Yanga akimfunga TP Mazembe naacha rasmi kushabikia mpira

Yanga akimfunga TP Mazembe naacha rasmi kushabikia mpira

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Ndugu zangu sioni ni jinsi gani Yanga atamfunga giant TP Mazembe hapo Jumapili.

Kwa aina ya uchezaji wa Yanga wa kutegemea goli kipa afanye makosa ndio washinde siioni hiyo nafasi Jumapili.

C8DB97AA-9A47-434C-B875-96302DB575E5.jpeg
 
Vipi kuhusu Simba itashinda au ndo kama Yanga!
Simba itashinda hilo sina wasi wasi kabisa

Hata mechi ya jana haikufaa iishe vile basi tu ni bahati

Ila hii ya Yanga huwezi kusema bahati kwasababu uwezo wa wachezaji ndio ulioamua mechi kuliko mbinu za kocha

Yanga sijaona shambulizi la hatari iliyofanya kiasi wapate kauli ya kusema ni bahati iliwabeba Monastr
 
Yanga wana dominate mpira lakini hawapeleki pressure kwenye timu pinzani

Wanaweza kushinda home lakini natabiri ugumu
Kuna namna kocha anatakiwa afanye katika mifumo yake ya uchezeshaji timu. Inafanya mashambulizi kunakuwa na idadi ndogo sana ya wachezaji kwenye box la mpinzani. Na pia akubaliane na hali kuwa Farid, Moloko na Kisinda sio mawinga ni wazuraji hivyo ajipange kwa namna nyingine
 
Simba itashinda hilo sina wasi wasi kabisa

Hata mechi ya jana haikufaa iishe vile basi tu ni bahati

Ila hii ya Yanga huwezi kusema bahati kwasababu uwezo wa wachezaji ndio ulioamua mechi kuliko mbinu za kocha

Yanga sijaona shambulizi la hatari iliyofanya kiasi wapate kauli ya kusema ni bahati iliwabeba Monastr
Mh basi hata mechi ya Yanga haikufaa kuisha vile, ilipaswa iwe sare ya bila bila maana hakuna mpira wowote wa ajabu wa monastir zaidi kutegemea ufupi wa akina Kibwana.
 
Simba itashinda hilo sina wasi wasi kabisa

Hata mechi ya jana haikufaa iishe vile basi tu ni bahati..
Sawa maoni yako ni hayo ila kwa upande wangu baada ya kuangalia mechi ya Jana na Leo, timu ya Jana ina uwezo mdogo kuliko inayokuja Raja, vilevile timu ya leo nayo sidhani kama ina uwezo kuliko Tp mazembe kwa hiyo naamini kwamba mechi zijazo Simba na Yanga hawawezi kushinda. Mechi tatu za mwanzo timu zetu zitaishia kupata point mojamoja tu kwa kutoa sare kule vipers na bamako
 
Kuna namna kocha anatakiwa afanye katika mifumo yake ya uchezeshaji timu. Inafanya mashambulizi kunakuwa na idadi ndogo sana ya wachezaji kwenye box la mpinzani. Na pia akubaliane na hali kuwa Farid, Moloko na Kisinda sio mawinga ni wazuraji hivyo ajipange kwa namna nyingine
Ila leo Kisinda alikuwa na bahati ya kukutana na mipira katika nafasi nzuri tena akiwa peke yake lakini maamuzi yake ya mwisho yalikuwa poor

Ila nilichokiona kwa game hizi mbili naona kuna haja kubwa ya kujinoa na mipira ya kutengwa

Kama tumeshindwa kocha basi tusajili wachezaji wazuri wanaocheza kwa ufanisi mipira hiyo.

Kabla ha game ya jana Simba nilimsikia Ahmedy Ally akisema kuwa kuna mchezaji namba 26 wanayemtazama kwa umakini kutokana na uwezo wake wa mipira iliyokufa

Wakati wa game nilipomuona anapiga ile freekick na kwa jinsi ulivyofika kwa hesabu nikasema kweli hii ndio role ya mchezaji anayostahili kusifika nayo.

Ligi yetu hatuna mtu wana namna hiyo, tunao wapigaji wa msimu na wengi kulingana na ubovu wa ukuta uliopangwa
 
Mh basi hata mechi ya Yanga haikufaa kuisha vile, ilipaswa iwe sare ya bila bila maana hakuna mpira wowote wa ajabu wa monastir zaidi kutegemea ufupi wa akina Kibwana.
Yap unaweza ukasema hivyo pia

Ila wale jamaa kwenye mipira ya kutengwa ni balaa, hata defense ingekuwa na watu warefu lingefungwa goli na tungejadili tatizo lingine na sio ufupi tena
 
Back
Top Bottom