeshi israel. marekani kuna wayahudi karibia 10m, ulaya ni wengi pia, australia na kwengine. wote hao ni wanajeshi, na ikitokea vita namna hii wanaweza kuitwa kurudi kupigania nchi yao.
Duuuh! hii tungeichukua nasisi,ili kuvimbiana kupungue.Huko sidhani kama Kuna inshu za mwanajeshi kumpiga dereva wa BUS makofi,maana anajua akiriakti ni mtiti.Tushukuru huku kuna wanaochukua mafunzo kwa gharama za serikali,halafu wanajipigia tu raia,waliotoa pesa kwa njia ya kodi,ili wakapate mafunzo.Kwanza Rais aamuru BOGI moja likatwe,liende kusaidia kufanya operesheni huko Gaza,tudumishe ushirikiano na Israeli au Palestina.
 
viongozi wa hamas wengi wapo uturuki na ukimbizini, wanaongea wakiwa mbali mkuu.
Kuna mmoja nimemuona amevaa kijeshi anasema yuko tayari afungiwe bomb arushwe nalo Tel aviv, alikuwa anawatia morali vijana wake. Tatizo humo gaza ni kama manzese pamebanana huwezi kujua hamas ni nani na nani ni raia.
 
1696700840341.png
 
Lex Friedman mwandishi nguli katika mahojiano exclusive na waziri mkuu wa Israeli Mh. Benjamin Netanyahu

View: https://m.youtube.com/watch?v=2OnxK94kzCI

Mheshimiwa Benjamin Netanyahu anatupa za ndani kuhusu taifa la Israeli na raia wake, uwekezaji, uchumi wasoko huru, demokrasia, mihimili 3 ya dola inavyofanya kazi, maendeleo ya taifa hilo katika nyanja mbalimbali kiasi cha kuwa nchi-tajwa ktk kila teknolojia, Cyber + AI- Artificial Intelligence, defence, market segments, market monopoly... demokrasia ya ku balance wengi wape na hapo hapo kuwalinda wachache au mtu mmoja mmoja majority rights vis-à-vis individual rights

Benjamin Netanyahu mwanafuzi mahiri aliyetwaa digrii kadhaa kutoka chuo kikuu tajwa duniani cha MIT Massachusetts Institute of Technology kilichopo Cambridge, Massachusetts USA ... chuo kinatoa wahitimu vichwa vikali sana wa mfano ...

Upande wa siasa za kimataifa anajibu masuala mengi .............Mh. Benjamin Netanyahu nimewahi kuhojiwa na vituo viwili vya Iran na kituo kimoja kikiangaliwa views 16,000,000 na kingine zaidi 25,000,000 views za wa Iran walitazama .... hiyo inakupa picha pana zaidi ....

Source : Benjamin Netanyahu
 
“Niliwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, kwanza niliwaagiza kusafisha makazi ya magaidi waliojipenyeza – operesheni hii inafanyika saa hizi.

"Wakati huo huo, niliamuru vita vya kulipiza kisasi kwa nguvu na kwa kiwango ambacho adui hakuwahi kujua.

"Adui atalipa gharama ambayo hajawahi kujua. Wakati huo huo, natoa wito kwa raia wote wa Israeli kutii maagizo ya jeshi na mengine watakayopewa na mamlaka.

"Tuko kwenye vita na tutashinda.'

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu
Wameshatikiswa wametikisika,, safi sana. Tusisikie upande mwingine wakipiga mayowe.
 
Kuna mmoja nimemuona amevaa kijeshi anasema yuko tayari afungiwe bomb arushwe nalo Tel aviv, alikuwa anawatia morali vijana wake. Tatizo humo gaza ni kama manzese pamebanana huwezi kujua hamas ni nani na nani ni raia.
anasema hivyo ila bomb likidondoka karibu yake anavyoruka na kukimbia anakuwa wa kwanza. they are just cowards.
 
kinachosikitisha ni kwamba, majority ya raia wa israel waliovuka 18 ni wanajeshi. hamas ametoa wito kwa wapalestina gaza na west bank waingie vitani wakati hawana ujuzi wa kivita. anataka wakateketee?
 
Back
Top Bottom