Uchaguzi 2020 Yanayotokea Tanzania Leo yalitokea Indonesia 1998

Uchaguzi 2020 Yanayotokea Tanzania Leo yalitokea Indonesia 1998

Sijui kama watakuelewa.
Lissu hafai kuwa raisi hata kwa mwezi mmoja tu.
Akishinda uraisi itakuwa janga kwa taifa. Sijamsikia akiongea mambo yoyote ya maendeleo na huduma za kijamii.
Hadi sasa sijui kwa hakika dira au sera za chama chake ni zipi. Angalau Membe na ACT nimewasikia wakigusia mambo kadhaa muhimu tatizo utekelezaji wake utakuwa mgumu kama atafungulia kila kitu na kurudisha kama ilivyokuwa awamu ya nne.
They are just unrealistic goals.
US yenye uchumi mkubwa duniani, nchi ambayo ina miundombinu ya ku support any industry you can think of, financial institution zenye uwezo kukopesha billions of dollars to fund new investment, big business which can grow organically from retained earnings and create employments na hiyo nchi ikitengeneza ajira mpya million 1 kwa mwaka huyo raisi atajitapa sio kidogo.

Wewe huna miundombinu (ndio kwanza Magu anatengeneza tena wapinzani wanapinga), huna big business zenye uwezo wa kukuwa na kutengeneza ajira, huna bank ata moja yenye uwezo ya kukopesha bila ya mtaji wake kuyumba kampuni za size ya kati kama 100 tu zenye kuhitaji mkopo wa wastani wa dollar 10-50 zitakazoweza ajili kati ya watu 50-300.

Katika hali kama hiyo hizo ajira million 10 kwa miaka 5 mitano utazitengeneza vipi na kuna watu wanapigia vigelegele kabisa porojo za Zitto bila kuuliza how is that even possible.
 
Beberu ni hili linalotumia nguvu ya dola kubaki madarakani, Hili beberu hata mkia halina , liende zake Chato likalime ugoro , URAISI UMEMSHINDA
hizi ni akili za kuchora, kamwe hatutawahi fika popote ikiwa tutafanya mambo ajili ya kuwaridhisha mabeberu.
 
Wakati mnachukua pesa zao hamuwaiti mabeberu ,mnawata wafadhili .beberu ni babako
CCM wakienda kuomba omba misaada kwa wazungu huwapigia magoti kwa kuwaita wahisani cha ajabu hao hao wazungu wakikataa ujinga wao wote hukimbilia kuwaita wanaume wenzao mabeberu utazani CCM wao ni mbuzi jike.
 
Jamaa wamejipanga kuliko maelezo, na mipango yao imeanza takribani miaka kadhaa iliyopita.
Kwa sasa wanafanya final touches tu.

Jamaa walivyo wekeza kwenye media aina zote, na mengineyo ni hatari.
Hata ujipange vipi nguvu ya umma ikiamua hubaki
 
tindo you must face the reality vyama vingi vya upinzani havikuwekeza kwenye media. Hapa nawalaumu zaidi CHADEMA sababu walipoongeza ruzuku walitakiwa waongeze na uwekezaji kwenye media aina zote kuanzia conventional (e.g.redio, magazeti, TV) hadi digital media.
Hizo conventional media ndiyo zinawafikia watu wengi wa vijijini ambao wanaichagua CCM kwa kura nyingi kila mwaka.

Magari mliyokimbilia kununua ni machahce sana na hayawezi kuwafikia watu wengi kama hizo media za kizamani (conventional media).
Sisemi msingenunua magari bali mgewekeza basi hata kwenye kiredio cha chama mkarusha yale wanayo ogopa redio zingine kuyarusha,.
Nyie badala ya kufanya hivyo wenyewe mnawashambulia media warushe kisha wakifungiwa mnawaacha wapambane wenyewe na faini. Wale nao si wajinga ni wafanyabiashara wanataka faida siyo hasara za faini au kufungiwa kabisa kisa kufurahisha kila mtu au kila chama.
 
hizi ni akili za kuchora, kamwe hatutawahi fika popote ikiwa tutafanya mambo ajili ya kuwaridhisha mabeberu.

BANIANI BAYA KIATU CHAKE DAWA

Mnapopeleka bakuli hakuna cha beberu, Manapojisifu corona imeondoka mnawasifia waje

Mna akili nyinyi na HILO BEBERU LENU LISILO MKIA KUTOKA CHATO???
 
laiti hayo unayoyasema angeyaendeleza magufuli point yako ingekua na mashiko bt yote kayafyekelea mbali na mabeberu wamekosa upenyo ndo maana wamerudi kupitia mlango wa nyuma wapinzani..

mkuu kubali kataa mabadiliko tunayoyataka kwa sasa waafrika ili tujikomboe ni kubadili hiyo mifumo ya mabeberu wanayotuimbisha daily ajili ya maslah yao.

Chama kinachonufaika na hiyo mifumo hakitakaa kibadilishe lazima kiingie chama kingine kama ilivyokuwa Kenya ndo maana walipata hadi katiba mpya na tume huru ingekuwepo KANU hadi leo wangekuwa kwenye mfumo uleule wa utawala wa kifalme ninlazima kubadilisha chama kinachotawala ndipo tuweze kubadilisha mfumo wa utawala. Huyo Magufuli hawezi kubadilisha mifumo anatumia nguvu yake binafsi badala ya kujenga mifumo ndiyo maana watu wanamuogopa yeye badala ya kuogopa sheria hii ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Nyerere alishaonya kuhusu ubaya wa kuogopa mtawala siyo jambo zuri kabisa.
 
US yenye uchumi mkubwa duniani, nchi ambayo ina miundombinu ya ku support any industry you can think of, financial institution zenye uwezo kukopesha billions of dollars to fund new investment, big business which can grow from retained earnings and create employments na hiyo nchi ikitengeneza ajira mpya million 1 kwa mwaka huyo raisi atajitapa sio kidogo.

Wewe huna miundombinu (ndio kwanza Magu anatengeneza tena wapinzani wanapinga), huna big business zenye uwezo wa kukuwa na kutengeneza ajira, huna bank ata moja yenye uwezo ya kukopesha bila ya mtaji kuyumba kampuni za size ya kati kama 100 tu zenye kuhitaji mtaji wa wastani wa dollar 10-50 zitakazoweza ajili kati ya watu 50-300.

Katika hali kama hiyo hizo ajira million 10 kwa miaka 5 mitano utazitengeneza vipi na kuna watu wanapigia vigelegele kabisa porojo za Zitto bila kuuliza how is that even possible.
I couldn't add even a single word.
You said it all mkuu.
 
Hii ndiyo tunaita kujifariji au kukariri.
Media maarufu zenye subscribers wengi karibu zote zinapiga safari hadi miakoani kuonesha miradi iliyofanywa na jamaa kisha wanarusha kila kitu kila kona. Wanarusha hadi miradi ya choo au jiko la shule au zahanati.
Unafikiri mtu anaye fanya hivyo ametishwa?
Fedha za hizo safari anatoa wapi?

Media zote zinafanya live coverage ya matukio ya zinduzi zote za wale wa ngazi za juu kila kona ya nchi, unataka kusema wanafanya hivyo sababu wametishwa?

Hujaliona hilo jambo toka miaka angalau mitatu iliyopita? Watu wanakula mahindi, madafu, mapapai kule forodhani ufukweni, watu wanakaa chini na walemavu wajane, wazee, migogoro ya ardhi inatolewa maamuzi papo hapo kwenye misafara, teuzi katikati ya mikutano au hotuba.

Watu wanaongeza umiliki wa media za chama kama 'Channel Kumi', n.k. wewe bado unahisi vitisho tu?

Je ninyi upinzani mmewekeza angalau redio moja ya chama ya kurusha live matangazo hadi vijijini ambako wengi hawana smart phones hawaingii mitandaoni? Msifikiri watanzania wengi wana vifaa vya kuingia na kuona matangazo mitandaoni.
Kuna mikoa maskini huko wengi hawana simu wala computer.

Hiyo ya media kutorusha mambo ya chama chenu kwenye media inaweza kuwa hoja yako na mimi naikubali huenda ni vitisho, lakini tujiulize swali.
Hivi kama media flani ina mkataba wa ku-brand chama flani na mgombea wake, na katika Terms za mkataba wao wamekubaliana ili tukupe dau hili basi usitangaze brand ya mpinzani wetu hiyo ni kosa kibiashara?
Ukumbuke media nyingi binafsi zinaendeshwa kibiashara kama biashara zingine. Ni kama vile Emirates wanafadhili Arsenal wanaweka mashariti uwanja wenu na jezi zenu marufuku kuweka au kutangaza wapinzani wetu kama Qatar au KLM, n.k.
Je, utawalaumu Arsenal kwa kutoweka matangazo ya brand hizo zingine uwanjani kwao na kwenye vipindi vya TV zao?

MY TAKE: Kutangazwa na media flani siyo hisani bali ni biashara ambayo lazima uingie gharama kubwa kushinda dau la mshindani wako.

Hizi biashara za media zimeanza kipindi hiki cha Magufuli? Au wakati wa JK wapinzani walikuwa wanatangazwa bure na hizo media? Naona unashindwa kutofautisha kutangazwa sana na kukubalika. Kukubalika ni jambo linalofanyika kwa hiyari, lakini unapotangazwa sana utafahamika, bali kukubalika ni jambo jingine. Tatizo la kutangazwa ww peke yako muda wote tena kwa shuruti, pindi wanapotokea washindani wako, unakuwa kwenye wakati mgumu, maana unajikuta huna uwezo wa ushindani, na hapo ndio unaona matumizi makubwa ya nguvu, ukatili, ushenzi na uhayawani wa wazi ili utangazwe mshindi. Mfano mrahisi wa kukubalika kwa hiyo ccm ni ule upuuzi walioufanya kwenye uchaguzi wa SM. Kama kweli ccm wanakubalika, ni kipi kilimfanya rais aagize uchaguzi unajisiwe?
 
US yenye uchumi mkubwa duniani, nchi ambayo ina miundombinu ya ku support any industry you can think of, financial institutions, big business which can grow and create employment na nchi ikitengeneza ajira mpya million 1 kwa mwaka huyo raisi atajitapa sio kidogo.

Wewe huna miundombinu (ndio kwanza Magu anatengeneza tena wapinzani wanapinga), huna big business zenye uwezo wa kukuwa na kutengeneza ajira, huna bank ata moja yenye uwezo ya kukopesha kampuni za size ya kati kama 100 tu zenye kuhitaji mtaji wa wastani wa dollar 10-50 zitakazoweza ajili kati ya watu 50-300.

Katika hali kama hiyo hizo ajira million 10 kwa miaka 5 mitano utazitengeneza vipi na kuna watu wanapigia vigelegele kabisa porojo za Zitto bila how kuuliza how is that possible.
Acha ujinga wapinzani hawana porojo bank mitaji siyo kazi ya chama hivyo vipo endapo chama chochote kikiunda Serikali huviwezesha kuimarika na kuendelea, kazi ya upinzani ni nini? Kazi ya upinzani ni kukosoa kupinga mabaya ya Serikali iliyopo madarakani, hana miradi ya CCM isiyo na mapungufu ufisadi, kasoro ndiyo maana upinzani huwapinga kwa 100% Maendeleo siyo Hisani za CCM na maendeleo siyo pesa binafsi toka mfukoni mwa mtukufu, maendeleo ni pesa za walipa kodi ambao wengi ni wapinzani na wananchi wasio na vyama, cha ajabu wanaccm ndiyo wanufaika wa 10% kwenye miradi yote mikubwa lazima upinzani upige kelele kwa mabaya yote pasipo kubagua kitu.
 
Kwani hao wanaoongelea mambo ya maendelea kila siku wameleta maendeleo gani. Hapa tunahitaji mtu wa kubadilisha mfumo mzima wa utawala ili watu waogope sheria siyo kuogopa mtu na hili linawezekana kama tutakuwa na mihimili iliyo imara isiyoegemea muhimili mwengine yakitatuliwa hayo ndipo tutapata maendeo. Huku kutiana hofu na kunyamazisha vyombo vya habari hakuwezi kutufikisha tunakokwenda. Tunataka maendeleo ya watu na hayawezi kupatikana kama watu hawaishi kwa uhuru katika nchi yao.
Kwani sasa hakuna sheria zinazo kataza rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma?
Hakuna sheria inayokataza matumizi mabaya ya madaraka?

Umejiuliza kwanini sheria hizo hazijafanya kazi zake hapa nchini kwa miaka mingi?
Ukiapata majibu ndiyo utajua tatizo letu ni zaidi ya uwepo wa sheria au vyombo vyovyote vya kusimamia hizo sheria.

Tatizo letu ni kupata watu sahihi wa kuziendesha hizo taasisi mnazotaka ambao baadhi ya waliopita au baadhi ya waliopo hawana utashi na maadili ya kuendesha hizo taasisi. Taasisi ni watu, mifumo inaendeshwa na watu, kwa hivyo ukikosa watu wenye moyo, hari na maadili sahihi hata uwe na mifumo (taasisi) gani bado hizo taasisi hazitafanya kazi iliyokusudiwa kwa ufanisi mkubwa.
 
Ndio maana Mkapa aliwaita wapinzani marofa na wapumbavu, huo mfumo unaotaka utaongozwa na maroboti, ndg mifumo ipo mzuri tu ila tulikuwa akuna msimamizi sahihi kusimamia, na ndio tatizo la Tanzania, mfno hapo juzi wakati Rais anatoka mtwara anafika kibiti anakutana na watu wanasema hawana choo zaidi ya miaka huku wanakusanya bilion 1.8, gari la kubeba wagonjwa limepaki Kwa kukosa tairi, naili nalo linaitaji mfumo Hipi? Ungesema tunaitaji viongozi wenye uthubutu maana hata kama kutakuwa na mfumo mzuri nanma hipi kama kiongozi atakuwa hana utashi mfumo utakwama maana haujiongozi
 
tindo you must face the reality vyama vingi vya upinzani havikuwekeza kwenye media. Hapa nawalaumu zaidi CHADEMA sababu walipoongeza ruzuku walitakiwa waongeze na uwekezaji kwenye media aina zote kuanzia conventional (e.g.redio, magazeti, TV) hadi digital media.
Hizo conventional media ndiyo zinawafikia watu wengi wa vijijini ambao wanaichagua CCM kwa kura nyingi kila mwaka.

Magari mliyokimbilia kununua ni machahce sana na hayawezi kuwafikia watu wengi kama hizo media za kizamani (conventional media).
Sisemi msingenunua magari bali mgewekeza basi hata kwenye kiredio cha chama mkarusha yale wanayo ogopa redio zingine kuyarusha,.
Nyie badala ya kufanya hivyo wenyewe mnawashambulia media warushe kisha wakifungiwa mnawaacha wapambane wenyewe na faini. Wale nao si wajinga ni wafanyabiashara wanataka faida siyo hasara za faini au kufungiwa kabisa kisa kufurahisha kila mtu au kila chama.

Ni kweli kabisa, cdm kukosa media zao binafsi inawagharimu. Lakini hata kama wangekuwa na media zao binafsi, bado tabia binafsi za rais huyu zingewaathiri. Kama vyama tu kama vyama hairuhusiwi kufanya mikutano au kutembea nchi nzima kusaka wanachama wapya, hata kama wangekuwa na TV stations 10, wangefanya nini zaidi ya kuishia kufungiwa? Mfano gazeti la Tanzania daima lilikuwa huru kukosoa na kuandika upande wa upinzani, leo hii liko wapi?

Narudia tena, ccm hawakujipanga chochote kwa maana halisi ya kujipanga kiushindani, bali ni kwa sababu ya unfair competition baina ya ccm na vyama vingine. Na yote hayo ni kutokana na matumizi mabaya ya madaraka ya urais. Wala usitake kunipa uchambuzi fake ambao naona fika tatizo liko wapi.
 
Acha ujinga wapinzani hawana porojo bank mitaji siyo kazi ya chama hivyo vipo endapo chama chochote kikiunda Serikali huviwezesha kuimarika na kuendelea, kazi ya upinzani ni nini? Kazi ya upinzani ni kukosoa kupinga mabaya ya Serikali iliyopo madarakani, hana miradi ya CCM isiyo na mapungufu ufisadi, kasoro ndiyo maana upinzani huwapinga kwa 100% Maendeleo siyo Hisani za CCM na maendeleo siyo pesa binafsi toka mfukoni mwa mtukufu, maendeleo ni pesa za walipa kodi ambao wengi ni wapinzani na wananchi wasio na vyama, cha ajabu wanaccm ndiyo wanufaika wa 10% kwenye miradi yote mikubwa lazima upinzani upige kelele kwa mabaya yote pasipo kubagua kitu.
Kwa ivyo hizo ajira mpya million 10 za ACT zitatokea serikalini? Au ni kwa namna gani haswa zitatengenezwa embu tusaidie?

Kugusia mambo mengine ya Ilani yao ata shida ni vitu tu vya kujiandikia tu ni sawa na mtu mwenye mshahara wa million 2 kwa mwezi anaetoa ahadi ya kupanga nyumba ya vyumba vitano masaki, kusomesha watoto wawili Feza, kununua Range Vogue la 2016, etc na watu wanasifia jamaa ana mipango mizuri japo wanafahamu mshahara wake.

It requires matching financial resources to accomplish an economic plan, sasa lazima useme na hizo mbinu zako, vinginevyo ni wishful thinking ndio ilani yote ya ACT Wazalendo.
 
Ndio maana Mkapa aliwaita wapinzani marofa na wapumbavu, huo mfumo unaotaka utaongozwa na maroboti, ndg mifumo ipo mzuri tu ila tulikuwa akuna msimamizi sahihi kusimamia, na ndio tatizo la Tanzania, mfno hapo juzi wakati Rais anatoka mtwara anafika kibiti anakutana na watu wanasema hawana choo zaidi ya miaka huku wanakusanya bilion 1.8, gari la kubeba wagonjwa limepaki Kwa kukosa tairi, naili nalo linaitaji mfumo Hipi? Ungesema tunaitaji viongozi wenye uthubutu maana hata kama kutakuwa na mfumo mzuri nanma hipi kama kiongozi atakuwa hana utashi mfumo utakwama maana haujiongozi
Kama mifumo ipo tunahitaji serikali itayaoweza kuikarisha Law and Order na kwanini miaka 60 ya itawala wa CCM hilo limeshindikana?
 
Indonesia ilikuwa na utawala uliojulikana kama New Order ulioendeshwa na Rais Surharto. New Order ili dumu madarakani kwa miongo mitatu, watawala walikuwa wamepumzika na hawakuangalia tena matatizo ya wananchi walala hoi.

Mwaka 1998 upinzani ulifanya campeni ya nguvu. Pamoja na New Order kuwa na jeshi, polisi na Usalama wa Taifa, ushindi wa upinzani ulikuwa mkubwa mno.

Mabadiliko makubwa ya kiutawala yalifanywa na Upinzani ulipoingia madarakani. Haikua kazi rahisi na walipitia mwaka mzima wa mtikisiko wa kuichumi. Baada ya hapo mpaka sasa hali ya siasa a uchumi iko shwari.

Mnaopenda kusoma zaidi nendeni Wikipedia msome The history of Indonesia.
Nione PM
 
Kwani sasa hakuna sheria zinazo kataza rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma?
Hakuna sheria inayokataza matumizi mabaya ya madaraka?

Umejiuliza kwanini sheria hizo hazijafanya kazi zake hapa nchini kwa miaka mingi?
Ukiapata majibu ndiyo utajua tatizo letu ni zaidi ya uwepo wa sheria au vyombo vyovyote vya kusimamia hizo sheria.

Tatizo letu ni kupata watu sahihi wa kuziendesha hizo taasisi mnazotaka ambao baadhi ya waliopita au baadhi ya waliopo hawana utashi na maadili ya kuendesha hizo taasisi. Taasisi ni watu, mifumo inaendeshwa na watu, kwa hivyo ukikosa watu wenye moyo, hari na maadili sahihi hata uwe na mifumo (taasisi) gani bado hizo taasisi hazitafanya kazi iliyokusudiwa kwa ufanisi mkubwa.

Kwani huyu aliyepo ndio mtu sahihi kwa maana ya mtu sahihi wa kusimamia hizo sheria? Ukishaona kiongozi ana double standard kwenye usimamizi wa sheria jua bado uko mbali na mtu sahihi.
 
Indonesia ilikuwa na utawala uliojulikana kama New Order ulioendeshwa na Rais Surharto. New Order ili dumu madarakani kwa miongo mitatu, watawala walikuwa wamepumzika na hawakuangalia tena matatizo ya wananchi walala hoi.

Mwaka 1998 upinzani ulifanya campeni ya nguvu. Pamoja na New Order kuwa na jeshi, polisi na Usalama wa Taifa, ushindi wa upinzani ulikuwa mkubwa mno.

Mabadiliko makubwa ya kiutawala yalifanywa na Upinzani ulipoingia madarakani. Haikua kazi rahisi na walipitia mwaka mzima wa mtikisiko wa kuichumi. Baada ya hapo mpaka sasa hali ya siasa a uchumi iko shwari.

Mnaopenda kusoma zaidi nendeni Wikipedia msome The history of Indonesia.
Thanks sister! Tatizo hawa jamaa kuishi kimazoea inawadanganya sana. Wanajisahaulisha makusudi uchaguzi huu una watu wengi sana wameumizwa na familia zao kuanzia wakulima, wanafunzi vyuo vikuuu, watumishi wa umma. Mjipange mwaka huu ni wakura za hasira, muondoke na mpotee kabisa, mnatia kichefuchefu.
 
Back
Top Bottom