Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Kwa masiku kadhaa kumekuwa na posts ambazo zinanasibisha na Maandamano yanayo tokea Ulaya kuwa yanachagizwa na uwepo wa wahamajia kutoka nchi za kiarabu
Labda niwaulize hawa wajinga wachache,je source ya habari zenu huwa mnatoa wapi wenzetu?
Nikisema kwamba habari zenu zinachagizwa na chuki yenu dhidi ya Uislamu je,nitakuwa nakosea?
Uislamu pamoja na kuchukiwa na hii inatokana na propaganda ambazo zinapandikizwa duniani kote,lakini kwa uwezo wa Allah bado Uislamu upo imara na kila kukicha wafuasi wapya wanazidi kuijua dini hii na kuwa waislamu kutokana na hoja zenye akili zenye kukinaisha nafsi ya mwanadamu na kuujua ukweli
Mambo ambayo yanatokea Ulaya yapo wazi,ikiwemo hali ngumu ya maisha ya wananchi walio wengi
Ufadhili mdogo wa masomo kwa vijana wanaosoma shule na vyuoni
Kipato cha wananchi kuwa kidogo kiasi kwamba mtu anaweza kufanya ajira mbili na kipato chake hakifiki mwisho wa mwezi
Hayo ni kwa uchache tu,na hali hii imechagizwa zaidi na serikali zao kutakiwa kuchangia fedha zao kwenye jeshi la Nato tofauti na awali ambapo Marekani peke yake ndio alikuwa mchangiaji mkuu
Sasa serikali zao zinapata changamoto za kufadhili mambo yao ya ndani,halafu wanatokea wajinga wachache hapa jf na kuhamishia lawama kwa wahamiaji wa kiislamu.
Kuna wajinga wengine wanaweza kuuliza mbona huko nyuma maandamano hayakuwa na sura ya fujo na machafuko?
Je,mnadhani kila siku mambo yanaweza kuwa sawa tu,siku hizi Gen Z ndio wako front kwenye maandamano mengi,je hiki kizazi unafikiri kinaendeshwa na nini Kama sio hisia zao na utashi wao?
Acheni ujinga,think big
Ni hayo tu!