Yanga alipata magoli mawili halali huku Simba ikipata moja leo pale kwa Mkapa

Execute

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
3,000
Reaction score
7,336
Nilichokiona baada ya kuangalia marudio

1. Yanga kafunga magoli halali mawili ambayo ni lile la kwanza na la tatu. Kwahiyo Yanga anastahili kupongezwa kwa ushindi.

2. Goli la pili la Yanga kulikuwa na faulo kabla mpira haujachukuliwa, goli la nne kulikuwa na offside ya mchezaji aliyetoa pasi ya pili kabla ya ile ya mwisho.

3. Inonga aliugusa mpira kwenye box hivyo Ile penati haikuwa halali.

4. Simba ina wachezaji wazee, wamepitwa na wakati. Waachane na akina Bocco, Hussein, Chama, Kapombe na Ntibazonkiza.

Kisasi cha 5 kimelipwa, bado kile cha 4 na cha 6.
 
Kalime Dengu tu, uchambuzi haukufai

4 tu ndio point
 
Ukisikia kuchanganyikiwa ndio huku, kweli aliyetoa msemo wa "MPAKA USEME" kwenye hii derby aliwaza mbali. Kila mtu anakuja na nyuzi za kutapa tapa mwingine ana dai kuwa kuna usaliti, wewe nawe unekuja na magoli sio halali. Hakuna anayetaka kukubali kuzidiwa, tufanye hizo sababu zote ni sahihi hivyo tumalize mjadala Simba ni timu bora iliyokamilika Yanga wamepata magoli kwa msada wa wasaliti na waamuzi. Mficha maradhi...........
 
Mmh ngoja tuanze kukupinga kwa hoja
1.Magoli yote ya YANGA ni halali...
2.Goli la 2 sio faulo ukiangalia mech ya Yanga vs Azam goli la 3 au unaangaliaga bundesliga au uefa refa analeta tu sio KILA kitu filimbi......Naongezea unakumbuka faulo MUdathiri kadakwa mguu na kapombe kwenye box ile ilikuwa ni kitu ganii?????(CLEAR penalty)) ila refa alivunga tu
3.Angalia vizuri inonga aligusa mguu wa max kwanza mpira hajaugusa
4.Wachezaji wazee Wana umuhimu ila kuwaondoa kwenye timu ni taratibu taratibu kama Guardiola anavofanyaga kutafuta back up
 
Gamond nae katili mno. Badala ya kurusha fataki yeye kawatupia NYUKILIA
 
Mimi nimeandika nilichokiona na sio suala la ushabiki.
 
Kosa likifanyika mechi moja halihalalishwi kwenye mechi nyingine.
 
Hii nchi kazi rahisi kuliko zote ni uchambuzi wa soka.
 
Huku akipepesuka,aliendelea kujifariji kuna kipigo cha 5,sijui 6. Unasahau ulitanguliwa kugongwa 6 na YANGA. Au unajichomoa fiuz dada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…