LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
naunga hojaa...nyambizii aina ya ohio class zimetinga maeneoo mazee dah...gaza itabaki historiaa...mwarab anazidi kupelekewa motoo
IMG_20231106_063336_344.jpg
 
Gaza imekuwa ikisumbua muda mrefu toka Enzi za zamani mno limekuwa mwiba kwa Israel karne na karne kabla hata Yesu Kristo hajazaliwa

Dawa yake Kwa ajili ya Usalama na amani ya taifa la Israel,Israel iteke eneo la Gaza na ilikalie moja kwa moja milele

Hii vita ya sasa iwe ya kuchukua hilo eneo moja kwa moja sio kupiga na kuondoka
Nadhani Plant B ,itakuwa ni hiyo, kwa sasa tayari wameigawa Gaza pande mbili.
Kwa kitendo hicho tu Hamas kama chama kitakuwa hakina muunganiko kati ya kaskazini na kusini, lakini pia kwa upande Hamas kijeshi watakuwa wamedhiofushwa sana kwani hakuna msaada watakapokuwa kutoka kwa raia wao au marafiki
Chakula, maji, vifaa tiba, madawa, na hata vifaa vya kivita.
Hii ndiyo maana halisi ya Netanyau kusema ni vitu ngumu na ya muda mrefu. Wakishawazingira basi wao Hamas watabaki mashimoni hadi waishiwe huduma za kijamii na mwisho watajisalimishe au wafe huko kwenye mashimo.
 
Kinachofanywa ni kuziba mashimo yote na kuyadhibiti, hakuna wa Kutoka Wala wa kuingia. Nadhani hamasi wajiandae tu kwenda kupokea bikra wao walioahidiwa.
 
Gaza imekuwa ikisumbua muda mrefu toka Enzi za zamani mno limekuwa mwiba kwa Israel karne na karne kabla hata Yesu Kristo hajazaliwa

Dawa yake Kwa ajili ya Usalama na amani ya taifa la Israel,Israel iteke eneo la Gaza na ilikalie moja kwa moja milele

Hii vita ya sasa iwe ya kuchukua hilo eneo moja kwa moja sio kupiga na kuondoka
1699332158861.png
 
Idara Kuu ya Usalama ya Marekani imetangaza kuwa Ohio Nuclear Sub marine imewasili Mashariki ya Kati katika mkakati wa kuhakikisha Eneo hilo linabaki salama

Source: Al jazeera news
 
Na Tayari Gaza imeshagawanywa mara mbili. North Gaza na South Gaza. Sijajua intention ya Israel ni ipi.
 
Watu mnachanganya sana Israel nchi na Israel ambae ni Jacob (Yakoub) baba wa Yusuf.

Wana wa Israel (Yakoub) ni tofauti na nchi inayoitwa "Israel" iliyoanzishwa na Muingereza.
Unayechanganya ni wewe, kwanza Kwa kuikopi BIBLIA TAKATIFU na tena kuipotosha hapahapa, Wewe unaijua Kaanani?

Na unajua Kwanini Yakobo aliitwa Israel?

Sasa kama unakubali kuna WaTanzania hiyo Tanzania ikwapi huoni unajichanganya mwenyewe?

Unachoongea hapa ni kitu hata hukielewi...

Soma BIBLIA TAKATIFU Jeremia 24:1-10 ndipo utaelewa unavyojichanganya.

Tunaongelea Mungu muumbaji na mmiliki wa vyote versus nguvu zingine....
 
Nadhani Plant B ,itakuwa ni hiyo, kwa sasa tayari wameigawa Gaza pande mbili.
Kwa kitendo hicho tu Hamas kama chama kitakuwa hakina muunganiko kati ya kaskazini na kusini, lakini pia kwa upande Hamas kijeshi watakuwa wamedhiofushwa sana kwani hakuna msaada watakapokuwa kutoka kwa raia wao au marafiki
Chakula, maji, vifaa tiba, madawa, na hata vifaa vya kivita.
Hii ndiyo maana halisi ya Netanyau kusema ni vitu ngumu na ya muda mrefu. Wakishawazingira basi wao Hamas watabaki mashimoni hadi waishiwe huduma za kijamii na mwisho watajisalimishe au wafe huko kwenye mashimo.
Ni kweli
 
Majibu yapo humu

Nimeyasoma hayo majibu.

Waarabu wanapaswa kujilaumu wenyewe kuhusu hili kosa walilofanya. Baadhi yao walikuja kulegeza msimamo when it was too late.

Hapa tulipofikia, kile ambacho walikikataa miaka ile ni kikubwa zaidi kuliko kilichopo mezani hivi sasa.
 
Ni makosa kuwahukumu wapalestina wa sasa kwa makosa ya wazee wao.
 
Hoja ya Netanyahu ni kwamba wapalestina ni waarabu walivamia, na ndio hoja za hao mashetani wa west aka Zionism, ni hoja dhaifu ambayo inapingika kirahisi kwa
1. Sayansi
2. Historia
3. Dini.

1. Kisayansi wapalestina si waarabu per Se, ukipima gene zao asilimia hadi 60 zinafanana na wayahudi na watu wa kale wa kaanani, Kifupi wapalestina wana gene kali za kiyahudi kuliko hao wanaojiita wayahudi, ila Netanyahu na washenzi wenzake kila siku wanapingana na hawa wana sayansi.

2. Kidini ukisoma Conquest za kiisilamu maeneo yote Egpty, Nenda mpaka Spain Andalusia, nenda North America, Iran mpaka Mongolia huko waarabu walipeleka tu viongozi hawakujichanganya na raia husika za Hizo nchi ndio maana Egpty mpaka Leo Imepakana na Ghuba ila ukipima Dna Zao ni chini ya Asilimia 20 wana Dna Ya kiarabu.

So waarabu hawapo popote si Egpty, si Palestina, si Algeria si Morocco, Hata ukienda Iran ambayo imepakana karibu na waarabu ni Kama asilimia 2 tu dna yao ni ya Kiarabu.

Hivyo si kweli kwamba wale ni wavamizi toka Nchi za kiarabu

3. Angalia Culture Wapalestina na levant kwa Ujumla hawavai Kanzu, nguo zao tofauti na waarabu wengine, Aina zao za kucheza, vyakula vyao, na mambo mengine tofauti kabisa na waarabu wenyewe.

So wapalestina ni wapalestina, mpalestina wa Leo na aliekuwepo hapo Miaka 3000 aliopita ni yule yule, hatuna Haja ya kuzunguka, DNA pekee Inatosha kuthibitisha hili. Ashkenaz Jews Leo wana DNA dhaifu ya kiyahudi kushinda hao Wapalestina wanao waua.

Ukitaka kuelewa Mchezo wa Zionist/British wana force kila mtu awe mwarabu, Mcopt wa Egpty hataki kuitwa mwarabu ila wanalazimisha, Berbers wa Libya ama Algeria hataki kuitwa mwarabu ila anaitwa hivyo hivyo, Druze, amazhingh, Chechens, kushite, Assyrian, Samaritan na makundi kibao hapo Middle East yoyote yanajumushwa yanaitwa tu waarabu hali ya kuwa waarabu ni wale tu wanaoishi kwenye ile Ghuba.
Kwa mara kadhaa sasa hoja zako nyingi zimejikita dhidi ya Netanyahu. Matokeo yake unakosa kuwa objective. Nimeanza kuona dalili za kujikuta tunaanza kujadili conspiracy theories!

Iko hivi, hoja za Netanyahu ni zake Netanyahu. Mimi nina hoja zangu mwenyewe na nitazingatia facts za kisayansi!

Nianze kwa kusema kwamba, hakuna tafiti ya kisayansi inayosema kwamba Wapalestina wa sasa sio Waarabu ama hawana asili ya Kiarabu. Tafiti zilizopo zinaonesha asili ama chimbuko la Modern Palestinians ni eneo linalofahamika kama Arabian Peninsula miaka mingi iliyopita.

Upo utafiti (genetic research) uliobaini kuwa Wapalestina wa sasa, Wasyria na Wairaki wana baadhi ya genes za sub-Saharan African (Mwafrika mweusi), wakati jamii zingine za watu wasio Waarabu katika eneo la Mashariki ya Kati (mfano Jews) hawana hizo genes. Ukizingatia ukaribu wa Arabian Peninsula na jamii za watu wa kusini mwa jangwa la Sahara, inaonesha kuwa hizo jamii tatu zinahusiana historically.

Waarabu ambao wanafahamika kama "real Arabs" walitokea Arabian Peninsula na wao ndio chanzo cha kuuneza Uarabu pale Mashariki ya Kati. Miongoni mwa jamii ambazo ziliambukizwa Uarabu kupitia intermarriage n.k. na kuchangamana na lugha pamoja na tamaduni za "real Arabs" ni pamoja na baadhi ya "Wapalestina" waliokuwepo katika eneo lililofahamika kama "Palestine".

Kwa mujibu wa utafiti, hawa "real Arabs" wa Arabian Peninsula ni weusi kwa asilimia 35 genetically na ndio chanzo cha uwepo wa baadhi ya genes za sub-Saharan African kwa Wapalestina wa sasa, Wasyria na Wairaki.

Nilisema awali kwamba hawa Wapalestina wa hivi sasa ni tofauti na waliokuwepo huko nyuma wakati wa "Palestine". Hawa wa sasa chimbuko lao ni arabized Palestines waliotokana na muunganiko wa "real Arabs" na "Wapalestina wa kale" ndio maana hawa wa sasa wanaitwa "Wapalestina wa Kiarabu". Hakuna conspiracy theories hapo maana hata wao wenyewe wanajitambulisha hivyo rasmi!

Hiki hapa chini ni kipande cha Palestine Liberation Organization (PLO) charter ya mwaka 1964 (zingatia maneno niliyopigia mstari mwekundu). Hoja yako kwamba Zionist/British wanalazimisha kila mtu awe Mwarabu haina mashiko.
plo.jpeg

Umeleta utafiti kwamba Wapalestina wana uhusiano wa kiasi fulani na Wayahudi genetically. Nakubaliana na wewe!

Upo utafiti mwingine pia uliobaini ukaribu wa genes kati ya Wapalestina wa sasa na Wayahudi wa sasa wakiwemo Ashkenazi ambao walitokea sehemu za Ulaya wakati wa Zionism. Pia, kuna suggestions kwamba baadhi ya genes za Wapalestina zilitokana na Wayahudi huku kukiwa na mfanano wa kipekee wa genes kati ya Wapalestina na Wayahudi kwa ujumla kuliko either na Waarabu wa Arabian Peninsula ama na Europeans.

Maana yake ni kwamba, hizo jamii mbili chimbuko lao ni moja kulingana na huo utafiti (sources zipo mwishoni). Huu utafiti unazima yale madai kwamba kuna "Wayahudi feki" waliotoka Ulaya na kuvamia eneo la "Palestine".

Vyanzo/sources:
Utafiti kuhusu Waarabu (wakiwemo Wapalestina wa sasa) kuwa na vinasaba vya sub-Sahara African:

Uhusiano wa Wayahudi na Mashariki ya Kati:

Uhusiano wa vinasaba kati ya jamii zote za Kiyahudi:

Uhusiano wa vinasaba kati ya Wayahudi na Waarabu:

Uhusiano wa vinasaba kati ya jamii za watu wa Mashariki ya Kati:
 
Mbona unatudanganya kaka?!
Maeneo aliyoteka Israel yote ni ya kupanua Jewish state na yeye ndiye aliyeanza kuvamia hakuanza kuvaniwa.
Pia Palestine ilitakiwa kupaya uhuru Toka kwa Uingereza sip Jordan na Egypt kama unavyotudanganya hapa.
Kasome historia kuhusu hizi vita mbili:

1) 1948 Arab-Israeli War

2) 1967 Six-Day War

Sio lazima ulete mrejesho!
 
Unataka kuleta ubishi usio na msingi. Israel kama nchi imeanzishwa na Muingereza mwaka 1948.
Hoja yako ni nini hasa?

Syria ya sasa ilianzishwa na Mfaransa; Lebanon ya sasa ilianzishwa na Mfaransa.

Jordan ilianzishwa na Muingereza; Iraq ya sasa ilianzishwa na Muingereza. Nchi hizo zilikuja kupata uhuru baadaye.

Nchi nyingi zilizopo hapo Mashariki ya Kati hivi sasa ziliundwa baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia. Soma 'The partition of the Ottoman Empire'.

Nikukumbushe; hata Tanganyika ilianzishwa na wakoloni kisha baadaye ikapata uhuru.

So, unachotaka kusema ni nini? Kuwa muwazi!
 
Nilishauri kwamba tuutazame huu mgogoro katika perspectives zote! Nina maswali kadhaa kwaajili yako:

1) Ni kwa sababu zipi Wayahudi wanaofahamika kama "Zionists" hawana uhusiano na hilo eneo?

2) Je, Wayahudi waliotoka Ulaya na kwingineko na kuhamia "Palestine" chimbuko ama asili yao ni wapi hasa?

3) Ni nani alikuwa na uhalali (legality) wa milki ya eneo lililoitwa "Palestine" wakati wa Zionism?

Mfano wako kuhusu Wakongo nimeshauzungumzia. Sijaukwepa! Tanzania ni sovereign state. Hakuna uhalali wowote wa hao Wakongo kudai "nchi yao" ndani ya Tanzania bila ya Tanzania yenyewe kupoteza uhuru wake kwanza.

Vilevile, Tabora haijawahi kuwa nchi huru yenye mipaka inayotambulika. Kulingana na sheria ya kimataifa, mfano wako hauna uhalisia. Huwezi kudai kurudishiwa kitu ambacho haukuwa nacho hapo awali!
Unamjibu vizuri sana, nimefuatilia tangu kule juu. Lakini anashupaza tu shingo.. ili aweze kujifunza anatakiwa kuwa na open minded badala ya fixed minded na kutake side.
 
Wapalestina Wakristo hata 3% hawafiki, ni negligible asilimia chache kuliko hata Wakristo wa Saudi Arabia. So tukisema takribani Wapalestina wote ni Waislamu hiyo sio ajabu.

Si ni kama hivi umesema unavyohisi, au ulitaka niseme kila kitu cha Wakristo Palestina? Mbona hujasema wanavyonyanyaswa uko Gaza hadi wapo wachache, au nayo hii tumlaumu USA. Almost Wakristo wote wa Palestina wapo West Bank.
Takwimu ni 0.05
 
Kwa mara kadhaa sasa hoja zako nyingi zimejikita dhidi ya Netanyahu. Matokeo yake unakosa kuwa objective. Nimeanza kuona dalili za kujikuta tunaanza kujadili conspiracy theories!

Iko hivi, hoja za Netanyahu ni zake Netanyahu. Mimi nina hoja zangu mwenyewe na nitazingatia facts za kisayansi!

Nianze kwa kusema kwamba, hakuna tafiti ya kisayansi inayosema kwamba Wapalestina wa sasa sio Waarabu ama hawana asili ya Kiarabu. Tafiti zilizopo zinaonesha asili ama chimbuko la Modern Palestinians ni eneo linalofahamika kama Arabian Peninsula miaka mingi iliyopita.

Upo utafiti (genetic research) uliobaini kuwa Wapalestina wa sasa, Wasyria na Wairaki wana baadhi ya genes za sub-Saharan African (Mwafrika mweusi), wakati jamii zingine za watu wasio Waarabu katika eneo la Mashariki ya Kati (mfano Jews) hawana hizo genes. Ukizingatia ukaribu wa Arabian Peninsula na jamii za watu wa kusini mwa jangwa la Sahara, inaonesha kuwa hizo jamii tatu zinahusiana historically.

Waarabu ambao wanafahamika kama "real Arabs" walitokea Arabian Peninsula na wao ndio chanzo cha kuuneza Uarabu pale Mashariki ya Kati. Miongoni mwa jamii ambazo ziliambukizwa Uarabu kupitia intermarriage n.k. na kuchangamana na lugha pamoja na tamaduni za "real Arabs" ni pamoja na baadhi ya "Wapalestina" waliokuwepo katika eneo lililofahamika kama "Palestine".

Kwa mujibu wa utafiti, hawa "real Arabs" wa Arabian Peninsula ni weusi kwa asilimia 35 genetically na ndio chanzo cha uwepo wa baadhi ya genes za sub-Saharan African kwa Wapalestina wa sasa, Wasyria na Wairaki.

Nilisema awali kwamba hawa Wapalestina wa hivi sasa ni tofauti na waliokuwepo huko nyuma wakati wa "Palestine". Hawa wa sasa chimbuko lao ni arabized Palestines waliotokana na muunganiko wa "real Arabs" na "Wapalestina wa kale" ndio maana hawa wa sasa wanaitwa "Wapalestina wa Kiarabu". Hakuna conspiracy theories hapo maana hata wao wenyewe wanajitambulisha hivyo rasmi!

Hiki hapa chini ni kipande cha Palestine Liberation Organization (PLO) charter ya mwaka 1964 (zingatia maneno niliyopigia mstari mwekundu). Hoja yako kwamba Zionist/British wanalazimisha kila mtu awe Mwarabu haina mashiko.
View attachment 2806818

Umeleta utafiti kwamba Wapalestina wana uhusiano wa kiasi fulani na Wayahudi genetically. Nakubaliana na wewe!

Upo utafiti mwingine pia uliobaini ukaribu wa genes kati ya Wapalestina wa sasa na Wayahudi wa sasa wakiwemo Ashkenazi ambao walitokea sehemu za Ulaya wakati wa Zionism. Pia, kuna suggestions kwamba baadhi ya genes za Wapalestina zilitokana na Wayahudi huku kukiwa na mfanano wa kipekee wa genes kati ya Wapalestina na Wayahudi kwa ujumla kuliko either na Waarabu wa Arabian Peninsula ama na Europeans.

Maana yake ni kwamba, hizo jamii mbili chimbuko lao ni moja kulingana na huo utafiti (sources zipo mwishoni). Huu utafiti unazima yale madai kwamba kuna "Wayahudi feki" waliotoka Ulaya na kuvamia eneo la "Palestine".

Vyanzo/sources:
Utafiti kuhusu Waarabu (wakiwemo Wapalestina wa sasa) kuwa na vinasaba vya sub-Sahara African:

Uhusiano wa Wayahudi na Mashariki ya Kati:

Uhusiano wa vinasaba kati ya jamii zote za Kiyahudi:

Uhusiano wa vinasaba kati ya Wayahudi na Waarab

Uhusiano wa vinasaba kati ya jamii za watu wa Mashariki ya Kati:
Vyema Ukiweka Dna uweke na Percentage zake, 4-15% ya Sub Sahara Dna prove nothing mkuu, mtu mwenye 60% ya Canaanite na 10% ya Sub Sahara utasema huyo mtu katoka Africa? Hizo evidence zako hebu zirudie vizuri kuzisoma.

Pia kama percentage ndogo ni Kigezo cha kutokua mpalestina basi hata jews wa sasa hawana haki Hio sababu nao pia wana DNA zilizochanganyika na sub saharan

Pia wapalestina wamekua arabized karne zaidi ya 10 zilizopita na we unaweka ushahidi wa PLO serious? Kundi ambalo lipo baada ya Ukoloni wa kingereza?

AS I told you before Levant Arabs na waarabu wa kawaida (Gulf) ni mbingu na Ardhi hata sasa hivi hapa Tanzania kuna omba omba wanatoka Syria na maeneo mengine ya Levant kama wakimbizi, mtu asipokuambia hawa sio wazungu huamini, Hapa Kariakoo watu kibao wanashangaa

1. Mwarabu wa Gulf Anavaa Kanzu mwanaume na Baibui mwanamke Plain most of time, Levant arabs wanavaa Suruali na Wanawake hata kama wanavaa Hijab kuna sense of Fashion

2. Waarabu wanakula Wali, pilau, Biriani na vyakula vingine vyenye asili ya india/Iran tunafanana nao kama huku ila Levants Arab utakuta Majani majani, Kebab, na vitu vingine ambavyo sio much cooked, kuna Hotel ya kilebanon mjini inaitwa Al Basha ukipata wasaa Nenda kaangalie Utaona Vyote Culture, appearance na mapishi.

3. Mwarabu wa gulf yupo dark wakati wa Levant ni kama wazungu etc

Kifupi mkuu uarabu kwa definition ya sasa sio Race wala Ethnicity bali ni muunganiko tu wa Nchi zinazoongea kiarabu, Mtu wa Sudani ni mweusi/Kushite anaitwa mwarabu, mtu wa Lebanon ni Levant anaitwa mwarabu etc
 
Back
Top Bottom