Hii ndiyo tunaita kujifariji au kukariri.
Media maarufu zenye subscribers wengi karibu zote zinapiga safari hadi miakoani kuonesha miradi iliyofanywa na jamaa kisha wanarusha kila kitu kila kona. Wanarusha hadi miradi ya choo au jiko la shule au zahanati.
Unafikiri mtu anaye fanya hivyo ametishwa?
Fedha za hizo safari anatoa wapi?
Media zote zinafanya live coverage ya matukio ya zinduzi zote za wale wa ngazi za juu kila kona ya nchi, unataka kusema wanafanya hivyo sababu wametishwa?
Hujaliona hilo jambo toka miaka angalau mitatu iliyopita? Watu wanakula mahindi, madafu, mapapai kule forodhani ufukweni, watu wanakaa chini na walemavu wajane, wazee, migogoro ya ardhi inatolewa maamuzi papo hapo kwenye misafara, teuzi katikati ya mikutano au hotuba.
Watu wanaongeza umiliki wa media za chama kama 'Channel Kumi', n.k. wewe bado unahisi vitisho tu?
Je ninyi upinzani mmewekeza angalau redio moja ya chama ya kurusha live matangazo hadi vijijini ambako wengi hawana smart phones hawaingii mitandaoni? Msifikiri watanzania wengi wana vifaa vya kuingia na kuona matangazo mitandaoni.
Kuna mikoa maskini huko wengi hawana simu wala computer.
Hiyo ya media kutorusha mambo ya chama chenu kwenye media inaweza kuwa hoja yako na mimi naikubali huenda ni vitisho, lakini tujiulize swali.
Hivi kama media flani ina mkataba wa ku-brand chama flani na mgombea wake, na katika Terms za mkataba wao wamekubaliana ili tukupe dau hili basi usitangaze brand ya mpinzani wetu hiyo ni kosa kibiashara?
Ukumbuke media nyingi binafsi zinaendeshwa kibiashara kama biashara zingine. Ni kama vile Emirates wanafadhili Arsenal wanaweka mashariti uwanja wenu na jezi zenu marufuku kuweka au kutangaza wapinzani wetu kama Qatar au KLM, n.k.
Je, utawalaumu Arsenal kwa kutoweka matangazo ya brand hizo zingine uwanjani kwao na kwenye vipindi vya TV zao?
MY TAKE: Kutangazwa na media flani siyo hisani bali ni biashara ambayo lazima uingie gharama kubwa kushinda dau la mshindani wako.