Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Wanakijiji unaowaongelea wewe ni wa dhana ya watu msioishi huko.Hapa naona unjivunia wanakijiji kwasababu ni rahisi kuwadhibiti wasipaze sauti zao kutokana na umasikini wao. Huko vijijini inajengwa taswira kuwa wanaikubali ccm, kwakuwa mifumo na mazingira haiwaruhusu kuweka hisia zao hadharani. Huku mjini kuna watu wengi wenye uelewa wa mambo, ndio maana ccm haijivunii, maana sio rahisi kuuongopea umma kuwa wanakubalika, hiyo ndio inayopelekea matumizi makubwa ya nguvu, ushenzi na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi maeneo ya mijini.
Laiti mazingira yangekuwa rafiki huko vijijini,hisia za wanakijiji zingekuwa wazi, lakini mazingira yaliyopo ni ngumu kwa wanakijiji kuweka hisia zao hadharani, zaidi ya wao kujifanya wanaikubali ccm kwa shingo upande. Na hata hiyo kuwa wanavijiji wanaokubali ccm sio kweli, maana wapinzani wakifika huko na kuwaamsha wote hujikuta hawaitaki ccm. Kisa cha Magufuli kupiga marufuku vyama vya siasa kuzunguka nchi nzima, ni kuhakikisha watu wa vijijini hawatoki kwenye gereza la ccm, ambalo huwa wanawatumia bila ridhaa yao.
Hivi amjajifunza kitu kutoka awamu ya tano ambapo watumishi wametakiwa kutatua kero, amjaona kwenye hizo ziara wanakijiji wanavyojielewa.
Wanakijiji halisi wanajua wanataka nini na wana demand, wanajua haki zao za msingi kama kaonewa basi atakueleza taratibu zote za kisheria alizofuata na kakwama wapi na kwa sababu zipi.
Tena wanakijiji wana uelewa wa haki zao kushinda percentage kubwa ya watu mjini. Tofauti ya watu mjini na vijijini ni priorities tu.
Sasa CCM sio mtaji wa wanavijiji eti kwa sababu wenyewe awaelewi mambo; hapana ni kwa sababu CCM aiwachukulii poa inajua wanachotaka.
Nyie nendeni huko muwaambie mnataka kuwapatia uhuru mkinyimwa kura zao sio kwa sababu awaelewi dunia inazunguka vipi; ni kwa sababu miaka yote amjawaelewa vipaumbele vyao on the basis of actual needs. CCM inawaelea na kutowachukulia poa ndio maana wana aminika zaidi.
We nenda kawaambie unataka kuwapatia uhuru halafu uone majibu yao kwenye sanduku la kura.
Halafu hakuna mkutano wa siasa uliozuiliwa isipokuwa muda wa campaign uliisha mikutano ikapigwa stop. Sasa hivi filimbi ishapigwa ruksa, ila mshaambiwa amani na utulivu kwenye mikutano sasa atutoshangaa CDM siku moja wakiamua kufanya vingine maana kauli za viongozi wao zinalenga huko.