1. Kuna mtu alitoa utabiri mechi ya IHEFU vs YANGA, mwanzoni alianza kwa kutukanwa ila mwishoni watu wakampa maua yake. Inaonyesha wengi humu ni Matomaso au wenye ujuaji wa hovyo siyo?
2.Kisa cha kifo cha JPM kilishasababisha nisiwe nawabishia sana watu,kama nina mashaka bora nikae kimya tu. Kama mtakumbuka, kabla hata ya Uchaguzi Mkuu 2020 kuna watu walishauri ingekuwa vyema JPM asingegombea tena maana hangemaliza mhula wake wa pili. Ila wabishi tukawatukana na kuwazodoa watabiri wale. Mambo yalivyotokea kama ilivyotabiriwa threads zikaanza kufufuliwa. Huwa tunasubiri hadi itokee eeeh?
3.Kitendo cha Simba kukipeleka kijezi chake kileleni mwa Mt.Kilimanjaro ni kiko ki spiritual zaidi. Na tahadhari ilishatolewa.