Yanga akili kubwa, kuleta jezi mpya ni kukomesha wezi wa jezi feki

Nani amekwambia hizi za Sasa watu watazinunua nyingi na gsm kupata faida?
 
Yanga alitoa jezi mbovu,kaona simba kalikamata soko wanakuja na ngonjera ya jezi mpya kudhibiti fake?sasa hizo nzao wakitoa fake?Utopolotafatua nyingine tena.

Yaan utopolo wanamini kwamba kupambana na fake ni kuzalisha nyingine,basi mzalishaji fake ndio atanufaika sana.
 
Kumkomesha jezi feki labda hizo jezi og muwe mnaziuza Tsh.10,000/= au chini ya hapo. Kwa maisha yalivyokaza watu huku Uswahilini na mikoani wako tayari kununua jezi feki ya 15,000/= kuliko original ya 40,000/=.

Kudhibiti jezi feki ni jambo lisilowezekana kwa hii nchi iliyooza.
 
Dawa nyingine ya Yanga kumkomesha jezi feki ni kucheza wakiwa tumbo/gongo wazi kama miaka ile. Warudie tu ile Historia yao.

Otherwise sisi wafyatua jezi fake tutazitengeneza hizo fake kila wakitoa toleo jipya.
 
Umemaliza kila kitu, shida sio ubora wa jezi, ni bei ya hiyo jezi.
Watu wengi hawaimudu, ndo watahamia kwa fake tyuuh.
 
Kilichofanyika ni ujinga wa hali ya juu!

Kwa vile mzigo umeisha kwao,hakukuwa na umuhimu wa kuzikandia ilhali bado mzigo huo umejaa madukani.

Ukiangalia maoni ya watu kwenye page ya Vunjabei baada ya kutangaza huo mzigo wa awali anao wa kutosha utaona jinsi anaenda kula hasara!!
 
Mkuu; unaelewa maana ya jezi fake?

Unaelewa athari ya hizo jezi fake kuwa mtaani?

Unaelewa hasara inayopatikana kwa kuacha jezi fake ziendelee kuwa mtaani bila kuchukua hatua yoyote?

Au tuendelee kuwaamini na kuwasikiliza Manara Sr. na JK tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…