Suala la maendeleo ya watu kwa sasa kutoka kwa viongozi wa CCM na itikadi wanayoisimia, ni kama mfano wa uliopo ndani ya maandiko matakatifu kuhusu kiriba cha kale na divai ya kale. Ukale huo unahakisiwa ktk sura ya maendeleo toka Tanganyika ilipopata uhiru wake mwaka 1961 mpaka nchi yetu ilipo hivi sasa.
Huwezi kuweka divai mpya ktk kiriba cha zamani, kwa kuwa kiriba cha zamani huifadhiwa divai ya kale, na hali kadhalika divai mpya ktk kiriba kipya, la sivyo kwa kufanya hivyo kiriba cha kale kitapasuka na divai mpya itamwagika yote na kupotea.
Nchi hii inahitaji viongozi wapya na maono mapya ya kiitikadi kwa ajili ya kesho ya siha na afya njema ya mama Tanzania. Kauli za kibabaishaji za CCM mpya ni kutaka kucheza kamari na maisha na maendeleo ya ways kwa mara nyingine tena.