Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Assistant Superintendent of Police (ASP) Fatuma Kigondo. Huyu ni afisa wa Jeshi la Polisi. Fatuma ndiye yule ‘afande’ aliagiza ‘JM’ abakwe na kulawitiwa.Assistant Superintendent of Police (ASP) Fatuma Kigondo ni msaidizi wa mkuu wa kituo cha polisi - Bunge (Dodoma). Ni afisa anayefahamika sana.
‘JM’ alikuwa mfanyakazi wake. ASP Fatuma Kigondo akahisi bwana wake (jina lake tunahifadhi kwa hatua za sasa) ana mahusiano na ‘JM’. Akaagiza atekwe.
ASP Fatuma Kigondo anamiliki grocery na liquor store Dodoma. JM ni mmoja kati ya wafanyakazi katika moja kati ya grocery au bar za ASP Fatuma Kigondo.
JM alikuwa anatoka kazini saa tano usiku, akavamiwa na pikipiki mbili, wakashuka watu watano wakiwa na visu mkononi. Wakamchukua na kuondoka naye.
JM amebakwa na kulawitiwa usiku huo hadi kesho yake asubuhi. Video ile imerekodiwa asubuhi wakati wahuni hao wanamaliza kufanya uhalifu.
Chanzo: Boniface Jacob Kupitia X na pia Martin Maranja kaandika
Pia soma: Watuhumiwa wa mande ya Ubakaji na ulawiti waliotumwa na afande wakamatwa
Pia, Kumbukumbu zinaonesha Askari Fatuma Kigondo aliwahi kutoa ushahidi Tarehe 18, Desemba 2017 akiwa shahidi wa upande wa Jamhuri kwenye Kesi dhidi ya JamiiForums, kwa kosa la kukataa kutoa “taarifa za mteja wao”.
Fungua kiungo hiki kusoma ushahidi huo: Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai waliomba taarifa za mteja bila kutaja ni kwa mujibu wa sheria gani