H
Urusi ina zaidi ya mwaka vitani na mafanikio yake na makosa yake hayahitaji nguvu nyingi kuyaona, Israel ina shambulizi halijatimiza hata 24hrs tiyari unailinganisha na Urusi.
KGB ilikuwepo wakati USSR inagawana mbao, Mossad imeipambania Israel ambayo imevamiwa mara nyingi na maadui superior lakini haipotezwi.
Tulete list ya missions za Mossad vs za FSB hapa tuone nani ana successful missions nyingi?
Si lazima niwepo kwenye ule uzi, sikuanzisha mimi. Nisipokuwepo unapungukiwa nini, zaidi ya mwaka vita inaendelea na sina muda wa kuzungumza jambo lilelile muda wote. Hii ya Israel hata miezi haitopita itakuwa imeisha na mambo mengine yaendelee.
Tuseme silaha za Magharibi sio bora, Israel wamezitumia miaka yote kupigana na maasimu wao na matokeo unayajua. Una silaha bora, ni jeshi la pili duniani ila unapigana na nchi dhaifu haipo hata kwenye majeshi 20 bora duniani unakaa mwaka mzima na silaha zako bora hata air dominance tu huna.
Ukibanwa unaleta visingizio Marekani inaisaidia Ukraine, wakati huo unadai silaha za Marekani ni dhaifu. Hutosikia Israel inalialia Hamas na Hezbollah kutumia silaha za kupewa na Iran.
Sio kwamba ni lazima uwepo ila tatizo ni ww kutokuja kutupa mrejesho wa silaha unazo ziita bora kuliko zingine.
Kwa hiyo makosa ya Israel kushindwa kuidhibiti hamasi zaidi ya miaka 15 ndo yana hitaji akili nyingi kuyaona sio?
Urusi inapambana zaidi ya mwaka na nchi yenye kila aina ya silaha kutoka kwa washirika wa nato mpaka maghara yao yameanza kukaukiwa silaha na yenye jeshi la watu zaidi 250,000 bado maelfu ya mamluki kutoka kote duniani.
Lakini Israel imepambana na Hamas ambaye haimiliki chochote zaidi ya bunduki na viroketi kwa zaidi miaka kumi na tano lakini mpaka sasa hatuja wahi kuona maajabu yeyote na mpaka sasa Hamas ipo na inaendelea kufanya mashambulizi yaliyo bora kuliko jana.
Alafu acha kunilisha maneno hakuna sehemu yeyote ambayo nisha wahi kuziponda silaha za kimagharibi kuwa ni dhaifu na silaha za Urusi ni bora kama kuna sehemu nilisha sema hivyo niletee ushahidi.
Hiyo hoja ya silaha za nchi fulani ni bora kuliko zingine uliileta ww.
Na ulikuwa ukibanwa unakimbilia kusema kuwa tusubili offensive ianze ndo tutakuelewa lakini cha ajabu ilipo anza ukaona mambo yanaenda kombo ukakimbia mazima.
Mm naamini silaha zote ni bora kutokana na jinsi mtumiaji atavyo itumia silaha husika, na ndio maana silaha za kirusi zilishindwa kwenye vita ya six day, lakini wakati huo silaha za kimagharibi zilishwindwa kwenye medani huko nchini ,Yemen, Syria, Vietnam ,na pia hizo silaha za kimagharibi zimeshindwa kuimaliza hamas kwa zaid ya miaka 15.
Haaa yaani silaha bora zenye thamani ya $50 billion mpaka sasa zimeshindwa kuisaidia Ukraine kukomboa hata wilaya moja 😀😀😃😃😃😃 dah