Hawajawekeza kwenye media kwa maana ya uwekezaji, bali media zote wamezitia hofu kupitia madaraka ya rais yanayotumika vibaya. Ukijaribu kufuatilia vizuri utaona kabisa kuwa ccm sio chama imara, ila kina mwenyekiti anayetumia madaraka yake kibabe, na kumuonea yoyote asiyemsujudia au kuisujudia ccm. Kwahiyo utawala huu wa mabavu na shuruti umetengeneza kukubalika bandia, kisha ndio kugeuzwa kuitwa uimara wa ccm.
Vyama vyote vinavyoongozwa na marais madictator hupewa sifa bandia kuwa ni imara, na huhakikisha washindani wao wote hawapati covarage kwenye media, ili wao tu ndio wasikike na kujifanya wanakubalika.
Hii ndiyo tunaita kujifariji au kukariri.
Media maarufu zenye subscribers wengi karibu zote zinapiga safari hadi miakoani kuonesha miradi iliyofanywa na jamaa kisha wanarusha kila kitu kila kona. Wanarusha hadi miradi ya choo au jiko la shule au zahanati.
Unafikiri mtu anaye fanya hivyo ametishwa?
Fedha za hizo safari anatoa wapi?
Media zote zinafanya live coverage ya matukio ya zinduzi zote za wale wa ngazi za juu kila kona ya nchi, unataka kusema wanafanya hivyo sababu wametishwa?
Hujaliona hilo jambo toka miaka angalau mitatu iliyopita? Watu wanakula mahindi, madafu, mapapai kule forodhani ufukweni, watu wanakaa chini na walemavu wajane, wazee, migogoro ya ardhi inatolewa maamuzi papo hapo kwenye misafara, teuzi katikati ya mikutano au hotuba.
Watu wanaongeza umiliki wa media za chama kama 'Channel Kumi', n.k. wewe bado unahisi vitisho tu?
Je ninyi upinzani mmewekeza angalau redio moja ya chama ya kurusha live matangazo hadi vijijini ambako wengi hawana smart phones hawaingii mitandaoni? Msifikiri watanzania wengi wana vifaa vya kuingia na kuona matangazo mitandaoni.
Kuna mikoa maskini huko wengi hawana simu wala computer.
Hiyo ya media kutorusha mambo ya chama chenu kwenye media inaweza kuwa hoja yako na mimi naikubali huenda ni vitisho, lakini tujiulize swali.
Hivi kama media flani ina mkataba wa ku-brand chama flani na mgombea wake, na katika Terms za mkataba wao wamekubaliana ili tukupe dau hili basi usitangaze brand ya mpinzani wetu hiyo ni kosa kibiashara?
Ukumbuke media nyingi binafsi zinaendeshwa kibiashara kama biashara zingine. Ni kama vile Emirates wanafadhili Arsenal wanaweka mashariti uwanja wenu na jezi zenu marufuku kuweka au kutangaza wapinzani wetu kama Qatar au KLM, n.k.
Je, utawalaumu Arsenal kwa kutoweka matangazo ya brand hizo zingine uwanjani kwao na kwenye vipindi vya TV zao?
MY TAKE: Kutangazwa na media flani siyo hisani bali ni biashara ambayo lazima uingie gharama kubwa kushinda dau la mshindani wako.