Uchaguzi 2020 Yanayotokea Tanzania Leo yalitokea Indonesia 1998

Uchaguzi 2020 Yanayotokea Tanzania Leo yalitokea Indonesia 1998

Hizi biashara za media zimeanza kipindi hiki cha Magufuli? Au wakati wa JK wapinzani walikuwa wanatangazwa bure na hizo media? Naona unashindwa kutofautisha kutangazwa sana na kukubalika. Kukubalika ni jambo linalofanyika kwa hiyari, lakini unapotangazwa sana utafahamika, bali kukubalika ni jambo jingine. Tatizo la kutangazwa ww peke yako muda wote tena kwa shuruti, pindi wanapotokea washindani wako, unakuwa kwenye wakati mgumu, maana unajikuta huna uwezo wa ushindani, na hapo ndio unaona matumizi makubwa ya nguvu, ukatili, ushenzi na uhayawani wa wazi ili utangazwe mshindi. Mfano mrahisi wa kukubalika kwa hiyo ccm ni ule upuuzi walioufanya kwenye uchaguzi wa SM. Kama kweli ccm wanakubalika, ni kipi kilimfanya rais aagize uchaguzi unajisiwe?
Mkuu bado una safari ndefu kuhusu mambo ya branding.
Unafikiri Coke au Pepsi 'hazifahamiki'?
Kwanini zinaendelea kufanya matangazo aggressively, progressively and persistently kila uchao?

Kila unapofanya tangazo hautangazi ilimradi umetangaza tu, hurudii tangazo hilihilo miaka mitano.Kuna watu wanakaa chini wapendekeza mabadiliko angalau kidogo tu hata ya kijinga kama muonekano flani au kifungashio, au ujazo n.k.
Vivyo hivyo kwenye chama unabadili vitu falani vidogo tu katika utendaji , nk, kisha unavishikia bango kwenye matangazo. Siwezi kueleza zaidi hapa sababu hiyo ni kazi na watu wanaliowa kwa hiyo kazi. Sitoi 'elimu bure' kama serikali. ..😃😃

NOTE: Zingatia kipande cha promo kwenye maandishi niliyokoleza rangi, unielewe zaidi kuhusu mfano wa tangazo lenye maboresho madongo in actual sense lakini unayashikia bango kwenye PR.
 
Endelea kujifariji wakati kuna wakulima, Askari, watumishi wa umma, vijana kila mmoja amekata tamaa ya maisha katika serikali hii.
Daaaah mbona leo mnakuwa wakweli kupitiliza na wenye akili sana
 
Indonesia ilikuwa na utawala uliojulikana kama New Order ulioendeshwa na Rais Surharto. New Order ili dumu madarakani kwa miongo mitatu, watawala walikuwa wamepumzika na hawakuangalia tena matatizo ya wananchi walala hoi.

Mwaka 1998 upinzani ulifanya campeni ya nguvu. Pamoja na New Order kuwa na jeshi, polisi na Usalama wa Taifa, ushindi wa upinzani ulikuwa mkubwa mno.

Mabadiliko makubwa ya kiutawala yalifanywa na Upinzani ulipoingia madarakani. Haikua kazi rahisi na walipitia mwaka mzima wa mtikisiko wa kuichumi. Baada ya hapo mpaka sasa hali ya siasa a uchumi iko shwari.

Mnaopenda kusoma zaidi nendeni Wikipedia msome The history of Indonesia.
We shall overcome
 
Nchi ina miaka zaidi ya 50 haina maendeleo kabsa licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, kama siyo CCM mda huu Tanzania ingekuwa ni makao makuu ya UN ingekuwa ni level ya Marekani, German, Japan, china, UK, Oman, India , Rusia na mataifa yote Tajiri yaliyosalia Duniani ikiwemo canada, korea kusini nk, Mda huu Rais wa Tanzania angekuwa ndiyo Rais wa ulimwengu akikohia Dunia nzima inatetemeka, CCM imefuja pesa nyingi kwa mambo yasiyo na tija kwa Taifa, Mfano sasa Pesa nyingi inapotelea kwenye kuwanunua wabunge madiwani kurudia chaguzi ndogo kwa gharama kubwa kuwalipa watengeneza propaganda mabilioni , cyprian Musiba ametajirika kwa mgongo wa kuihujumu kuudhofisha kudidimiza demokrasia, na endapo CCM wangezitumia hizo pesa kujenga viwanda kila kata, vyuo vikuu kila wilaya, Hosptal za rufaa kubwa zenye madaktari Bingwa kila mkoa, barabara vijijini kote, daraja toka Dsm mpaka Zanzibar na pemba, wangevuna kura pasipo kutumia nguvu kulazimisha CCM kupendwa, wananchi wanataka maendeleo kulingana na pesa zilizopo siyo kutumia pesa zao kukandamiza demokrasia.
 
Kiongozi hawezi kubadilisha uchumi wanchi kama wananchi hawajabadilika, katika mambo kadhaa, kama kufanya kazi kwa bidii, kubadili mtizamo kwa kuacha kutegemea kuajiriwa kisha kujiajiri, na kuachana na kulalamika kijiweni kwa kisigizio hakuna kazi.

Hata aje malaika kutuongoza watanzania bado tungemuona hafai kama hatujabadilika wenyewe.
 
Sijui kama watakuelewa.
Lissu hafai kuwa raisi hata kwa mwezi mmoja tu.
Akishinda uraisi itakuwa janga kwa taifa. Sijamsikia akiongea mambo yoyote ya maendeleo na huduma za kijamii.
Hadi sasa sijui kwa hakika dira au sera za chama chake ni zipi. Angalau Membe na ACT nimewasikia wakigusia mambo kadhaa muhimu tatizo utekelezaji wake utakuwa mgumu kama atafungulia kila kitu na kurudisha kama ilivyokuwa awamu ya nne.
They are just unrealistic goals.
Hivi kweli hamjuai tangu2o15 nyuma ya pazia hakuna anayeruhusiwa nchi hii kufanya siasa isipokuwa Magu peke yake?
 
Nikweli but just think Lisu Kuwa Rais? Or Member? Nadhan nibora tuongozwe na Jiwe Tu. Tunasafari ndefu Sana bado vyama vya upinzani Kuwa vyenye uwezo kutuongoza. Tutakuwa tumepoteza
Why not Lissu or Membe?
 
Kwani huyu aliyepo ndio mtu sahihi kwa maana ya mtu sahihi wa kusimamia hizo sheria? Ukishaona kiongozi ana double standard kwenye usimamizi wa sheria jua bado uko mbali na mtu sahihi.
Kubadili maadili ya watu siyo kitu rahisi, unazungumzia kuhusu kubadili tabia kitu ambacho kinakuwa hard-coded kwenye ubongo wa watu tangu wangali vijana wadogo au watoto.

Mabadiliko makubwa kama hayo yanaleta vita kubwa sana na ukaidi ambao lazima ushughulikiwe accordingly. Na hauwezi kushughulika na mambo yote na watu wote kwa wakati mmoja.
Kuna wakati mengine au wengine unawaacha ili uwatumie au uvitumie kwa muda wakati sahihi ukifika navyo unaachana navyo tu.
It's a gradual process kufanya mabadiliko ya mifumo.
 
Kiongozi hawezi kubadilisha uchumi wanchi kama wananchi hawajabadilika, katika mambo kadhaa, kama kufanya kazi kwa bidii, kubadili mtizamo kwa kuacha kutegemea kuajiriwa kisha kujiajiri, na kuachana na kulalamika kijiweni kwa kisigizio hakuna kazi.

Hata aje malaika kutuongoza watanzania bado tungemuona hafai kama hatujabadilika wenyewe.
Maana ya kurekebisha mfumo ni pamoja na kuboresha ushindani. Utakapomuona jirani yako amejenga nyumba kwa kuuza karanga, na soko la karanga lipo na wewe utalima karanga.
 
Kiongozi hawezi kubadilisha uchumi wanchi kama wananchi hawajabadilika, katika mambo kadhaa, kama kufanya kazi kwa bidii, kubadili mtizamo kwa kuacha kutegemea kuajiriwa kisha kujiajiri, na kuachana na kulalamika kijiweni kwa kisigizio hakuna kazi.

Hata aje malaika kutuongoza watanzania bado tungemuona hafai kama hatujabadilika wenyewe.
Naked truth💕💕💕
 
Kilichofanyika na JPM ni kikubwa, hata waungane tena wawaite na majirani wawasaidie hawashindi.
 
Ni kweli kabisa, cdm kukosa media zao binafsi inawagharimu. Lakini hata kama wangekuwa na media zao binafsi, bado tabia binafsi za rais huyu zingewaathiri. Kama vyama tu kama vyama hairuhusiwi kufanya mikutano au kutembea nchi nzima kusaka wanachama wapya, hata kama wangekuwa na TV stations 10, wangefanya nini zaidi ya kuishia kufungiwa? Mfano gazeti la Tanzania daima lilikuwa huru kukosoa na kuandika upande wa upinzani, leo hii liko wapi?

Narudia tena, ccm hawakujipanga chochote kwa maana halisi ya kujipanga kiushindani, bali ni kwa sababu ya unfair competition baina ya ccm na vyama vingine. Na yote hayo ni kutokana na matumizi mabaya ya madaraka ya urais. Wala usitake kunipa uchambuzi fake ambao naona fika tatizo liko wapi.
Umejiuliza kwanini Lissu mlimpokea hata baada ya katazo la jeshi la polisi na hakuzuiliwa wala kusumbuliwa?
Umejiuliza kwani sasa anaongea mengi ambayo awali alikuwa anaongea anasumbuliwa na vyombo vya kusimamia sheria?

Sasa nakuambia hata kungekuwa na vyombo vya habari vya chama siyo vya mwanachama (e.g. Mbowe) wangeona aibu kuvifungia wakati huu.
 
Mkuu bado una safari ndefu kuhusu mambo ya branding.
Unafikiri Coke au Pepsi 'hazifahamiki'?
Kwanini zinaendelea kufanya matangazo aggressively, progressively and persistently kila uchao?

Kila unapifanya tangazo hautangazi ilimradi umetangaza tu, hurudii tangazo hilihilo miaka mitano.Kuna watu wanakaa chini wapenekeza mabadiliko angalau kidogo tu hata ya kijinga kama muonekano flani au kifungashio, au ujazo n.k.
Vivyo hivyo kwenye chama unabadili vitu falani vidogo tu katika utendaji , nk, kisha unavishikia bango kwenye matangazo. Siwezi kueleza zaidi hapa sababu hiyo ni kazi na watu wanaliowa kwa hiyo kazi. Sitoi 'elimu bure' kama serikali. ..😃😃

NOTE: Zingatia kipande cha promo kwenye maandishi niliyokoleza rangi, unielewe zaidi kuhusu mfano wa tangazo lenye maboresho madongo in actual sense lakini unayashikia bango kwenye PR.

Mfano wako ni irrelevant, hao Pepsi wanafanya matangazo kwakuwa wako kwenye ushindani wa soko huria, ambapo mteja ananunua bidhaa kwa ridhaa yake. Umewahi kuwaona Pepsi wamezuia Cocacola kuuzwa mahali kisa wao pepsi walitangulia kufungua tawi eneo hilo? Huu mfano wako inaonyesha kabisa umeishiwa na hoja, ndio maana unatoa mifano isiyoendana na hali ya kisiasa tunayoijadili hapa.
 
Kubadili maadili ya watu siyo kitu rahisi, unazungumzia kuhusu kubadili tabia kitu ambacho kinakuwa hard-coded kwenye ubongo wa watu tangu wangali vijana wadogo au watoto.

Mabadiliko makubwa kama hayo yanaleta vita kubwa sana na ukaidi ambao lazima ushughulikiwe accordingly. Na hauwezi kushughulika na mambo yote na watu wote kwa wakati mmoja.
Kuna wakati mengine au wengine unawaacha ili uwatumie au uvitumie kwa muda wakati sahihi ukifika navyo unaachana navyo tu.
It's a gradual process kufanya mabadiliko ya mifumo.
Kama wakoloni waliweza kubadili mind set zetu na kukubali ku slimu na kubatizwa na kuacha kutambikia mizimu. Tulianza kwenda hospitali tukiugua badala ya kuchemsha mizizi.

Tena siku hizi kuna mass media kuelimisha wananchi inawezekana.
 
Back
Top Bottom