LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Yeah, Bennett alikua ni Komandoo, kama alivyokuwa Benjamin Neyanyahu. Maana Netanyahu naye alikua ni kiongozi wa kikosi cha Makomandoo wa IDF.
Sema Bennett alizingua, wakati wake ndiyo hayo makundi yalijijenga sana.

Ariel Sharon nae alikua mtata sana, nakumbuka siku anachaguliwa kuwa waziri Mkuu wapalestina walilaani sana Kwa jinsi alivyokua na misimamo mikali.

Wakati Marekan wanataka kuvamia Afghanistan kumsaka Osama, Israel ilikua inashambuliwa Sasa USA wakasema Israel asijibu Kwa vile itaamsha ghadhabu ya mataifa ya Kiarabu wakati huo.

Ariel hakusikiliza kelele zozote alivurumisha makombora na akisisitiza usalama wa waisrael hauhitaji ushauri wa taifa lolote.
 
Wapalestina Wajanja sana Wanajifanya eti kwamba hicho ni kikundi cha Wanamgambo wa Sheria Kali Ndo kinafanya hayo Mashambulizi,

Ila kwa sisi tuliosomea Cuba tunajua kwamb hilo Ni Jeshi Kamili la Palestina linatoa kipigo Kwa kivuli cha Wanamgambo.
 
Maisha ya hao jamaa ni ya uhasama hata wakiwa nje ya mipaka ya ardhi zao...

Miaka ya nyuma nilipata kusoma chuo ambacho kina Wapalestina kadhaa, sasa kuna intake moja akaja dada Myahudi ila bahati nzuri wadau tunaojua hizi migogoro yao tukamtonya yule Myahudi juu ya uwepo wa 'ndugu zake hao' ili ajue ni namna gani aweze kuepuka mtifuano...ikabidi a lay low tu

Sikuwahi iona hii, shukrani umenipa kitu cha kutazama weekend...

Kama uliipenda Fauda, hii nayo utaifurahia bila shaka.

Wale uhasama wao mkali sana. Mfano hapa Kuna raia watapata misukosuko na kupoteza maisha bila sababu. Hamas wako Kwa raia, jamaa wakirusha makombora wanatandika makazi ya watu. Very tricky
 
Usicheze na waisrael tangu watoke Misri hadi sasa maisha yao yote yamekuwa vita.
 
Halafu kuna Waafrika kutwa kucha wanashinda makanisani kujidai eti wana muomba Mungu wa Israel asiyeshindwa.

Waisraeli hao wanao daiwa kwamba ndio taifa la Mungu, wanashambuliwa vibaya mno.

Tukisema kwamba Mungu huyo hayupo.

Walokole hao wa Mungu wa Israel ndio wa kwanza kubisha...[emoji1][emoji1]
 
Screenshot_20231007-203759.jpg
Screenshot_20231007-203710.jpg

Historia inaonyesha Israel ameua wapalestina wengi tangu kuanza kwa Choko Choko yao hiyo
 
H
Urusi ina zaidi ya mwaka vitani na mafanikio yake na makosa yake hayahitaji nguvu nyingi kuyaona, Israel ina shambulizi halijatimiza hata 24hrs tiyari unailinganisha na Urusi.

KGB ilikuwepo wakati USSR inagawana mbao, Mossad imeipambania Israel ambayo imevamiwa mara nyingi na maadui superior lakini haipotezwi.

Tulete list ya missions za Mossad vs za FSB hapa tuone nani ana successful missions nyingi?

Si lazima niwepo kwenye ule uzi, sikuanzisha mimi. Nisipokuwepo unapungukiwa nini, zaidi ya mwaka vita inaendelea na sina muda wa kuzungumza jambo lilelile muda wote. Hii ya Israel hata miezi haitopita itakuwa imeisha na mambo mengine yaendelee.

Tuseme silaha za Magharibi sio bora, Israel wamezitumia miaka yote kupigana na maasimu wao na matokeo unayajua. Una silaha bora, ni jeshi la pili duniani ila unapigana na nchi dhaifu haipo hata kwenye majeshi 20 bora duniani unakaa mwaka mzima na silaha zako bora hata air dominance tu huna.
Ukibanwa unaleta visingizio Marekani inaisaidia Ukraine, wakati huo unadai silaha za Marekani ni dhaifu. Hutosikia Israel inalialia Hamas na Hezbollah kutumia silaha za kupewa na Iran.
Sio kwamba ni lazima uwepo ila tatizo ni ww kutokuja kutupa mrejesho wa silaha unazo ziita bora kuliko zingine.

Kwa hiyo makosa ya Israel kushindwa kuidhibiti hamasi zaidi ya miaka 15 ndo yana hitaji akili nyingi kuyaona sio?
Urusi inapambana zaidi ya mwaka na nchi yenye kila aina ya silaha kutoka kwa washirika wa nato mpaka maghara yao yameanza kukaukiwa silaha na yenye jeshi la watu zaidi 250,000 bado maelfu ya mamluki kutoka kote duniani.
Lakini Israel imepambana na Hamas ambaye haimiliki chochote zaidi ya bunduki na viroketi kwa zaidi miaka kumi na tano lakini mpaka sasa hatuja wahi kuona maajabu yeyote na mpaka sasa Hamas ipo na inaendelea kufanya mashambulizi yaliyo bora kuliko jana.

Alafu acha kunilisha maneno hakuna sehemu yeyote ambayo nisha wahi kuziponda silaha za kimagharibi kuwa ni dhaifu na silaha za Urusi ni bora kama kuna sehemu nilisha sema hivyo niletee ushahidi.
Hiyo hoja ya silaha za nchi fulani ni bora kuliko zingine uliileta ww.
Na ulikuwa ukibanwa unakimbilia kusema kuwa tusubili offensive ianze ndo tutakuelewa lakini cha ajabu ilipo anza ukaona mambo yanaenda kombo ukakimbia mazima.

Mm naamini silaha zote ni bora kutokana na jinsi mtumiaji atavyo itumia silaha husika, na ndio maana silaha za kirusi zilishindwa kwenye vita ya six day, lakini wakati huo silaha za kimagharibi zilishwindwa kwenye medani huko nchini ,Yemen, Syria, Vietnam ,na pia hizo silaha za kimagharibi zimeshindwa kuimaliza hamas kwa zaid ya miaka 15.

Haaa yaani silaha bora zenye thamani ya $50 billion mpaka sasa zimeshindwa kuisaidia Ukraine kukomboa hata wilaya moja 😀😀😃😃😃😃 dah
 
Nakazia✍️✍️✍️
Wale askari wa jwtz wanaopiga raia na kunyang'anya magwanda wapelekwe Gaza chap kutuliza mzozo ili wapate uzoefu
Dah nawacheki hamas aisee...kikundi lakini kimejipanga sana...wana technology nzuri kutuzidi..na sisi jeshi letu liige vitu hivi..
Hatuwezi kufikia israel lakini tukifika kwa hamas inatosha
 
Israel atapata kifinyo ngoja mtaona

Gaza ni eneo dogo sana...

Israel kinachomuwia vigumu ni kwamba eneo la Gaza ni sehemu pia ya makazi ya Wapalestina, hivyo hawezi kishisha mitulinga yenye nguvu zaido atapiga maeneo kadhaa ambayo anahisi ni ngome za Hamas...
 
Toka ameondoka Mossad na baadae kufariki Meir Dagan kuna kujisahau kwingi sana pale Mossad.
Netanyahu asipokula kichwa cha Mossad Spy Chief wa sasa nitashangaa sana.
 
Ariel Sharon nae alikua mtata sana, nakumbuka siku anachaguliwa kuwa waziri Mkuu wapalestina walilaani sana Kwa jinsi alivyokua na misimamo mikali.

Wakati Marekan wanataka kuvamia Afghanistan kumsaka Osama, Israel ilikua inashambuliwa Sasa USA wakasema Israel asijibu Kwa vile itaamsha ghadhabu ya mataifa ya Kiarabu wakati huo.

Ariel hakusikiliza kelele zozote alivurumisha makombora na akisisitiza usalama wa waisrael hauhitaji ushauri wa taifa lolote.
Kuna kitu aliwafanya alipokuwa Waziri wa Ulinzi. Sasa alipokuja kuwa waziri mkuu ndiyo wakaona huyu mwehu wamempa nchi sijui wanataka atufanyeje?
 
Back
Top Bottom